Peter Nsangano
New Member
- May 22, 2024
- 1
- 1
Habari wapendwa,
Hebu tutazame kidogo hili swala la kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake,
Je, ni nani muhanga hasa wa jambo hili?
Maana katika hali ya kawaida inaonekana wanawake na watoto ni waathirika wakubwa katika hili jambo. Sijui wewe unalionaje.
Lakini kwa upende wango najaribu kutazama kwa jicho la tatu naona kuna kundi moja limesahaulika na ndio linaathirika zaidi na unyanyasaji. Kundi hilo ni wanaume!
Yes, mwanaume ananyanyasika sana lakini vyombo vingi vya kupinga ukatili na unyanyasaji vimeelekeza macho upande mmoja zaidi na kuacha upande mwingine. Wanaume walio kwenye ndoa zao wanapitia changamoto kubwa lakini hawasemi kwa sababu tayari kipaumbele amepewa mwanamke,
Pia mtoto wa kiume amesahaulika kwenye baadhi ya haki na malezi na kipaumbele amepewa mtoto wa kike.
Kwanini hii kampeni isipewe nguvu sawa kwa makundi yote?
Kama nimeona vibaya basi naomba mnisaidie mawazo yenu!
Napendekeza pia vyombo vinavyohusika na swala hili pamoja na jamii yote kwa ujumla tusifumbie macho haya mambo kama kweli tunataka kutengeneza mustakabali mzuri wa jamii ya kesho kwasababu anaesababisha matatizo ndio huyo huyo anayeathirika na matokeo ya tatizo.
Asanteni na karibuni kwa maoni yenye hoja.
#PeterNsangano
#Author|Content Creator| Visionalist
#TambuaKipajiChakoTimizaNdotoZako