Wanaume wenzangu njooni tusemezane na tukumbushane

Wanaume wenzangu njooni tusemezane na tukumbushane

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za muda huu ndugu jamaa na marafiki, ni matumaini yangu kuwa sote hatujambo na wenzetu wanaopitia mitihani mbali mbali ya kiafya au kiuchumi Mungu awasimamie maana yeye ndio muweza wa yote.

Sote tunafahamu kwamba sisi wanaume ndiyo vichwa na viongozi wa familia zetu. Ukichwa na uongozi huo unakuja kutokana na kuwajibika kwa familia kwa kuwaandalia kesho iliyo yao njema.

Katika kutimiza na kukamilisha wajibu huu wa kijamii na kimaumbile tunajikuta tunatumia rasilimali muhimu kama muda, nguvu na akili kwa wingi na kwa muda kwa manufaa ya wale tunaowajibika kwao. Hili ni jambo la msingi na muhimu kwenye msingi wa familia bora na ustawi wa jamii zetu.

Lakini utekelezaji wa jambo hili halisimamishi miaka na umri wa kuishi mpaka kufika uzeeni, lakini pamoja na jitihada tunazofanya wanaume kwa faida ya vizazi na familia zetu, lakini ni aghalabu sana kwa wanaume kulipwa kwa jitihada hizi.

Kutokana kutumia rasilimali zako zote kwenye kuwapigania hao unaowajibika kwao kama kichwa cha familia unajikuta mpaka unafika umri wa kustaafu bado hujaandaa mazingira ya wewe kuishi baada ya kustaafu. Matokeo yake unakuwa tegemezi kwa watoto ambao muda mwingine wanajipigania kusimama kimaisha.

Rai yangu ni kwamba wakati tunaandaa maisha au kesho za vijana wetu tusijisahau kuandaa na kesho zetu, maana maisha ya uzeeni ya kutegemea vijana wakuhudumie ni maisha ya lawama, na msongo wa mawazo unaofupisha maisha ya wazee wengi sana. Tusijisahau sana hata uzeeni uwe na kakitu ka kukupatia pesa ndogo ya kukidhi mahitaji yako ya kila siku wewe na mkeo.

Nawasilisha.

NB: Nimemuona rafiki yangu kipenzi akiishi maisha ya dhiki baada kutumia miaka mingi akitimiza wajibu wake kama baba wa familia kwa mke na watoto wake, ambao leo wamekuwa wakimsimanga kila anapohitaji msaada kwao, na mke kwa sababu ya uduni wa maisha muda mwingi anaishi kwa watoto wake ambao wanaonekana wana unafuu wa maisha.
 
Wanaume maisha yetu kama simba dume msituni. thamani yake ni akiwa na nguvu akiishiwa hufukuziwa mbali na huishia kufa kwa njaa.
 
Fainali uzeeni.

Tafuta, fanya kazi kama mtumwa ili uishi kama mfalme.

Weka akiba na wekeza.

Watu wengi wanajidanganya kwa kuweka akiba ya hela badala ya kuwekeza.

Tafuta hela, ili baadaye hela ikutafute. Hapa watu wengi wanakwama kwa kutafuta hela maisha yao yote badala ya kuweka mazingira ya kufuatwa na hela.
 
Back
Top Bottom