Wanaume waoaji lazima tujifunze vinginevyo tutakufa mapema

Wanaume waoaji lazima tujifunze vinginevyo tutakufa mapema

Wake wenyewe ni hawa pHd za €hupi mixer ujuaji u-feminist humo humo hakuna atakaetoboa,dawa oeni wanawake waliolelewa kifamilia siyo hao waliotoka makwao wakaenda vyuo sasa wapo mitaani.View attachment 3039064
Komwe lenyewe kama la Zingerthropus afu masharti tani 1000 😏🤔

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Maisha haya aise,ni kuchanga kalata flesh.Mwanaume ukimpata aliye sahihi utainjoy,vilevile Mwanamke akimpata aliye sahihi atainjoy.
Kwa nn tageti iwe kuachana na sio kuzeeka pamoja kwa mafanikio ya familia yenu?!.
Matatizo hayana mwenyewe.

Kumbuka pia,Kuna wanaume vichomi na vilevile kuna wanawake vichomi pia.
Hakuna aliyekamilika kwa 100%.

Usimwoe huku ukiwa na mawazo kwamba utaachana nae,sio vizuri.

Mchague ambaye unaendana nae,umjue akijue mtaishi kwa furaha hata kama hamna Mali na pia mkijaaliwa kuwa na Mali pia.

Maisha ya kuviziana sio mazuri.
Usiolewe kwa mihemko,Wala kuoa kwa mihemko.🙏
Pined 📌
 
Ndoa nyingi hazidumu kwa kuwa tunajiandaa kutalakiana kuanzia dakika ya kwanza, hivyo hatujitoi kwa moyo mmoja.

Ni bora tusioe/msiolewe kuliko kuingia mguu mmoja ndani, mwingine nje.

Kutokuoa/kuolewa siyo dhambi.
Sio dhambi lakini sasa utakuwa master of masturbation
 
Mwanaume, ukitaka kuoa jitahidi kama una pagala au una nyumba hujaimalizia, malizia mwenyewe usimshirikishe huyo mkeo unaye muoa au unayetaka kumuoa, mali alizokukuta nazo zibaki za kwako binafsi au wanao kama unao wa nje ya ndoa, kwanini, ukimshirikisha akiwa na hela zake akaziweka kwenye ujenzi jua kwamba akiamua kuvunja ndoa ataomba mgawane mali bila ya kujali ulihangaika sana kulipata lipagala lako.

Ni vema mkatafuta kiwanja cha jasho lenu mkaanza kujenga kwa jasho lenu si vinginevyo. Vya mwanamke ni vyake ila anavyovikuta kwa mwanaume ni vyenu wote hapa ndio huwa kuna tatizo, haijawahi tokea mwanamke aka deicate mali zake kuwa ni za wote punde tu mnapooana, ni kwa wachache sana sana sana, hapa lazima wanaume wajue namna, siku hizi ukimwambia mwanamke tukatafte chetu au tukapange muachane na nyumba yako hawataki.

Kwanza ukimkomalia hivyo anatafuta namna muachane. Nimewaamsha kwa swala hili msilale, ila mliopigwa kwa haya matukio mje mtwambie na mliolazwa makaburini kwa matukio kama haya ndugu waje wasimulie ili wengi waamke.
Haya mambo ni magumu pa de zote
Labda niulize, ni vipi endapo mwanamke mfanyakazi anamiliki nyumba yake na baadae akaoana na jamaa wakaishi hadi mwanamke kastaafu na katika mafao yake akaongeza nyumba nyingine
Huyu njemba anahusika?
 
Mali mnazo kusanya mkiwa pamoja/ mlivuna mkiwa wote ni mali za wote, hata kwenye kugawanya, mmeoana akiwa kazini mpaka ana staafu wote mpo kazini, hizi mali za wote. Tatizo ni ulizo mkuta nazo ndio zinaleta ukakasi.
 
Wadogo zangu ambao hamjaolewa mna kazi kubwa sana kwa wanaume wa sasa... kama mtu anaingia kwny ndoa na mind set ya kuja kuachana kuna ndoa hapo? Upendo haupo na uwajibikaji haupo...huwezi ukaoa kwa upendo wote halafu ufiche vitu pembeni..kama hamko tayari kuoa msioe..waache walioamua kuoa na kuwa vichwa vya familia vifanye hivyo...
 
Wadogo zangu ambao hamjaolewa mna kazi kubwa sana kwa wanaume wa sasa... kama mtu anaingia kwny ndoa na mind set ya kuja kuachana kuna ndoa hapo? Upendo haupo na uwajibikaji haupo...huwezi ukaoa kwa upendo wote halafu ufiche vitu pembeni..kama hamko tayari kuoa msioe..waache walioamua kuoa na kuwa vichwa vya familia vifanye hivyo...
Si kwa wa kike tu bali hata wa kiume, maisha ya karne hii ya 21 ni maigizo tupu ya kuviziana ilimradi tu mwonekano wa nnje ni ndoa takatifu.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Back
Top Bottom