Elections 2010 Wanavyuo hawana lolote

Elections 2010 Wanavyuo hawana lolote

Hili ni tatizo kubwa sana kwa wanafunzi wengi wa elimu ya juu katika vyuo vyetu. Mfano ni pale CBE Dar es salaam campus, 90% ya Filed work reports au reseach reports ni copy&paste tu. wanavyuo hawana ile brain-storming wao ni kucopy na kupaste na kutegemea ujanja ujanja kwenye mitihani tu. Huu ni mfano tu wa hali ilivyo katiak vyuo vyetu vya elimu ya juu hapa nchini.
Hii imefanya hata serikali yenyewe kuwadharau na kuamua wasipige kura, dharau ambayo nchi za wenzetu ambako wasomi wanafunzi wa vyuo vikuu ni chanzo cha mabadiliko kitu kama hiki kisingetokea.

Hii itatoa changamoto kwa wanafunzi na wasomi hawa wafahamu kuwa hii serikali iliyowatumia kupata kura mwaka 2005 hawakuwa na nia thabiti ya kuwasidia bali iliwatumia tu kama nguzo na pindi watakaporudi vyuoni walikumbuke hilo na wajiandae kukosa boom ikiwa CCm itarudishwa madarakani kwani CCM imetumia hela nyingi sana kufinance kampeni zake ambazo ni lazima watazichota serikalini kulipia madeni yao, ila ikiwa CHADEMA wataingia basi huenda ikawa neema kwao kwani CHADEMA watabana matumizi ili wao wasome na yale madeni ya kampeni CCM watatakiwa kulipa wenyewe na si serikali tena!!
 
ndugu PLATO nakupongeza kwa thread yako, huo ni mtazamo wako. Members 8 wa kwanza kujibu thread yako wameanza kwa mishangao, nahisi hawakutarajia kukuta walichokikuta, mimi binafsi nakubaliana na wewe lakini pia naweza nikawatetea wanachuo hao kama ifuatavyo;
1; wanafunzi wengi kwa sasa wanatokea shule za kata au hata kama ni shule kongwe za serikali mf. galanos, tosamaganga, old moshi,
pugu.....etc, hazina walimu ambao wengi wao kwa sasa wanakimbilia private school kwenye malipo makubwa, au hawafundishi kwa
ufanisi coz wana part time kwenye shule za kulipia, mwanafunzi huyu akiwa chuo hawezi kuwa na critical thinking coz msingi wake ni
madesa (handout) wanazonunua wakiwa sec. ili wakariri waweze kufaulu.

2; wakiwa chuoni wanabaguliwa kimadaraja, yaani means test, anaepewa 100% hawezi kuwa sawa na wa 40%, huyu wa 40% akipewa
bumu analigawa kulipa sehemu ya ada ya chuo, (pata picha maisha atakayoishi akiwa chuo km udsm na anaishi mabibo, na
anatoka familia ya akina kajamba nani km mimi, wkt huo ana wadogo zake wapo shule za kata wamekosa ada ya elfu
20 inabidi awalipie, bado hujajumuisha na bei za vitu kuwa juu
) WALAHI HATAKWEPA DESSA.

3; System ya vyuo kuingiliwa na mashushu wanafunzi au wahadhiri (siwezi kuthibitisha hilo) huwafanya wanachuo kuishi kwa hofu na
hivyo kuwashawishi kuandamana hasa kwa chuo cha mkuu wangu MKANDALA km ilivyokuwa kwa mkuu wangu wa ukweli
PROF. LUHANGA is impossible.

my take, ni kwamba huyu mwanafunzi aliyelegea kwa njaa, anayeingia library kudesa hawezi kujenga hoja na hawezi kuandamana coz hapo alipo anafikiria akam'bomu nani amsaidie hela ya kauzu maana kafeteria hapaingiliki na mda huo kachoka kutembea kwa miguu kutoka mlimani hadi mabibo jua kali, NA TUMSAIDIE MWANAFUNZI HUYU KWA KUUNG'OA UTAWALA WA KIBAGUZI ILI ASOME KWA KUJIAMINI TOFAUTI NA SASA, TUSIMLAUMU TU. hilo la kondom kuzagaa inawezekana ni kwa wale wachache wanaotoka familia bora maana huyu maskini sidhani km ananguvu ya KUJIGIJIGI wkt hajala chakula cha maana japo akifanya hivyo si mbaya maana anajaribu kusahau shida zake. KUMBUKA chuo wapo wanachuo wakike pia hawana hela hivyo wanajamii kutoka posta kazini au kinondoni huchangamkia hizo tenda za wasomi wakike wanaoganga njaa ili shule iishe wapate wao mradi, so huenda humalizia shida zao hapo hapo maeneo ya public area ili watoto wa watu wawahi discussion na wenzao.
 
This is totally assumption and gossip; please stop!!!

true this assumption gossip, unajua chuoni wapo wanafunzi wengi sana na wenye tabia chafu unaweza kukuta ni 0.001 na inategemeana unazungumzia chuo gani.

Tatizo la wanachuo wa siku hizi wengi wao si wajanja hata kidogo, hata tabia ya kujisomea wapate maarifa tofauti na yale ya darasani wengi hawana ingawa ikitokea mtu wa kuwahamasisha wanahamasika.

wanafunzi wa siku hizi ni wachache sana wanaoweza kuhusianisha mawazo fulani ya mwanafalsafa au saikologia na tukio at hand, kwa kuwa wengi hawajisomei kutafuta maarifa zaidi.

Mi naonenelea kukomaza akili zao walimu watunge mitihani ya kuwafikilisha zaidi na si ile ya barabara, Yaan (FILL BLANKS).

hata hivyo nadhani inakinzana na wingi wao hivyo walimu wanapunguza zigo la kusahihisha.

Mi naona kitendo cha kufuta ma RAIS wa vyuo na kuondoa REV SQUARES hakkika kinapunguza ujasili wa wanafunzi kujifunza kwa wenzao hivyo kuweza kujifunza jinsi ya kujenga hoja, hata hivyo hii inarahisisha kuwatawala.

kama wewe ni mtawala wa chuo ni nzuri sana, hutapata mgomo hata siku moja labda tu boom lichelewe kidogo wanaweza kujikakamua.

Na kuhusiana na uchaguzi, si mbaya wakija kuchagua viongozi wao kwa kuwa serikali itayochaguliwa inawagusa na wao, hafu kaka uzinzi na siasa ni sawa na mbingu na dunia, wala havina uhusiano.
 
lakini kuona condom inaonyesha kuwa wanajali, japo naamini wapo ambao kamwe hawezi kuinunua condom wkt anaitafuta hiyo hele kwa nguvu zote atoe copy ya dessa, bilashaka wanaojigijigi ni wale wenye pesa zao wanaotoka mitaani kuja kuwanunua dada zetu chuoni kwa mwendo wa kibajaji kwenye public area. {mwendo wa kibajaji=mwendo wa fasta fasta ukojoe niwahi lecture}
 
Plato..Hili la condoms wapongeze,Mengine nafikiri umeongea kweli.Mimi binafsi bahati mbaya au nzuri nimesomea nje baada ya six yangu.Kwa mara ya kwanza nilifika chuo kikuu dar wakiwa wanajadili mambo ya uraia wa nchi mbili,Kwakweli niliyoyasikia pale sina hamu kwakweli.Maneno ya Msemaji mmoja na ambaye alishangiliwa sana na wenzake."Kama wanataka kukaa ulaya au marekani si wakae ukouko na watuachia sisi na nchi yetu,wao wanataka kufaidi uko na uku?" kwakweli jamaa alishangilia sana kwa maneno haya..Nilifikiri wanafunzi watakuja na faida na hasara za kuwa na uraia wa nchi mbili lakini palitawaliwa na kuponda Watanzania walioko nje..Mimi mwenye sina uwezo wa kuwa na uraia wa nchi mbili lakini sioni ubaya wa badhi ya Watanzania kuwa na uraia mbili kama usala wa wote sisi utakuwepo.
 
Hizi ni habari mbaya kwa wanavyuo na wanaharakati.mimi ni mwanachuo,ukweli ni kwamba wakati jambo la kubadili muda linaanza niliwaambia wanachuo bila mafanikio kuandamana kupinga jambo hilo kwani ni njama.hawakunielewa.ukweli ni kwamba munaowaita wasomi wala hawako hivyo japo si wote,wengi ni bora liende.tungeandamana wakati ule ingesaidia.niko tayari kukosolewa,lakini wengi hawana interest na critical analysis,ila madesa tu.so wanaharakati mnapoteza muda na pesa,hata vyuo vikifunguliwa,hawataenda,na wengi wanaoweza kupiga kura hawatapiga.vyuo siku hizi ni madanguro tu,nenda kama hamtakuta kondoms kila mahali hadi public places

asiyesoma utamjua tu!!!
 
Hizi ni habari mbaya kwa wanavyuo na wanaharakati.mimi ni mwanachuo,ukweli ni kwamba wakati jambo la kubadili muda linaanza niliwaambia wanachuo bila mafanikio kuandamana kupinga jambo hilo kwani ni njama.hawakunielewa.ukweli ni kwamba munaowaita wasomi wala hawako hivyo japo si wote,wengi ni bora liende.tungeandamana wakati ule ingesaidia.niko tayari kukosolewa,lakini wengi hawana interest na critical analysis,ila madesa tu.so wanaharakati mnapoteza muda na pesa,hata vyuo vikifunguliwa,hawataenda,na wengi wanaoweza kupiga kura hawatapiga.vyuo siku hizi ni madanguro tu,nenda kama hamtakuta kondoms kila mahali hadi public places

Duh!
 
acha unafiki kama uliwaambia useme ni chuo gani hicho sio una generalize vyuo vyote!
Ziningine ni colleges na taasisi sijui unaongelea "wanachuo" wa wapi hawa na uli waambiaje wana vyuo nchi nzima kama una generalize na kama nani maana binafsi sija kusikia!!!
Nadhani ushahidi wa kwanza ni huyu speaker.anakimbilia kuongelea chuo wakati mimi nimeongelea wanavyuo. Pia anakimbilia kujitoa kwa kusema nimegeneralise wakati kwenye post yangu kuna neno 'japo si wote'. Ni wazi kuhusu danguro nime romanticise makusudi lakini kuna ukweli juu ya maadili yanayopotea.
Mimi nasoma constituent college moja ya udsm,mimi nakiita chuo cha kata.hakuna library,na wanafunzi wa mwaka wa tatu wanafundishwa na tutorial assistants.kwenye seminar ukiuliza swali gumu la uelewa walimu na wanafunzi wanachukia eti unakomoa.hakuna academic discussions kwenye premises zaidi ya kujadili arsenal na chelsea,ukikuta wakati wa news wanaangalia chanel 5.wanavaa t shirts zimeandikwa mimi ni intellectual kujitambulisha.
Nimekuwa kwenye conferences na wanafunzi toka vyuo mbalimbali.ranking yangu ni kuwa namba moja kwa mtazamo wangu ni St.AUGUSTINE, 2 ni SUA, 3 ni MZUMBE, 4 ni UDSM, 5 ni TUMAINI NK.
Mmesikia st.augustine walivyokataa ujinga wa serikali.they are becoming a most reputable institute now with Jordan college at Morogoro offering philosophy and theology,not available at our state university. Udsm is now a relic.labda tuichallenge iwe tena university.
 
Kama wanachuo ndio wanajitokeza hata kumchangia mgombea urais pesa badala ya kumpelekea kero zao,ni wazi hata akili zao ni za kimaslahi zaidi si kizalendo,tusiwalaamu ila tuwasaidie kutambua haki zao za msingi likiwa hili la kupiga kura
 
WAA CHE WAENDELEE NA UJINGA WAO KWANI CHUO NI NI SIKU HIZI KWANI WANAJUA WATAUZA MIILI YAO KAMA KAWAIDA ILI WAPATE PESA ZA KUJIKIMU NI KWELI MKUU ULICHO NENA ILA ELIMU BADO HAIOJAWAINGIA NJAA INAWASUMBUA NA ULIMBUKENI
cONQUEST-ACHA LIENDE IKIFIKA SIKU TUTAPIGANA:mmph:
 
Plato una kichaa cha mapenzi au unarukwa na akili? Yani vyuo unaviita madanguro? Hata kichaa atajiuliza mara mbili kama una akili...jaman,acheni kujadili mambo ya ajabu. Wataalam wetu wote wamepitia uko uko alaf leo yanaitwa madanguro? Unataka kusema mh.rais anateua ma-Principals na ma-V.Presidents kuongoza madanguro? Huwezi ukawa ujalewa! Sina maneno machafu ila ningeyapata ningekutukania sana,jaribu kuwa positive thinker mkuu.
 
mbona kama vile unajihami kwa kusema, nipo tayari kukosolewa??? Kukosolewa hakuhitaji mtu kuwa tayari au la,,,,,, mpwa bwana
 
Back
Top Bottom