Wanawake huongoza kudhalilishwa mitandaoni kutokana na kupiga picha zenye utata

Wanawake huongoza kudhalilishwa mitandaoni kutokana na kupiga picha zenye utata

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
TCRA yataja sababu Wanawake kuongoza kudhalilishwa mtandaoni

MAMLAKA ya Mawasiliano (TCRA), imesema wanawake wanaongoza kwa kudhalilishwa mitandaoni kutokana na kuwa na tabia za kupiga picha zenye utata na kuzituma mitandaoni pamoja na kutumia simu za wapenzi wao kupiga picha za utupu.

Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria na Masharti ya Leseni, Dk. Philip Filikunjombe, alibainisha hayo jana wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari na wanachama wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC).

Alisema takwimu hizo ni kwa mujibu kesi wanazopokea katika mamlaka hiyo ambazo nyingi zinawahusu wanawake kudhalilishwa mitandaoni.

"Wanaodhalilishwa mitandaoni, dada zetu wanaongoza kwa sababu wanapenda kupiga picha na ni wachangiaji wakubwa wa masuala binafsi mitandaoni.

"Changamoto ya usumbufu wa picha zao kuchapishwa na watu wengine mitandaoni inawakuta kwa sababu ya tabia ya kutuma picha mitandaoni," alisisitiza Dk. Filikunjombe.

Aliendelea kutolea mfano kuwa waathirika wa matukio hayo wanapofika TCRA kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya waliofanya uhalifu huo, hubainika kuwa walihusika kuzichapisha wenyewe.

"Unakuta dada aliweka picha kwenye mtandao kupitia ukurasa wake na labda wakati huo alikuwa na mpenzi wake ambaye wameshaachana na pengine yeye anatakiwa azifute, lakini anakuwa hakumbuki nywila ya kuingia kwenye ukurasa wake," alisema.

Alisema suala hilo pia linachangiwa na ugawaji wa nywila kwa watu wa karibu au wapenzi wao na tabia ya kupiga picha za utupu au kuzipokea na kuzihifadhi kwenye simu.

Aliwataka Watanzania kuepuka kutuma picha za udhalilishaji mitandaoni kwa sababu ni kosa kisheria na ili kuepuka usumbufu kwa sababu teknolojia imekua na picha inavyotumwa ni rahisi watu kuichukua na kuihifadhi.
 
TCRA yataja sababu Wanawake kuongoza kudhalilishwa mtandaoni

MAMLAKA ya Mawasiliano (TCRA), imesema wanawake wanaongoza kwa kudhalilishwa mitandaoni kutokana na kuwa na tabia za kupiga picha zenye utata na kuzituma mitandaoni pamoja na kutumia simu za wapenzi wao kupiga picha za utupu.

Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria na Masharti ya Leseni, Dk. Philip Filikunjombe, alibainisha hayo jana wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari na wanachama wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC).

Alisema takwimu hizo ni kwa mujibu kesi wanazopokea katika mamlaka hiyo ambazo nyingi zinawahusu wanawake kudhalilishwa mitandaoni.

"W
Ingesema wanawake wanaongoza kwa kudhalilishana mtandaoni ingekuwa na ukweli zaidi. Ona pages za matusi na kuchamba instagram zinamilikiwa na wakina nani na uwa mara nyingi wanawadhalilisha wakina nani.
 
Sikio la kufa...

Na hii tathmini ya TCRA ni kama inawachochea kutuma za kupofusha macho.
SUBIRINI, YAJAYO YANAFURAHISHA
 
Thamani ya wanawake imeshushwa sana na wao wenyewe. Wanakubali kushindana kupost picha za kuonyesha maungo yao kwa kudanganywa na likes na kupata followers.

Hizo likes mnazotafuta kwa kukaa uchi ipo siku mtazijutia
 
Mwenyezi Mungu ameweka sababu katika kila jambo. Sababu nyingine ziko dhahiri kwa kila mtu na nyingine zipo kwa wenye kuzitafakari.

Wanawake hawafanyi chochote kipya bali wameamua kuyaishi maandiko...

"Katika zama za mwisho WANAUME WATAKUA NA HAYA KULIKO WANAWAKE"

Isipokua kwa wale wenye kumcha Mungu na kufuata maamrisho yake...
 
Mwanamke hajawahi kuwa mkombozi kwa Mwanamke mwenzie na ndo sababu watu wote wenye akili wana shangaa uwepo wa nafasi za VITI MAALUM....
 
Weka picha ya mfano
Dizain hizo mkuu
IMG-20201018-WA0003.jpg
 
Mbona sielewi mana wazungu wanatuambia mwanamke kuvaa hijabu na baibui ni kumnyimba haki yake ya kuvaa vipedo pusha huku wabongo mnalalamika wanawake wanaongoza kwa kutukanwa mitandaoni kwa kuwa hawajisitiri wanapiga picha wakibinua makalio na kujipost mitandaoni Sasa tumsikilize nani.???? Yote tisa ila uislamu umempa heshima kubwa Sana mwanamke ila kuna watu wapingaji wanajifanya vipofu hawaoni lakin mioyoni mwao wanajua ukweli ni upi.
 
Wanawake wasiojiamini na wenye mapungufu sehemu ndo utumia mwili wao. Wakaa uchi wote wanakasoro
 
Back
Top Bottom