Wanaume wanaongoza kwa kujiua kila mwaka Tanzania

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kila mwaka Septemba 10, Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kuzuia Kujitoa Uhai Duniani, huku wataalamu wa afya ya akili wameeleza kuwa tatizo hilo limekuwa tishio kubwa nchini hususan kwa vijana.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Septemba 10, 2025 katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Lawala amesema kundi kubwa la watu wanaotaka kujiua au wanaojiua ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 29.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2018 mtu mmoja alifariki kwa kujitoa uhai kila baada ya sekunde 40 duniani, huku kiwango cha wastani kikiwa ni watu 720,000 kwa mwaka.

Katika kipindi hicho, takwimu za WHO zilionesha kuwa zaidi ya watu 3,000 nchini Tanzania walijaribu kujiua au kufariki kwa kujitoa uhai. Njia zinazotumika mara nyingi ni kula sumu, kujinyonga, na matumizi ya silaha, huku sababu zikihusiana na mchanganyiko wa hali za kibaolojia, kisaikolojia, kijamii, upweke, magonjwa sugu na matumizi ya vilevi.

Dkt. Lawala, ameongeza kuwa kati ya Januari hadi Desemba 2024 na Januari hadi Julai 2025, Tanzania imerekodi matukio 1,141 ya kujitoa uhai, jambo linalothibitisha ukubwa wa tatizo na umuhimu wa hatua za haraka.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Thomas Rutachunzibwa, amesema familia nyingi zinakabiliwa na changamoto za migogoro na mahusiano, hali inayochangia matukio ya kujitoa uhai.

Ameitaka jamii kuishi kwa upendo na mshikamano ili kupunguza tatizo hilo. Pia amewashauri watumishi wa afya na wananchi kwa ujumla kutafuta vyanzo mbadala vya kipato ili kuepuka msongo wa mawazo unaotokana na changamoto za kiuchumi.

Ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa wanaume wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kujitoa uhai kwa sababu mara wanapochukua maamuzi ya kujiua, hutekeleza moja kwa moja tofauti na wanawake ambao mara nyingi hueleza changamoto zao kabla ya kuchukua hatua

Chanzo: Jambo TV
 
Ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa wanaume wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kujitoa uhai kwa sababu mara wanapochukua maamuzi ya kujiua, hutekeleza moja kwa moja tofauti na wanawake ambao mara nyingi hueleza changamoto zao kabla ya kuchukua hatua.

Ndio maana tunatengenezewa kila aina ya vilevi ili kutusaidia kupunguza msongo wa mawazo.
 
Kufa na tai shingoni kwa madai wewe ni kidume ni bora uje hapa ubwatuke itakusaidia pia
Mwaga maumivu yako hapa jamvini Kuna watakaokuunga mkono wengine watakupinga itakupa guts za kusonga mbele na kujua hauko pakee yako katika shida uliyonayo.
 
Kila mwaka Septemba 10, Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kuzuia Kujitoa Uhai Duniani, huku wataalamu wa afya ya akili wameeleza kuwa tatizo hilo limekuwa tishio kubwa nchini hususan kwa vijana.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Septemba 10, 2025 katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Lawala amesema kundi kubwa la watu wanaotaka kujiua au wanaojiua ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 29.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2018 mtu mmoja alifariki kwa kujitoa uhai kila baada ya sekunde 40 duniani, huku kiwango cha wastani kikiwa ni watu 720,000 kwa mwaka.

Katika kipindi hicho, takwimu za WHO zilionesha kuwa zaidi ya watu 3,000 nchini Tanzania walijaribu kujiua au kufariki kwa kujitoa uhai. Njia zinazotumika mara nyingi ni kula sumu, kujinyonga, na matumizi ya silaha, huku sababu zikihusiana na mchanganyiko wa hali za kibaolojia, kisaikolojia, kijamii, upweke, magonjwa sugu na matumizi ya vilevi.

Dkt. Lawala, ameongeza kuwa kati ya Januari hadi Desemba 2024 na Januari hadi Julai 2025, Tanzania imerekodi matukio 1,141 ya kujitoa uhai, jambo linalothibitisha ukubwa wa tatizo na umuhimu wa hatua za haraka.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Thomas Rutachunzibwa, amesema familia nyingi zinakabiliwa na changamoto za migogoro na mahusiano, hali inayochangia matukio ya kujitoa uhai.

Ameitaka jamii kuishi kwa upendo na mshikamano ili kupunguza tatizo hilo. Pia amewashauri watumishi wa afya na wananchi kwa ujumla kutafuta vyanzo mbadala vya kipato ili kuepuka msongo wa mawazo unaotokana na changamoto za kiuchumi.

Ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa wanaume wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kujitoa uhai kwa sababu mara wanapochukua maamuzi ya kujiua, hutekeleza moja kwa moja tofauti na wanawake ambao mara nyingi hueleza changamoto zao kabla ya kuchukua hatua

Chanzo: Jambo TV
KATAA NDOA. NDOA NI ULAGHAI NA UTAPELI.
 
Matatizo ya afya ya akili , hata humu jf ukichunguza kwa umakini afya ya akili ni tatizo , mtu anarupuka tu anaanza makasiriko ma matusi bila sababu ya msingi , tatizo ni kubwa 🤔
Najua unamaanisha Ritz houthi na mi hamas ikibinywa jamaa anaingia jamvini na makasiriko na kutupiako malink uchwara na ya kutunga kutoka twitter.
 
Back
Top Bottom