Wanaume wanaojihusisha na Mapenzi ya Jinsia moja ruksa kujiunga na Upadre

Wanaume wanaojihusisha na Mapenzi ya Jinsia moja ruksa kujiunga na Upadre

Heading haijakaa vizuri. Unaliaibisha kanisa.
Pole sana aisee,
Kuamini kwako au kutokuamini hakuwezi kuubadili ukweli,

Fuateni imani zenu bila kuongozwa na hao wazungu,wanawapotosha,
Wanatumia dini kuhalalisha ushoga,kitu ambacho hakikubaliki,

Taasisi moja inapoanza kubariki na kusupport ushoga sio jambo jema kwa jamii zote,coz huko mbele itaonekana kua ushoga ni jambo la kawaida tu,

Watu wote bila kujali imani zao na tofauti zao, wanatakiwa kuungana na kupinga hizi ajenda za wazungu kusambaza ushoga kwa kutumia dini.
 
Hili ni dhehebu langu KANISA MOJA TAKATIFU KATOLIKI LA MITUME ila Sasa hii ni too much.
Nafikiri ifike wakati Africa sasa ijitenge na Vatican iwe African Catholic na sio Roman Catholic.
Tuwe na kanisa linalodumisha Mila, tamaduni na desturi zetu sisi kama Waafrika.
Makadrinali na Maaskofu wa Africa huu ndio wakati wenu wa kuchora mstari mwekundu.
Umeongea kitu cha maana sana Mkuu.
 
Watanzania tuna unafiki. Hata mwezi haujapita, shoga maarufu nchini aitwaye Aggrey ameokoka na kupokelewa kwa walokole, na anafanyiwa mpango akasomee uchungaji
wa kanisa gani huyo aggrey?
 
wa kanisa gani huyo aggrey?
Sijajua jina la kanisa, ila ni la kipentekoste

1737003422255.png
 
Huyu papa ndio mpinga Kristo mwenyewe
Usiingie katika mtego. Kama elimu yako ni walau kidato cha sita kwenda juu, soma content uelewe. Lakini kama ni chini ya kidato cha sita, basi subiri utafsiriwe
 
Soma maelezo uelewe mwenyewe, usiburuzwe na tafsiri ya mtu. Title ya uzi hutegemea uamuzi na dhamira ya mleta mada, na wakati mwingine elimu
Hii habari ingekua inahusu dini ya kiislam ungecomment pumba pasipo kufuata maelezo
 
Kanisa linazidi kujichanganya,tutaona mengi,hii ni sawa na kuruhusu unywe pombe lkn usilewe, wakati pombe tayari inakilevi!!,hawa jamaa wanastaajabisha!!
 
Usiingie katika mtego. Kama elimu yako ni walau kidato cha sita kwenda juu, soma content uelewe. Lakini kama ni chini ya kidato cha sita, basi subiri utafsiriwe
unadhani kila aliyeishia form four hajui kiingereza vema? Una mtazamo finyu
 
unadhani kila aliyeishia form four hajui kiingereza vema? Una mtazamo finyu
Wapo watu wengi tu nchini wanajua kusoma na kuandika kiarabu lakini hawajui tafsiri zake hadi watafsiriwe
 
Mimi naomba kuulizia la kizushi:
1. Mwizi hawezi kuja kuwa padri, mchungaji au shehe?
2. Muongo hawezi kuja kuwa padri, mchungaji au shehe?
3. Muuaji hawezi kuja kuwa padri, mchungaji au shehe?
4. Mzinzi hawezi kuja kuwa padri, mchungaji au shehe?
5. Mshirikina hawezi kuja kuwa padri, mchungaji au shehe?
6. Anayetamani mali au mke wa mtu hawezi kuja kuwa padri, mchungaji au shehe?

Kwa nini ushoga unaonekana kama 'dhambi maalum' na kwamba haistahili kusamehewa na binadamu?
Kwa wenye akili za juu tu wanaelewa hili.
 
Soma mwenyewe hapo uelewe ndugu, usiogozwe na kichwa cha habari maana mleta mada anaweza akawa hajui lugha
Hakuna cha lugha ngeni hapo, Vatican imeruhusu kiangalifu wanaume wanao/waliowahi kushughulikiwa au wabomoaji kujiunga na useminary ili waje kuwa mapadri kwa sharti la wao kuacha ukundufu.
Kuficha ficha core problem kwa kisingizio cha watu kuwa hawajaelewa lugha ni ama kushiriki au kufumbia macho ussengen huo.
 
Usiingie katika mtego. Kama elimu yako ni walau kidato cha sita kwenda juu, soma content uelewe. Lakini kama ni chini ya kidato cha sita, basi subiri utafsiriwe
Unatetea ushoga?
 
🙂 🙂 🙂 🙂 wale wakatoliki wa kazuramimba sijui wapo kwenye hali gani. Bado sijutii uamuzi wangu wa kuachana kabisa na mambo ya dini hususani ukatoliki.

NB: nimekuwa kijana wa altareni kwa zaidi ya miaka 9

 
Back
Top Bottom