Wanaume wengi ni Misukule ya Wanawake. Wana utumwa wa kifikra.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Hamjamboni!

Kuna Misukule ya aina nyingi.

1. Kuna Misukule ya Imani
Hii ni Misukule ambayo waumini hutafuta pesa kwa Hali na Mali. Kwa jasho na damu na kwenda kupeleka Mali hizo kwa Mitume na Manabii WA mchongo. Wengine hupeleka kwa Waganga.

Ukitaka ujue mtu ni Msukule utampima kwenye Mzani wa Sheria na Kanuni.
Je pesa anazotoa kama Sadaka au Zaka zimeamrishwa na Dini au vitabu vya muongozo kama Biblia au Quran? Utagundua pesa hizo nyingi anazotoa zipo Nje ya Kanuni.

Je anachotoa kina lingana na anachopata?
Ukitoa pesa tunatarajia upate Pesa, au bidhaa Fulani au huduma Fulani.
Watu hawatoi pesa wapewe huduma ya maombi Bali wanataka utajiri, uponyaji, mahusiano Bora, Kazi n.k.
Je unapotoa pesa kwa Manabii, wachungaji au Manabii unapata uponyaji unaonekana? Je unapata Kazi hapohapo au Ndio inasubirishwa?
Kwa nini pesa yako wanaitaka papo hapo na sio wasubiri Mpaka uponyaji au upate utajiri?

Jibu ni kuwa Wewe ni MSUKULE

2. MSUKULE WA MAPENZI.
Wanaume wengi ni Misukule ya Mapenzi na wanawake wengi wamejipatia lundo la Misukule inagowahudumia na kuwapa pesa.

Mwanaume anayefikiri kumhudumia mwanamke na kutoa pesa nyingi kwa kujitesa kuwa huo ndio uanaume ni aina ya Mtu aliyeharibiwa Akili, Usukule umemkolea, na kumharibu vibaya.

Mwanaume huyo hana tofauti na Ile Misukule ya kiimani inayopeleka pesa kwa waganga wa kienyeji au Manabii Fake.

Unakakuta kakijana Ka watu kamechoka, kanavuja jasho, kanahangaika kucha kutwa Kutafuta pesa.
Hakalali
Halali vizuri
Hakavai vizuri.
Kanahangaika Kutafuta pesa ili kamhudumie mwanamke.
Alafu Kenyewe kanakuambia ndio uanaume😂😂. Alafu Misukule Wana wimbo wao wenye kiitikio cha Wanaume wameumbwa mateso.
Sio wanaume wameumbwa mateso.
Mtunzi wa wimbo huo angemalizia Wanaume misukule Wameumbwa Mateso kuhangaikia Wanawake na bado wanalizwa na hawapewi Shukrani wala heshima yoyote.

Ukitaka ujue wewe ni Msukule wa MAPENZI
1. Unamtunza mwanamke kuliko unavyojitunza wewe. Wewe ni MSUKULE tuu huna jina la ziada zaidi ya Hilo.
Mwanaume asiye Msukule hawezi kumtunza mwanamke zaidi ya anavyojitunza yeye.

Ikiwa Mungu anataka Moja ya kumi ya Mali zako iweje mwanamke ale zaidi ya nusu ya kipato chako kama kweli wewe sio MSUKULE?

2. Hujaoa, unampangishia mwanamke sehemu nzuri ya kuishi wakati wazazi wako wanaishi nyumba isiyoeleweka.
Embu niambie wewe kama sio MSUKULE ni kiumbe gani?
Uliwahi kuona wapi mwanaume shababi mwenye akili mtimamu ampangishie mwanamke sehemu nzuri ya kuishi ilhali Mamaake au Babaake anaishi sehemu isiyoeleweka. Uliona wapi? Kama hauna Laana wewe ni nini?
Huo ndio Usukule wenyewe.

3. Badala utafute pesa kwa ajili yako. Unatafuta pesa ili uwaridhishe Wanawake au mwanamke. Wewe ni MSUKULE tuu.

Mwanamke aliumbwa kwaajili yako. Yeye ndiye yupo kwaajili yako, na sio wewe uhangaike kwaajili yake. Shauri yako.

4. Unamnunulia mwanamke kitu cha thamani ambacho wewe mwenyewe haujawahi kukinunua kwaajili yako MWENYEWE. Wewe ni MSUKULE.

Mwanaume asiyejitambua ndio hufanya hayo.
Ni kweli hauna Akili. Ni kweli Kabisa
Lakini hauna Baba au wajomba au Babu zako wakakupe ushauri? Jinsi ya kuwa Mwanaume?

5. Unafanya mambo ili kutaka Kuwafurahisha Wanawake kutaka wasipende.
Nani alikuambia wanawake wanapenda wanaume wasiojiamini? Nani aliyekuambia wanawake wanapenda wanaume misukule.
Sio ajabu unatoa pesa hizo pesa wanaenda Kula wanaume Halisi ambao hawatoi hata shilingi Mia Mbovu.

Wanawake ndio hufanya mambo Kuwafurahisha wanaume wa kweli ambao hao wanaume hawana habari na Wanawake.

6. Unajiamini Kisa Pesa. Wewe ni MSUKULE tuu.
Mwanaume Halisi hahitaji pesa ili ajiamini.
Mwanaume anayejiamini Kisa Pesa Hana tofauti na mwanamke anayejiamini Kisa Kapaka Wanja au Make-up.

Huhitaji kuwa na Pesa ili ujiamini kama mwanaume uwapo mbele ya mwanamke.
Hiyo itakufanya uwe mtumwa wa wanawake.

Mwanamke kama hakutaki usimbembeleze.
Kama anataka kuhudumiwa ndio kigezo chake kikubwa mwambie atafute Msukule wake lakini sio wewe.

Fanya Kazi
Jipende,
Jijenge na jiimarishe.
Usiwafuate na kubembelezana na wanawake. Watakufuata wenyewe.

Usiwekeze kwa Mwanamke. Muache mwanamke awekeze kwako.
Mwanamke anampa thamani mwanaume aliyewekeza kwake. Yaani mwanamke awekeze kwako. Ndio atakupa thamani. Na ni hakika utakuwa na thamani.

Mwanaume unapowekeza kwa mwanamke mwenye thamani ni huyo mwanamke sio wewe. Hawezi kukupa thamani kwani tayari wewe huna hiyo thamani zaidi yake.

Wekeza kwa mwanamke aliyewekeza kwako hiyo ni Kanuni ya wakati wote.

Watu wote walioponzwa na Wanawake wao ndio waliwekeza kwa Wanawake.
Ukisikia kina Samson kina Adamu wote waliwekeza kwa Wanawake.

Lakini muangalie Musa kwa Sipora.
Sipora ndiye aliyewekeza kwa Musa.
Muangalie Rebecca aliwekeza kwa Isaka.
Muangalie Sarah kwa Ibrahim

Muangalie Khadija kwa Muhammad.

Usiwe Mjinga. Shauri yako.
Kama hawataki waache, atakuja mwenye sifa.

Acha nikalale

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
20250218_125124.jpg
 
Well said
 
Back
Top Bottom