Wanavyuo walipe madeni kwa kufundisha sekondari!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Watanzania wenzangu inasikitisha sana kuona viongozi wetu wote serikali na upinzania kushidwakutatua matatizo ya elimu Tanzania. Inajulikana fika kwamba Tanzania kunatatizokubwa la walimu na inajulikana fika vilevile kwamba tunavijana wengi kwenyevyuo wanaochukua mikopo ya serikali na hawatailipa. Kama wote tunajua haya jeni kwanini wanavyuo wasifundishe mashuleni?. Wakali wa likizo wanavyuowanafanyanini wakati kazi hamna si bora wangefundisha shule za sekondariTanzania nzima na kusaidia taifa hata kama hawatalipa mikopo waliyopewa. Mradikama ulivyokuwa wa JK unatakiwa uletwe kwenye elimu kunusuru Tanzania. Shulezote hasa za binafsi zinafelisha wanafunzi kila mwaka lakini serikali badala yakutafuta suluhisho wamekuwa wakiacha kama vile hakuna kitu ambacho wanawezakufanya. Wapinzani nao wamekuwa ni watu wa kuongelea siasa kila siku bila kutoamawazo kama haya ambayo yatatusaidia kwa miaka mingi ijayo.
 
Hivi kila mtu anaweza kufundisha djarasani bila kuwa na mafunzo ya kufundisha kwa kuwa tu ana elimu? Hilo ndiyo linatufikisha hapa tulipo na matokeo yetu.
 
Labda waanzishe vibanda vya tuition ambavyo vimezagaa kama vibanda vya chips mayai.
 
Watanzania wenzangu inasikitisha sana kuona viongozi wetu wote serikali na upinzania kushidwakutatua matatizo ya elimu Tanzania. Inajulikana fika kwamba Tanzania kunatatizokubwa la walimu na inajulikana fika vilevile kwamba tunavijana wengi kwenyevyuo wanaochukua mikopo ya serikali na hawatailipa. Kama wote tunajua haya jeni kwanini wanavyuo wasifundishe mashuleni?. Wakali wa likizo wanavyuowanafanyanini wakati kazi hamna si bora wangefundisha shule za sekondariTanzania nzima na kusaidia taifa hata kama hawatalipa mikopo waliyopewa. Mradikama ulivyokuwa wa JK unatakiwa uletwe kwenye elimu kunusuru Tanzania. Shulezote hasa za binafsi zinafelisha wanafunzi kila mwaka lakini serikali badala yakutafuta suluhisho wamekuwa wakiacha kama vile hakuna kitu ambacho wanawezakufanya. Wapinzani nao wamekuwa ni watu wa kuongelea siasa kila siku bila kutoamawazo kama haya ambayo yatatusaidia kwa miaka mingi ijayo.

Wewe ni mwehu nini? Unadhani kila mtu anaweza kufundisha? au unadhani kufundisha ni kazi rahisi kama siasa za akina Wassira? Eti unazungumzia likizo , hujui wanakua field hao wanachuo? Badala uishauri serikali kubuni nafasi za ajira ili watu waweze kulipa mikopo eti unataka wafundishe. Wangapi wamemaliza ualimu na hawana ajira wako mtaani?
 
Huyu jamaa HAZIMO KWELI! Yaani anadhani UALIMU ni kazi ya kila mtu? Hizi FIKRA MGANDO ndo zinaliangamiza Taifa! Hili janga la wanafunzi kufaulu chni ya asilimia 10, ni matokeo ya kudharau taaluma hii adhimu! tafadhali, TUACHE kufikri kwa masaburi!
 
hii ni idea nzuri sana.naamini huko mitaani vijana wanafundishwa na form six leavers sasa jukumu hili wapewe wanavyuo.mimi binafsi nilifundishwa na mchanganyiko wa walimu...form six leaver,mwanachuo wa education,peacecorps kutoka marekani na japan,wanafunzi wenzangu.kila mmoja alinipa kitu ambacho ninakikumbuka maishani.naungana na mtoa mada kwamba ni vyema na sahihi kwa vijana wetu wa chuo kufundisha mashule yetu ya kata.kuna kipindi mwanachuo yuko likizo anakaa bure mtaani kwa nini wasitumike?
 
hivi unafikiri ualimu ni kitu ambacho kila mtu anaweza kujiamulia na kukifanya eeh? kwa sababu tu ni mhitimu wa chuo?

i see ndo maana elimu ya tanzania inadidimia.....
 
Labda kwa kuwa umefundishwa na watu wasio na taaluma ya ualimu {umechanganyiwa madawa} ndio mana umefikiri na kuandika uliyoyaandika. Even you, you can teach, but not every one can educate! So wewe unataka watu wa kufundisha au kuelimisha?
 
Watanzania wenzangu inasikitisha sana kuona viongozi wetu wote serikali na upinzania kushidwakutatua matatizo ya elimu Tanzania. Inajulikana fika kwamba Tanzania kunatatizokubwa la walimu na inajulikana fika vilevile kwamba tunavijana wengi kwenyevyuo wanaochukua mikopo ya serikali na hawatailipa. Kama wote tunajua haya jeni kwanini wanavyuo wasifundishe mashuleni?. Wakali wa likizo wanavyuowanafanyanini wakati kazi hamna si bora wangefundisha shule za sekondariTanzania nzima na kusaidia taifa hata kama hawatalipa mikopo waliyopewa. Mradikama ulivyokuwa wa JK unatakiwa uletwe kwenye elimu kunusuru Tanzania. Shulezote hasa za binafsi zinafelisha wanafunzi kila mwaka lakini serikali badala yakutafuta suluhisho wamekuwa wakiacha kama vile hakuna kitu ambacho wanawezakufanya. Wapinzani nao wamekuwa ni watu wa kuongelea siasa kila siku bila kutoamawazo kama haya ambayo yatatusaidia kwa miaka mingi ijayo.

wazo lako halipishani sana na la wale waliofikiria kwamba solution ya kudhibiti uchakachuaji wa mafuta ni kupandisha kodi ya mafuta ya taa..! unapaswa uelewe kwamba sheria ya mikopo ni sheria kamili na kwa hiyo unapopata mkopo ni lazima urejeshe mkopo ili wengine waweze kusoma kwa hayo marejesho yako.. hayo uliyoyazungumzia ni mapungufu ya serikali ilio madarakani ambayo haina budi kutengeneza mipango ya kuinua elimu kwa njia nyingine.. 2ciwe na majibu rahic kwa maswali magumu tafadhali..
 
hivi unafikiri ualimu ni kitu ambacho kila mtu anaweza kujiamulia na kukifanya eeh? kwa sababu tu ni mhitimu wa chuo?

i see ndo maana elimu ya tanzania inadidimia.....
Ingawa sijafanya research nina uhakika zaidi ya 70% ya walimu wamesomea ualimu kwa bahati mbaya, wamesomea ili wapate ajira fasta na wengine matokeo ndo yamewapeleka huko.
So walimu kama hao hawana tofauti na Graduates wasio walimu.
Af kuna kipindi graduates wa field nyingine walikuwa wanaajiriwa na serikali kufundisha huu mpango sijui ulifia wapi?. Tuwe wakweli tuition gani zinafundishwa na walimu by Professional na watu wanaelewa, au wale walimu wa vodafasta walikuwa na tofauti gani na wahitimu wa kawaida?

kuliko class?!
 
Lakini utambue kuwa pamoja na kuwa kwa bahati mbaya lakini wamesomea tayari, mbinu za kufundishia wanazo tayari. kufundisha ni kipaji. kwani hujawahi kuona genius ameshindwa kukuelekeza kitu mpaka uelewe,unabaki unalalamika humuelewi naye anakushangaa kwa nini humuelewi?
 
Kwa hy unakubali kufundisha ni kipaji na uwezo wa mtu na sio kusomea!?
 
Kwanini watu wanadharau ualimu? Au kwavile Baba wa Taifa alifanya uamuzi wa busara kuacha ualimu na kujiunga na siasa!
 
Nawapongeza kwa mawazo yenu ndugu zangu lakini hili wazo ni zuri naomba nielezee hali ya sasa.

Tanzania ina makundi haya ya shule za sekondari shule za serikali, shule za mashirika ya dini, shule binafsi hizi ndiyo nazozifahamu mimi.

1. Shule za sekondari: Hakuna walimu wa kotosha na kwasababu hiyo basi ni vigumu kumpata mwalimu kwenye shule za mikoa midogo au kwenye shule za vijijini. Pamoja na kuwa na vyuo vya ualimu bado hakuna walimu wa kotosha Tanzania nzima.
2. Shule za mashirika ya dini: Kuna shule zinazofanya vizuri kama shule za katoliki na shule za Agha Khan lakini kuna shule nyingi sana mchwara ambazo zimeachiwa na serikali wakati zinatoa Div 4 na 0 kuliko 1,2 na 3. Moja ya sababu ni walimu kwani waalimu wazuri hawapendi kuwa na record ya kufelisha.
3. Shule binafsi: Hii ni miradi ya watu binafsi kama shule za Mkono hizi ni expensive hivyo sio za kila mtu. Hizi shule zina uwezo wa kulipa walimu.

Ndugu zangu kila kitu Tanzania ambacho kinakosekana wananchi wanataka serikali ifanye wakati huo huo wanalalamika serikali ni kubwa sana na hatuna pesa. Serikali sasa hivi inasomesha watoto kuanzia la kwanza mpaka vyuo vikuu, wanatoa mikopo halafu hao walimu wa chuo tena walipwe na serikali kila kitu ! serikali haitakuwa na uwezo huo badala yake tutakuwa na utaratibu wa sasa wa kumaliza shule bila kufundishwa na kujihesabu msomi. Halafu kutakuwa na Watanzania wenzetu kama hapa ambao wanalalamikia serikali kila siku lakini hakutakuwa na solution.
Mimi wazo langu ni fupi Kwa shule zote za serikali ni bora wanavyuo wapelekwe kufundisha kama ilivyokuwa JKT program kama umepata mkopo hupewi cheti mpaka ufundishe. Hata kama ufundishaji hautakuwa si mzuri kama wa waalimu lakini utakuwa bora kuliko kutokufundishwa kabisa!. Vile vile shule ambazo ni za binafsi hasa zile zinazofelisha hiyo pesa ambayo wangelipa walimu ambao hawapo watumie kuwapa marupurupu hawa vijana. Kama shule binafsi inaendelea kufelisha ifungwe kabisa badala ya kuiba pesa za wananchi. Je mnamfahamu nani aliyelipa deni la chuo Tanzania?
 
Ingawa sijafanya research nina uhakika zaidi ya 70% ya walimu wamesomea ualimu kwa bahati mbaya, wamesomea ili wapate ajira fasta na wengine matokeo ndo yamewapeleka huko.
So walimu kama hao hawana tofauti na Graduates wasio walimu.
Af kuna kipindi graduates wa field nyingine walikuwa wanaajiriwa na serikali kufundisha huu mpango sijui ulifia wapi?. Tuwe wakweli tuition gani zinafundishwa na walimu by Professional na watu wanaelewa, au wale walimu wa vodafasta walikuwa na tofauti gani na wahitimu wa kawaida?

kuliko class?!

Sidhani kama mtu akisomea kitu halafu asikipende anaweza fananishwa na yule abaye hajakisomea kabisa, hapo sioni hata chembe ya ufanano , yaani ni kama usingizi na kifo.
Kuhusu hawa Voda fasta ni janga la kitaifa, hawa jamaa ndio wamechangia kuporomoka kwa maadili na ufaulu kwa wanafunzi, fuatilia utaona.
Halafu, teaching is a proffesion like any other proffesions, huezi kua competent ndani ya proffession flani kama hujapata mafunzo yake, utateseka tu. Mwalimu wangu aliwahi kuniambia " anyone out of his proffesion is like a dislocated bone, he will suffer or cause sufferings" kama haitakusumbua basi utasumbua wanafunzi wako.
 
Hawa ma-Lecturer wa vyuo wanasomea wapi!?
 
tena hapa UDSM kuna vipanga wa telecom wana PCM point 3 na 4 nyingi sana,wanaweza saidia kuhokoa jahazi.
 
Hawa ma-Lecturer wa vyuo wanasomea wapi!?

They are known as lecturers not teachers. Hapa idea ya mleta uzi ni walimu hasahasa wa sekondari, tusihame hapo.
Halafu angalia kazi ya hao malecturer ufananishe na ya walimu wa msingi + sec ndipo utakapoona utofauti wao.
 
Back
Top Bottom