Wanaume: You have to grow up

Wanaume: You have to grow up

Sijaja kumsema mtu wangu hapa, nashukuru nina mwanaume anyejitambua, he is a "MAN" hiyo ni kwa wanaume mliokalia kulalama tuuuu hamtaki hata kujiongeza, mtajifanya kutafuta visingizio na maneno ya kila namna ila ujumbe umefika, kataeni umasikini, umasikini ni dhambi.

Ungekuwa naye huyo anaejitambua usingehangaika kuandika lijigazeti hapo juu... ungeacha waseme waliokutwa nayo!!!
you sound like mapenzi kwako sio kitu, unaangalia hela kwanza
 
hongera kwa mada yako ndefu...iliyojengeka katika misingi ya majungu na umbeya wa kikekike.....kibaya zaidi ume-generalize wanaume wote as if "you once happened to date all the men here in jf".....

ingekuwa busara na bora zaidi kama punch lines hizi au mistari konde hii ingemfikia mlengwa wako......throwing a stone in a stadium full of partying people has a chance of one millionth to hit your target.

next time ukitaka kuandika hapa jf fanya haya yafuatayo
1- andika kwenye karatasi points unazotaka kuziwasilisha
2- pumzika kwa muda wa takribani masaa matatu kabla ya kuandika kwenye computer or cellphone yako
3- punguza jazba na hasira dhidi ya unayemwandikia ujumbe huo
4- anza kuandika ujumbe wako
5- soma tena kabla ya kutuma ujumbe wako
6- ukijiridhisha kwa vyote ulivyoandika sasa unaweza kutuma ujumbe wako.
7- uwe mpole na mstaarabu wakati unasoma majibu na ujumbe toka kwa watu wengine waliosoma na kuelewa dhima ya ujumbe wako hata kama ni tofauti na wewe ulivyotaka ueleweke....we are not equal from the day we humans were created.

am just a normal person expressing my understanding of your post.....nothing personal

What maters ujumbe mmeupata, hayo mengine walaa hayana msingi kihivyo.
 
Huhuhuuuuuuu jiwe hilooooo, haya jiteteeni wahusika ila ujumbe mmeupata.
 
Ungekuwa naye huyo anaejitambua usingehangaika kuandika lijigazeti hapo juu... ungeacha waseme waliokutwa nayo!!!
you sound like mapenzi kwako sio kitu, unaangalia hela kwanza

Bwana Junior. Cux hebu acha basi kwani lazima yanatoletwa humu yawe ni yale yaliyowagusa wahusika tu? Hata likimkuta jirani yako kama linafaa kushare si unashare tu? Hili ni tatizo na linakua kwa kasi sana kama ukosefu wa nguvu za kiume ujue! Sema tu watu nanaliignore.
 
Last edited by a moderator:
Sijaja kumsema mtu wangu hapa, nashukuru nina mwanaume anyejitambua, he is a "MAN" hiyo ni kwa wanaume mliokalia kulalama tuuuu hamtaki hata kujiongeza, mtajifanya kutafuta visingizio na maneno ya kila namna ila ujumbe umefika, kataeni umasikini, umasikini ni dhambi.
Wewe utakuwa na babu kwa pesa zake,halafu pembeni una ka mariooo umekipenda halafu kanakupiga mizinga balaa.Hela zote anazokupa babu mariooo anabeba unakuja kulia lia jf.nyambaaaf
 
Ungekuwa naye huyo anaejitambua usingehangaika kuandika lijigazeti hapo juu... ungeacha waseme waliokutwa nayo!!!
you sound like mapenzi kwako sio kitu, unaangalia hela kwanza

Mapenzi na pesa ni pande mbili za sarafu zinazotegemeana, huo ndio ukweli mchungu hata kama huutaki. Yawezekana nishapitia hali hiyo thats why nimeliongelea ila pia ni ukweli usopingika kuwa hili jambo lipo kwa kiasi kikubwa mnoooo, ila am happy mume wangu yuko njema so nawaonea huruma wadogo zangu wanaohangaika na wanaume suruali wasiojitambua hata nini wanataka maishani.
 
Habari wana jf, poleni kwa shughuli za ujenzi wa taifa.
Huku mkiendelea kupokea matokeo ya uchaguzi, naomba niongelee jambo moja la msingi ambalo nimekuwa nkilishuhudia katika jamii zetu na hata humu jf ni very common.

Wanaume mmekuwa kama mmepatwa sijui na pepo gani! Yaani ni kama nanyi mnataka kuolewa, mmekuwa watu wa kulalamika tuuuuuuu, kazi hamtaki na hata wenye kazi akili zimekuwa mgando anategemea mshahara mdogooo hata hajitanui kimawazo kusaka hela zaidi, au kazi yenyewe anafanya kivivuuuu muda mwingi yupo kwenye mitandao ya kijamii kujibizana na kutukanana na watu asiowafahamu na wivu usio na mpango kwa waliomzidi kipato.

Imefikia hatua mwanaume anamuonea wivu binti mdogo aliyeolewa na mwanaume (wa makamo) mwenye pesa, utakuta wamekaa wakimjadili binti na hata kumtukana na kuwachanganya wanawake woote kuwa wanapenda pesa (who doesnt), badala wakae wajiulize ni kwa namna gani huyo mwanaume mwenzao amefanikiwa kiasi hicho nao wajitahidi wamfikie au hata kumpita wamekalia majungu tuuuuuuu!! Utasikia mara free manson,mara pesa za madawa (maneno ya wakosaji).

Ni kweli kwamba maisha magumu and so on, ila isiwe excuse ya kuwafanya muwe marioo bila kujijua, wanaume wengi ni marios ila hawajijui tu, sasa si bora mijitanabaishe tuolewe wote tu na sio kuwa walalamishi that much, ni aibu sana tena sana kwakweli.
Msije kujifanya hapa sijui wanawake tunapenda mteremko ndio maana tukaitwa wanawake nanyi wanaume, sisi ni jukumu lenu, sasa mambo yamebadilika siku hizi nasi tunafanya kazi ili tusaidieane ila sasa isiwe ndio chance ya nyie kubweteka na kuwa marioo, mwanaume lazima uwe "MWANAUME" hii itakupa heshima bila hataaa kutumia nguvu kuidai.

You have to man up na mchukue nafasi zenu kama wanaume, kulalamika hakutokufanya uwe Bakhressa au Mengi, wivu pekee unaotakiwa kuwa nao ni wa kupiga hatua na sio kumuonea wivu k'lyn kwa kuolewa na Mengi (vipi wataka kuwa mke mwenzie?)

Nawasilisha, likikugusa waruhusiwa kutukana si ndicho mkijuacho zaidi.

tatizo lako umezoea kutembea na vijana wa shule za msingi, tafuta saizi yako shenzi.
 
Wewe utakuwa na babu kwa pesa zake,halafu pembeni una ka mariooo umekipenda halafu kanakupiga mizinga balaa.Hela zote anazokupa babu mariooo anabeba unakuja kulia lia jf.nyambaaaf

Teh teh teh! Vipi wivu umekushika?? Ukweli lazima usemwe hata kama mchungu kiasi gani, unaruhusiwa kufikiria hivyo pia sikulaumu as ndipo upeo wako ulipoishia.
 
Mmh hivi hata kina Halima Mdee,Joyce Kiria,Esther Bulaya hua wana hivi vimaneno au ni nyie mnaopenda kitonga tu
 
Bwana Junior. Cux hebu acha basi kwani lazima yanatoletwa humu yawe ni yale yaliyowagusa wahusika tu? Hata likimkuta jirani yako kama linafaa kushare si unashare tu? Hili ni tatizo na linakua kwa kasi sana kama ukosefu wa nguvu za kiume ujue! Sema tu watu nanaliignore.

hahha angelileta vizuri sasa.. kuanza kuzunguka mbuyu mara watu wavivu, mara tunamapepo kumbe tatizo ni hela!!!
hili sio tatizo kama mnavotaka kulikuza, mbona rahisi tu ukiona mwanaume hana kipato unachokitaka wewe si unaondoka tu.. na yeye atatafuta mwanamke mwingine wa level zake atakaeweza kumhudumia

Tatizo mnataka kuishi kwa kucopy.. unakuta mtu yupo level za kawaida kabisa ila kwa vile kamiliki smartphone na marafik flani wa kishua atataka na ye date zake ziwe hyatt regency au double tree
 
Mapenzi na pesa ni pande mbili za sarafu zinazotegemeana, huo ndio ukweli mchungu hata kama huutaki. Yawezekana nishapitia hali hiyo thats why nimeliongelea ila pia ni ukweli usopingika kuwa hili jambo lipo kwa kiasi kikubwa mnoooo, ila am happy mume wangu yuko njema so nawaonea huruma wadogo zangu wanaohangaika na wanaume suruali wasiojitambua hata nini wanataka maishani.

Tatizo sio pesa... issue ni kiasi cha pesa unachokitaka!!! sa zingine hata ulipotoka ulikua huna access ya kiasi hicho cha fedha

muda mwingine ni vizuri mkajifunza kuvumilia... it may help you sometimes!!! Mwanaume ulietoka nae mbali atakuthamini kwa mengi kuliko umkute mtu kishajijenga na channel zote za hela... utafanywa mtumwa
 
hahha angelileta vizuri sasa.. kuanza kuzunguka mbuyu mara watu wavivu, mara tunamapepo kumbe tatizo ni hela!!!
hili sio tatizo kama mnavotaka kulikuza, mbona rahisi tu ukiona mwanaume hana kipato unachokitaka wewe si unaondoka tu.. na yeye atatafuta mwanamke mwingine wa level zake atakaeweza kumhudumia

Tatizo mnataka kuishi kwa kucopy.. unakuta mtu yupo level za kawaida kabisa ila kwa vile kamiliki smartphone na marafik flani wa kishua atataka na ye date zake ziwe hyatt regency au double tree

Unaposema "wa kawaida" unaongelea nini haswa? Huo ukawaida wake ni wa nini? Hapa mnajaribu tu kupindisha mada iwe vile mnavyotaka ila kaongelea kitu cha msingi mnoo basi tu kwavile ni jambo ambalo wengi humu huwa hampendi kuambiwa, huo ujumbe wako hapo chini nanyi mngeuzingatia aisee walaaa msingekuwa mnasumbua humu na nyuzi zenu zileeeeee.
 
Back
Top Bottom