Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,558
- 64,966
Kuna siku moja nilienda mkoa x kikazi, na katika timu niliyoikuta huko nilikutana na jamaa yangu mmoja nilisoma naye chuo miaka kadhaa iliyopita. Sikuwa na mahusiano naye ya karibu huko nyuma kutokana na tabia zake za kiunafiki au undumilakuwili, hasa kupenda majisifu yasiyokuwa na tija na yuko tayari wewe uumie yeye anufaike.
Baada ya kufika pale, tukasalimiana kwa sababu ni miaka mingi hatujaonana; baada ya kumaliza kazi kwa siku husika aliniomba niende nikapafahamu anapoishi kwa sababu kwa kule ndipo anapoishi. Basi tukaondoka na usafiri wake mpaka anapoishi, baada ya kufika getini ikabidi ashuke afungue geti yeye mwenyewe, baada ya kuingia ndani tukakuta watoto sebuleni wako bize wanaangalia katuni tu wala hawaonyeshi mapenzi yoyote kwa baba yao. Nyumba imepooza kama hakuna familia vile.
Basi tumekaa zaidi ya dakika 30 shemeji haonekani, zaidi ya sisi kuwa pale sebuleni tukibadilishana mawazo huku huyo jamaa akiwa ni muhudumu wa kunihudumia maji. Baada ya muda nikamwambia nataka niondoke kuna mishe fulani nataka nifanye hapo town, basi akaona aibu akasema hebu tutoke nje uangalie mifugo yangu. Baada ya kuzunguka upande wa pili wa nyumba ,tukawa tunaangalia mabanda na mifugo.
Kilichonisikitisha, nilimwona mkewe akiwa yuko bize anachambua mboga zake hana 'time' na mtu. Hata ile furaha ya kumlaki mumewe au mazungumzo ya furaha kwa mumewe hakuna. Basi jamaa akanitambulisha kwa mkewe, lakini alitikisa kichwa tu akaendelea na shughuli zake.
Jamaa kuona hivyo akaona soo, akaniambia Eqn x naomba utangulie kwenye gari nakuja tuondoke. Dah nilifikiri sana, kwa nini hawa wanaishi kama maadui, au tabia za mwanaume zimeathiri familia?