1. Mwako 2002 nilibahatika kwenda UK kwa mwaka mmoja na nusu. Basi jioni moja nilikuwa napunga upepo kwenye bustani ya Hyde Park London, akaja mzungu mmoja akaketi jirani nami. Akanisalimia huku akijipigisha story za hapa na pale kujenga atmosphere nzuri . Alipoona mazingira yanaruhusu alibadili mada taratibu akaanza kuingiza verse za kuniomba kinyeo. Yaani jamaa alikuwa kama mwendawazimu, akanipigia magoti eti, I promise it'll be ok!! Duh, kilistuka kwa mshangao mkubwa, nikapigwa bumbuwazi. Nikuwa wima (sikumbuki hata nilisimama saa ngapi) nilisonya kwangu kisha nikajikuta nimeacha tusi kwa Kiswahili, "kumbe wewe mshenzi sana". Jamaa aliona temper yangu akainuka ghafla akisema I'm sorry huku anasema. Kweli Ulaya mashetani wamejaa tele!
2. Mwaka 2006 nilihamishiwa kikazi kwenye mojawapo wa mikoa yenye baridi kali, nikiwa bado mgeni mkubwa wangu wa kazi aliniita chumbani mwake. Nikajua nakwenda kupokea maagizo ya kazi. Alikuwa maji ya kunde ana umbo la kike, matako makubwa yamelegea akikupa mgongo utadhani mwanamke. Anapiga pafyumu mpaka kero, akiingia sehemu, basi panafurika harufu kali ya marashi, ni mtanashati hatari. Nilipoingia akanijaribisha kiti, kisha akainuka akafunga mlango. Alikuwaamefunga taulo tu, basi akatupa taulo, pumzi ikanioanda vibaya sana, moyo unaunda mpaka nasikia, nikawa tayari kwa lolote, hasira kali sana ndani yangu. Jamaa kwa upole na unyonge akajilaza kitandani kifudifudi kisha akaniambia, huwa nina matatizo ya mgongo, naomba utoe nguo uje unijalie mgongoni uwe unanisugua mgongo. Huwezi amini, hasira zote zitaisha nikabaki nimepigwa bumbuwazi, sikupiga hatua, sijui hata niseme nini. Akasema tena baada ya muda, panda kitandani basi. Duh, ndipo fahamu zikanirudia, nikamwambia naomba nikatoa na jasho kwanza nakuja sasa hivi bosi. Basi akadhani nimemwelewa akasema nisichelewe kwani hali yake mbaya.
Nilipotoka nikamwita rafiki yangu mmoja mwenyeji (class mate wangu A Level) nikamhadithia mkasa, ndipo akanitonya, huyu bosi ni shoga na kuna mkubwa mwingine alishamfanya kama mkewe. Nilichoka mwili na roho.
**Haya ni matukio ya kweli kabisa.