Wanavuta bangi pale Arsenal?

Wanavuta bangi pale Arsenal?

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Hilo ni swali ambalo Mmiliki wa liverpool John w.Henry aliwahi kuuliza hasa msimu wa 2012/2013 pale ambapo Arsenal walitaka kumsajili Suarez kwa Paund mil. 40 wakaambiwa waongeze hela wakaongeza Paund mil. 1 na kuwa 41! Yeye W. Heny aliwaona kama mateja wasiojielewa wanataka nini!!

Nimeikumbuka kauli hii leo baada ya kuona eti Arteta anaenda kuwa Meneja mpya wa Arsenal kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu kwa mshahara ule ule wa Unai Emery wa Paund mil. 5 kwa mwaka!!! Najiuliza hv pale Arsenal wanavuta chaa Arusha tena chenye mbegu kabisa?

Mike Arteta hana historia ya kufundisha hata championship! Kama Emery mwenye CV nzuri ameshindwa je Arteta anaweza nini??

Naambiwa Arsene Wenger wakati anaondoka alipendekeza CARLO ANCELOTI wao wakapiga chini wazo lake! Nasikia walimwita Max Allegri kwenye interview ,Allegri aliwauliza arsenal 'Kwanini mnataka mimi kuwa meneja wenu? Arsenal wakakasirika wakamuona ni mjivuni na mkorofi hivyo hafai kabisa!

Nasikia Walivutiwa na Emery kwasabb jamaa alikuja na video analysis ya kila mchezaji wa arsenal ikionesha uimara na udhaifu wa kila mchezaji na akaonyesha namna atakavo improve wachezaji hao!Arsenal wakamuona anafaa kwasababu hatotumia fedha nyingi kwenye usajili!!!

Leo Arteta anapewa mkataba kisa anaijua arsenal na wachezaji wake!!!sababu hii ni ya ajabu!kwani Ljumberg haijui Arsenal?ina maana Arteta anaijua Arsenal kuliko Ljumberg?wakati fred ljumberg kafundisha Arsenal tim ya vijana na kila siku yupo viunga vya Arsenal tena aliichezea kwa mafanikio kuliko Arteta!Haya ni maajabu kabisa!!

Kumbe W.Henry hakukosea alipouliza "Do they smoke there at Arsenal"? Ngoja tuiione Arsenal ya MIKEL ARTETA!!!
 
Kama hawavuti bangi watamwachaje kocha kama Anceloti kwenda everton?Benitez kwenda China?Brendan rodgers hadi anachukuliwa na Leicester???Mashabiki wa arsenal watalia hadi lini???
Aya anza kuvuta sasa mmea afu ulete mrejesho...meneja gari yake brand umeliona we tafuta passo yako kwanza
 
Mikel Arteta asihukumiwe kabla.. ila apewe muda ajenge timu tuone ujuzi wake.
Hata Lampard sio kocha mkubwa ila Chelsea wamemuamini na anafanya vzr.
 
Kama hawavuti bangi watamwachaje kocha kama Anceloti kwenda everton?Benitez kwenda China?Brendan rodgers hadi anachukuliwa na Leicester???Mashabiki wa arsenal watalia hadi lini???
Anceloti huyu huyu Anaetimuliwa kila timu? Umri Umeshakwenda na Benitez Alietimuliwa Newcastle? Kuna Makocha Uwezo wao Umeshagota wamebaki kuganga njaa tu..
 
Hilo ni swali ambalo Mmiliki wa liverpool John w.Henry aliwahi kuuliza hasa msimu wa 2012/2013 pale ambapo arsenal walitaka kumsajili suarez kwa paund mil.40 wakaambiwa waongeze hela wakaongeza paund mil.1 na kuwa 41!Yeye W. Heny aliwaona kama mateja wasiojielewa wanataka nini!!

Nimeikumbuka kauli hii leo baada ya kuona eti Arteta anaenda kuwa meneja mpya wa arsenal kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu kwa mshahara ule ule wa Unai Emery wa paund mil.5 kwa mwaka!!!Najiuliza hv pale arsenal wanavuta chaa Arusha tena chenye mbegu kabisa?

Mike Arteta hana historia ya kufundisha hata championship!kama Emery mwenye CV nzuri ameshindwa je Arteta anaweza nini??

Naambiwa Arsene wenger wakati anaondoka alipendekeza CARLO ANCELOTI wao wakapiga chini wazo lake!Nasikia walimwita Max Allegri kwenye interview ,Allegri aliwauliza arsenal 'Kwanini mnataka mimi kuwa meneja wenu??Arsenal wakakasirika wakamuona ni mjivuni na mkorofi hivyo hafai kabisa!

Nasikia Walivutiwa na Emery kwasabb jamaa alikuja na video analysis ya kila mchezaji wa arsenal ikionesha uimara na udhaifu wa kila mchezaji na akaonyesha namna atakavo improve wachezaji hao!Arsenal wakamuona anafaa kwasababu hatotumia fedha nyingi kwenye usajili!!!

Leo Arteta anapewa mkataba kisa anaijua arsenal na wachezaji wake!!!sababu hii ni ya ajabu!kwani Ljumberg haijui Arsenal?ina maana Arteta anaijua Arsenal kuliko Ljumberg?wakati fred ljumberg kafundisha Arsenal tim ya vijana na kila siku yupo viunga vya Arsenal tena aliichezea kwa mafanikio kuliko Arteta!Haya ni maajabu kabisa!!

Kumbe W.Henry hakukosea alipouliza "Do they smoke there at Arsenal"? Ngoja tuiione Arsenal ya MIKEL ARTETA!!!
Umetema Pumba tupu
 
Issue ya Cv sio kigezo sana cha kumpata kocha bora! Makocha wenye vipaji wapo km walivyo wachezaji tu. Arteta anajua hali iliyopo arsenal kwa sasa, kwa hiyo anaingia pale akiwa anajua kabisa nini anatakiwa akifanye.
Kwanza asicheke na board kuhusu usajili km vipi ahakikishe wanamsapoti vilivyo ikiwa ni pamoja na kumlazimisha mmiliki aachie hela ili kujenga kikosi cha ushindani.
Pia asilazimishe sana kuipeleka timu uefa kama haiko sawa kimfumo vinginevyo itaenda kupata aibu zilezile kubugizwa magoli mengi.
Labda cha muhimu zaidi ni aachane na wachezaji wote ambao wanaona wao ni wakubwa kuliko klabu ambao ndo chanzo cha kushuka kwa morali kwa wachezaji wenzao. Na hii italeta umoja na maelewano baina ya wachezaji na kujenga morali ya kupigana kwa ajili ya timu yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naambiwa ,......!!!

Mimi nikishaona hilo neno kwenye habari yoyote ile naishia hapo hapo kwa sababu najua hiyo habari hamna kitu humo zaidi ya ujinga ujinga tu.

Et naambiwa!!!!

wabongo shida kweli.
 
Huyu Arteta si niliskia kuwa anasukwa na Guardiola kwa ajili ya kuachiwa Citeh for long term future plans? Mana Pep Fraudiola anajulikana kwa kuchupa jahaza hafla hafla bila kutegemea.
 
Mimi nikishaona hilo neno kwenye habari yoyote ile naishia hapo hapo kwa sababu najua hiyo habari hamna kitu humo zaidi ya ujinga ujinga tu.

Et naambiwa!!!!

wabongo shida kweli.
Mimi nikishaona hilo neno kwenye habari yoyote ile naishia hapo hapo kwa sababu najua hiyo habari hamna kitu humo zaidi ya ujinga ujinga tu.

Et naambiwa!!!!

wabongo shida kweli.
Neno naambiwa sio ishu!ni kutoka vyanzo vya uhakika kama sky sport,Daily mirror na n.k!au ningeandika nimesoma?au nimesikia?vyote nilivoandika ni ukweli usemwao na vyombo vya habari vya kuaminika!!!Hata leo Wenger kaongea kuwa yeye kama mshabiki wa arsenal atamsapoti kocha yeyote atakaekuja lakini ukweli ubaki pale pale kuwa ARTETA HANA UZOEFU KABISA WA KUWA KOCHA!!!
 
Ni sawa ila usipende kulitumia kwenye habari au jambo lolote LA maana, kwa sababu limekaa kiumbea umbea na udaku tu.
Linashusha hadhi ya habari au taarifa husika.
 
kumbukeni ata wenger mwenyewe hakuwa na cv lakini aliifanyia arsenal vingi sana so ata ateta hana uzoefu wa kufundisha ila anaijua vema ligi kuu ya england
 
Guardiola amemuonya arteta , amemwambia ni mzigo mzito
Amebebeshwa to turn things around pale Emirates , timu ina changamoto nyingi Sana na pia kuimarika Kwa baadhi ya timu za epl ni ngumu kwake mambo kumwendea vizur msimu huu
 
Back
Top Bottom