Wanaume wanaovaa cheni na hereni wanataka nini?

Mkuu kuwa msafi kukata kucha nywele inatosha..ila cheni na nini ni femenine behavior..sidhani kama ni poa kabisa..
 
Sasa tukikueleza habari za kuosha kucha kitaalam, scrubing kama sio mask, facial levent na pimpos disout , hair sprayin, tutakua tumekutukana sana pole aseeeee mutuwache sie wavaa cheni tuendeleeee na yetu mbona hatujasema msiovaa mnatuudhi?
Duh kuna kitu hakipo sawa hapa..ila ni malezi wakati mwingine..
 
mi navaa cheni na saa labda ungeniambia heleni tu ningekuelewa... cheni na saa vina tatizo gani, na nani alikuja akasema hivi ni vya mwanamke? designer wenyewe wanaandika "for men" sasa sijui wewe hayo yako umetoa wapi
Inashangaza kweli..hivi mnatetea kuvaa cheni na hereni..ndo maana bongo hapo hata mjini kama posta unakuta vijamaa vya ajabu ajabu tu..
 
Wanaume kama mabinti. Micheni, mihereni, poda, kutinda nyusi yote haya nimeyaona yanafanywa na baadhi ya wanaume wa siku hizi... basi mkafanye surgery mjiwekee na matiti ili mvae hadi brazia...mfyuuuuuuuu
Na kunawanaume wanatetea hapa kwenye huu uzi..mm nlikua nafanya kazi sekta ya afya bongo mjini posta hapo..nlikua nikiona akija mshkaji gentleman na mabrazamen..hata uelewa wa mambo ni tofauti, lkn hata aina ya shida zao ni tofauti..lkn mademu wanawafagilia sana ndo nashangaa..yaani unakuta mtu yupo na mtu anavaa vichupa chupa tu mpaka najiuliza inakuaje..ila ndo ukipita kwenye mitandao hata hapa wanawake wanalalamika wanaime hawawezi kazi na nini..ila unakuta wanadate na wavaa cheni na wavaa hereni
 
Ila hata viongozi wa dini zote kubwa yaani waislam na wakristo wanasisitiza wanandoa hata baada ya ndoa zao wazivae ili kuondoa/kupunguza usumbufu na maswali maswali mkuu.
Pete ya ndoa iko poa mkuu..tofauti na ile mipete ya rangi rangi..tusitete vitu vya ajabu..unakuta mwanamme kava mapete mikono yote na hadija kopa anavaa nini mkuu..tuache hizo..
 
Unajua mkuu kwenye huu mjadala tukitaka tupate muafaka ni lazima tuanze kuchimba huu utamaduni wa kuvaa hereni kwa wanaume umeanzia wapi/nchi gani. Tukimaliza hapo ndio tuje kujadili kama utamaduni huu hatukuuona hapo nyuma je kimetokea nini mpaka sasa tunayaona haya kwenye jamii yetu. Lkn kama tutajadili kwa kubishana nani mshindi au nani anapenda na nani hapendi hatutapata majibu sahihi. Kwa nionavyo mjadala huu ni hot kweli kweli, hebu wadau tuendelee kumwaga nondo kwa mwenye kujua historia ya hii kitu japo kidogo atutupie.
 
Unajua mkuu mm naishi magharibi nipo nao shule..hizo mambo za kina lil wayne za kwenye tv ..mtaani hazipo..nmekuja kugundua watu waharibiwa sana na tv..hao watu wanaovaa hereni na milege wapo..lkn hamna
watu wanawachukulia serious..yaani ukitokea gentleman unakuta matured women wanakupapatikia ..unawaacha wao wanadeal na viteneger girls ndo pertain ya mambo ilivyo..
 
Pete ya ndoa iko poa mkuu..tofauti na ile mipete ya rangi rangi..tusitete vitu vya ajabu..unakuta mwanamme kava mapete mikono yote na hadija kopa anavaa nini mkuu..tuache hizo..

hahahahahaha! mkuu, nimecheka sana--kama vile naisikia sauti yako jinsi unavyowafokea hawa wanaume kengeufu wanaopenda kuvaa hereni na cheni, halafu wanatetea huo ujinga using cheap statements....wamelaaniwa hawa sio bure!
 
Na mkuu hili jambo limekuwa sana hasa bongo hapo na nadhani pia like proportional na ile kasumba inayoendelea kwamba watoto hawataki kusoma kila mmoja anataka kuwa mwanamziki au bongo muvi.. Kwa hiyo mtu anajiweka kisani kisanii mapema..lakini na nchi maskini media za kimagharibi zimechukua nafasi kubwa sana.. Na magharibi hizo ishu zinafanywa na celebrities kutengeneza identity na brandy ili mtu apige ela na awe juu..akitoka kwenye media unakuta mtu yupo normal tu bongo tunafanya ndo maisha ya kila siku..mtu anaenda hospital cheni na hereni, bank na micheni, kwenye msiba,..na uswahili unakutana na ile ya kiswazi swazi ya uchafuu..ila na elimu nayo angalia tofauti ya raper niki wa pili na chid benzi
 
hahahahahaha! mkuu, nimecheka sana--kama vile naisikia sauti yako jinsi unavyowafokea hawa wanaume kengeufu wanaopenda kuvaa hereni na cheni, halafu wanatetea huo ujinga using cheap statements....wamelaaniwa hawa sio bure!
Mi inanishangaza mkuu na watu wanatetea kabisa..ila kuna baadhi ya mademu wasijitambua ndo wanawaendekeza hii dizaini ya watu...ila ukichunguza sana hawa watu wanakuaga na videmu vitinegers au wale masistadu wanaoigiza maisha ya muvi za wafilipino..
 
Sasa tujiulize nini chanzo cha kumomonyoka kwa maadili au ni kwanini identity yetu kama watz inapotea. Kwa mfano watangazaji wa redioni n.k je nao wamechangia kumomonyoka kwa maadili kwamba pengine vijana wamewaona hao nao wakaona poa tu. Tujiulize hii kitu imeanzia wapi na kwanini ipo/inaendelea kujiimarisha kwenye hii jamii yetu.
 
Kwa swala la heren nakuunga mkono ila kwa cheni na saa,hapana hapo uko peke yako....moja kati ya cfa kuu ya gentlemen ni kukeep time,sasa utakeep vipi time kama huna saa??
Fikiria tena mkuu
 

anaweza akavaa hereni asiwe shoga,au asivae na akawa shoga.mbona hata mashoga wachafu wapo.kuwa shoga ni kuliwa samvu la kopo sio kuvaa cheni au hereni. Au sio?
 
Huwa najiuliza sipati jibu laki nadhani ni mchanganyiko wa mambo matatu..low literacy, umaskini na poor parenting skills..
 
Kwa swala la heren nakuunga mkono ila kwa cheni na saa,hapana hapo uko peke yako....moja kati ya cfa kuu ya gentlemen ni kukeep time,sasa utakeep vipi time kama huna saa??
Fikiria tena mkuu
Na chain ni ya kazi gani..saa enzi hizi za simu kila kitu inaumuhimu huo kweli..
 
Na mwanamke aonekaneje?

Mimi ninachojua ni kwamba u-sexy ni kwa ajili ya wanawake tu--mwanaume anasifiwa kwa kazi na pesa sio kwa kuonekana SEXY! Kama kuna aliye handsome, hiyo inatosha. Mikufu, vidani na bangili kwa wanaume vya nini?
Kama ben kinyaia mkuu..
 
Inashangaza kweli..hivi mnatetea kuvaa cheni na hereni..ndo maana bongo hapo hata mjini kama posta unakuta vijamaa vya ajabu ajabu tu..
Sijatetea kuvaa hereni, na nimesema navaa cheni na saa peke yake which i don't find in anyway related na mawazo machafu uliyonayo.... Zamani watu walikua hawavai hata shati walikua wanafunika sehemu za siri tu, zikaja shorts, zikaja suruali, tshirts, shirts na wavu wanavaa, sasa mtu kuvaa cheni we kama inakuuma shida zako tu, afu unaita watu wa ajabu ajabu, au kwa sababu hatuwezi kukuona humu JF umejichunguza kwanza ukahakikisha uko perfect kabla ya kusema wenzako wa ajabu?
 
Akili ninayo kukuzidi hilo wala halihusiani na kuvaa cheni wala kitu kuandikwa for men au women... Na ndio maana designers wana akili kutokuweka neno "for men" kwenye skirt na ni kitu hakitotokea sababu wanajua its not for men... Mbona unajaribu kulazimisha negativity... what exactly do u want to prove? kama kitu kinakuboa potezea hujalazimishwa kuvaa cheni... kila mtu ana maana yake anavovaa kitu, sawa na pete, mbona same materials hutengeneza pete hutengeneza cheni, sasa labda unambie hadi pete hutaki labda ntakuelewa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…