Wanawake, acheni kuwa Ombaomba kwenye Mahusiano

Wanawake, acheni kuwa Ombaomba kwenye Mahusiano

AXIOM APEX VERBOSE

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
13,769
Reaction score
23,676
Na ninaomba niwe very serious katika hii kitu.

Kwanza kabisa nitaelezea kiufupi sana ila najua ujumbe utafika.

Wewe mwanamke kuingia kweenye mahusiano na mwanaume sio kibari cha kuanza kua Ombaomba.

Nitarudia wewe mwanamke kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mliekutana popote pale mkaanza mahusiano sio kibari cha wewe kujigeuza wale ombaomba wanaokaa kando ya barabara na vibakuri wakisubiri wapita njia wawape chochote kwenye bakuri zao.

Nimeyasema haya kutoka na nilichokishuhudia. Mtu tumeingia kwenye mahusiano hatuna hata wiki 4. Wiki ya kwanza kaanza na mzinga nikachomoa ila nikaona sio kesi nikamwachia Vocha. Tukaenda wiki ya 2 kaganda tena karusha mzinga mwingine wa nyuki nikachomoa tena nikakaza nikasema hii simpi.

Akaanza kununa, oya tumeanza kuwasiliana ndani ya wiki 1 unaanza vizinga?

Ikaendelea akapoa tukawa sawa kumbea ananiset alipoona nimechangamka akasema hapahapa ndio pa kurusha ndoana akaingiza bomu lingine kizinga km kawaida yake tena alianza na lawama za kwanini hivi na vile na hivi nikasema duuuh, akasema siku fulani anataka hicho kiasi, nikasema haina shida.

Nikaona sio kesi huyu nitampa na yeye mtihani mdogo sana akiushinda nampa akiushindwa najua hapa sina mwanamke wa maana simpi.

Nikamuomba kitu fulani kidogo sana na nilijua tu kabisa lazima atakataa eeh ikawa kweli akakataa katakata hataki kabisa na maelezo kibao. Nikasema hapa hamna kitu hapa hakuna mwanamke hii ni ombaomba tegemea upande mmoja inataka yeye tu ndio inufaike yeye tu ndio izoe kutoka kwangu haijui kanuni ya Quid-Pro-Quo na alichoomba hapati mshenzi anataka asaidiwe yeye tu.

Ikafika siku ya ahadi anasema usiku wa ahadi blabla nyingi nikampa jibu km alilonipa hio ndio kanuni ya Quid-Pro-Quo jinsi inavyofanya kazi.

Naomba niwaase sana wanawake na mabinti wengine, kuingia kwenye mahusiano sio kibari cha wewe kua ombaomba. Muache mwanaume mwenyewe akupe atoe mwenyewe sio unalazimisha lazima upewe lazima upewe kwani wewe umekua nani ndani ya wiki 1 unalazimisha upewe pesa for what umefanya kazi gani?

Hii hua inakera sana. Muache hio tabia inawaharibia mahusiano bila kujua.

Lastly, mimi ni bahiri sio kawaida pesa yangu hata nikiipeleka dukani nikaambiwa Sabuni 4000 naweza toa 4000 na bado nikasubiri chenji.

Yangu ni hayo tu.
 
Naomba niwaase sana wanawake na mabinti wengine, kuingia kwenye mahusiano sio kibari cha wewe kua ombaomba. Muache mwanaume mwenyewe akupe atoe mwenyewe sio unalazimisha lazima upewe lazima upewe kwani wewe umekua nani ndani ya wiki 1 unalazimisha upewe pesa for what umefanya kazi gani?
Wale Wazuri Wazuri ndio wanatania yakuomba omba Sana, kwa kuwa ni mzuri anajua usipompa wewe wengine watampa, ni Wakala wa Kodi ya mapato
 
Huyo hakupendi na hafai kuwa mwanamke wa malengo.

Kuna muda unawaza hivi huyu mtu kabla hatujajuana alikuwa anaishije?
Acha kabisa wanawake wa hivi ni wanaboa sana, sasa bora na yeye angeonyesha ushirikiano wanasema ...weka 500 niweke 500 iwe 1000, asiechangia kutia mkono marufuku.. sasa yeye hataki kuweka 500 ila anataka 1000.. unamuomba yeye kwamba emu nipe tag kitu fulani anachomoa mbaya hataki kabisa ila pesa anataka balaa tena katoa mimacho anataka pesa ya mwanaume bure bure kabisa wakati hio pesa kuna watu wanafanya kazi ya kusafisha vyoo na vioo ndio wanaipata yeye anataka bure, for what?
 
Wale Wazuri Wazuri ndio wanatania yakuomba omba Sana, kwa kuwa ni mzuri anajua usipompa wewe wengine watampa, ni Wakala wa Kodi ya mapato
Ndio manzi ni kisu ila hii nigga haimpi hela mpaka anashangaa imekuaje hii jamaa haitoi hela?
Screenshot_20261011_075849.jpg
 
Acha kabisa wanawake wa hivi ni wanaboa sana, sasa bora na yeye angeonyesha ushirikiano wanasema ...weka 500 niweke 500 iwe 1000, asiechangia kutia mkono marufuku.. sasa yeye hataki kuweka 500 ila anataka 1000.. unamuomba yeye kwamba emu nipe tag kitu fulani anachomoa mbaya hataki kabisa ila pesa anataka balaa tena katoa mimacho anataka pesa ya mwanaume bure bure kabisa wakati hio pesa kuna watu wanafanya kazi ya kusafisha vyoo na vioo ndio wanaipata yeye anataka bure, for what?
Kuna watu ni mizigo isiyobebeka na ukijichanganya ndio umejichimbia kaburi
 
Back
Top Bottom