Wanawake jifunzeni kumove on

Haki sawa ndio msingi wa yote leo unakubali mtoto wako wa kike kufanyiwa vitimbwi.
 
utakuwa umeanza kufanya majukumu ya kike. ni kama unashangaa wanang'ang'ania nini..., unavyojisikia wewe ni tofauti na wao. POLE AFU JICHUNGE
Mi ni wakiume ila natetea jinsia Ke wewe kama unapata shida ni wewe mkuu.
 
Hahaha aaah wapi! Wanne wote mpaka nikaamua kuwaacha mwenyewe kwa kuwaonea huruma... nimewaburuza sana[emoji23][emoji23]
Wewe unajisifu sio kwani unaandika hivi ukiwa mkoa gani???
 
Mi ni wakiume ila natetea jinsia Ke wewe kama unapata shida ni wewe mkuu.
Huo ni ushoga, kila siku unang'ang'ana na mapenzi waliyonayo wadada kwa wenzi wao, huo wivu gani kwa dada zako? if not yet soon utaingia full
 
Kwanza kabisa kwa utafiti wangu kwako namba moja, wewe ni muungwana mno. Hongera kwa kuwa muungwana.

Tukirejea kwenye swali lako, hapana mkuu siwatafuni hivyo hata.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
Asante sana kwa kunipa hizo sifa,
Kumbe huwatafuni siyo 😁
 
Mmh
KwNza Kila nikiwaza mambo yanayoendelea kwenye hizo ndoa 🙌
Mikifikiria dada aliyeong'olewa meno na jicho, sina hata hamu jamani


Kiukweli Hali ni tete....
 
Tatizo linaanzia pale tulipoamua kuacha maandiko matakatifu na kuanzisha utaratibu wetu katika mambo haya, biblia/qur'an zinaonekana kuwa outdated!
 
Hao dada zako wakichaga wanaojua kuua waume zao.
 
Wanawake msimsikilize huyu bwana...komaeni kwenye ndoa zenu hata kama ni Kwa shida...mkimove on huyu huyu atakuja na uzi wa single mothers...komaeni ndoa ngumu
 
Hii ni google translator?
 
Kiukweli hata mm siwez kuacha kazinet kisa nimefanya Kosa japo alichofanya sio sahihi alikosea Yani nisomeshwe na kijiji niache kazi kizembe kwaajili ya mtu tumekutana ukubwani hapana nimekataa
 
Udhalilishaji, wazungu wana move on tena fasta on spot....
We nawe. Wazungu ndiyo role models wako? Hawa hawa ambao karibia 75% ya ndoa zao zinaishia kwenye talaka kisa ufeminism? Ndiyo unataka dada zetu wawaige hawa? Ili jamii zetu ziwe kama zao mvurugano tu hakuna heshima huwezi jua yupi ni yupi kisa uhuru uliopindukia kimo?

Mambo haya kwa kawaida hufuata historia, mila na desturi za jamii husika na ni makosa kwenda kukopi na kupesti amali za jamii moja na kuzipeleka jamii nyingine bila kujali historia, mila na desturi za jamii hiyo unayoilazimisha kuipandikizia.

Mkondo wako huu wa mawazo ndiyo uliwafanya Wamarekani wakurupuke kwenda Iraq na Afghanistan eti wanapeleka demokrasia yao hii uchwara bila kujua hasa jamii hizo za Kiarabu zinaishije, historia yao ikoje na mila na desturi zao zina mkondo gani. Ni sawasawa na wewe uondoke na haya mawazo yako kengeufu na kwenda kuwahubiria wanawake wa nchi za Uarabuni. Ukirudi na kichwa chako kikiwa bado kimeungana na shingo yako shukuru Mungu!

Wazazi, familia, wazee pamoja na viongozi wa kiroho, ustawi wa jamii (na mahakama) wanayo nafasi ya muhimu sana katika kutatua migogoro ya kijamii hususan hii ya ndoa; na mingineyo. Sioni tatizo lo lote kwa migogoro ya aina hii kusuluhishwa huko na mara nyingi masuluhisho ya aina hii yamefanikiwa vizuri tu na maisha yakaendelea.

Kama unataka mabadiliko iruhusu jamii ibadilike pole pole; na mabadiliko hayo yatokane na jamii yenyewe na siyo haya ya kukurupuka na kuigaiga hovyo kisa eti wazungu wanafanya hivyo. Kuiga iga hovyo huku mwishowe kutakuletea na mambo mengine ambayo yataishia kusambaratisha kabisa taasisi ya ndoa na familia - taasisi ambazo ndiyo msingi imara wa uhai wa taifa lo lote hapa duniani.

Kesi unayoirejelea hapa ya huyo dada naamini ilikuwa ni chai; na hata kama haikuwa chai hayo ni maamuzi yake binafsi (mf. kuacha kazi) na mengineyo ni njia za kijamii katika kutafuta suluhisho la mzozo aliouleta katika familia yake na kumuumiza mwanaume ambaye mwenyewe anakiri kuwa alikuwa mtu mwema, rafiki wa kweli na baba bora kwa watoto wake.

Tusiige ige mambo hovyo bila kujali historia, tamaduni na mila zetu - hata kama yanatoka kwa wazungu ambao tunawaabudu na kuwaona kuwa wamekamilika!
 
Linapokuja swala la haki sawa, hapo ndo ushetani wenyewe unaanza na kufanya ndoa ziwe upuuzi flani, Fahari wawili hawakai zizi moja mkuu, acha mihemko na utafari kwa utulivu. Ikiwa ni haki sawa basi nawaunga mkono wazee wa kataa ndoa, hakuna haki sawa kwenye ndoa
 
mchepuko wa huyo dada alikua hana pasi ttz hahahahaha
 
Sasa mtu ameolewa amove on kivipi tena ikiwa hapigwi yan anakosa vitu ambavyo yeye mwenyewe alivisababisha .Kama n mkristo aendelee tu kumpambania mume wake japo kazingua kuacha kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…