Wanawake jiongezeni kwenye kuandaa futari ya Mwezi huu Mtukufu

Wanawake jiongezeni kwenye kuandaa futari ya Mwezi huu Mtukufu

Bila kukashifu imani ya mtu wafungaji wengi ni kama vile wanabadili tu ratiba ya kura tu basi.

Kuna jamaa yangu mimi miaka yote anafunga na hakuna siku anaamka saa kumi alfajili kwa ajili ya kula hichi kinachoitwa daku.

Yeye akishafuturu jioni, usiku by saa 4 au saa 5 anakula mpunga wake akiingia kulala shughuri imekwisha mpaka kesho muda wa kufuturu.
Na hapo shida iko wapi?

Daku sio lazima upige msosi wa nguvu hata maji tu yakunywa yanatosha au tende. Binafsi sinaga kawaida ya kula daku. Ila maji nakunywa na nafunga fresh tu.

Focus haipo kwenye misosi, bali ipo kwenye ibada na kuzidisha matendo mema.
 
Huwezi kupata mtu amekamilika kila idara,kuna mikoa mambo ya futari hamna(waislam jina)kikubwa ni kumwelekeza ukipata mda wahi nyumbani msaidie kuandaa futari,ikiwezekana kesho mpangia futari itakuwaje,(unaweza sema leo futari utaandaa hiki na hiki)
 
jaman jaman

mambo mengine ninkutafta dhambi tu

umeoa mtoto wa watu kutoka upande wa pili hajui hili wala lile , leo unataka akupikie ftari uliyozoea kula kwa mamako

acheni uonevu wanaume nyiee
Kujua kupika kwa mwanamke ni lazima haina cha upande huu wala ule
 
Huyo wa mkoani asiyejua kupika labda wa Moshi, Dar, Mbeya Iringa na Kilimanjaro
Shida sio kujua kupika, shida ni kupangilia milo kuendana na wakati unaotakiwa kuliwa.
 
Ukiwa na mke wa hvyo hakikisha unapomuachia ela unaacha umeorodheshea na vitu vya kuandaa kwaajiri ya futari.

Kwenye ndoa pia kuitaji mtu ujitoe kufanya imperfect perfect.
 
Ila wanawake siku hizi mapishi kwao changamoto kuna jamaa alikuwa na mke wake basi alikuwa akitaka kupika tu anaenda kumuita rafiki yake aje amfundishe chakula unachotaka kupika ye ni bize na fb WhatsApp Instagram.
 
Aisee!!? Uyo jamaa alikuwa na moyo
 
Kupangilia sio kazi mkuu kazi kukiandaa kilike
Mtaftie mtaalam amfundishe, kama akigoma kujifunza furuliza mwez mzima hauli chakula chake huku unasifia chakula cha mwanamke mwingne uone atakavyo Jifunza fasta fasta
 
Kwani ukila ugali mlaini na nyama Kuna shida gani?yaani mtu kushinda na njaa masaa machache ishakuwa kitu Cha kuogopesha kiasi Cha kutaka uji na urojo kweli?Ninachokiona hapo hao rafiki zako wamekariri tu Maisha...Maana Kuna siku zisizo za ramadhani mtu anakuwa busy hali siku nzima na jioni anaenda kula ugali tu fresh.
 
Bila kukashifu imani ya mtu wafungaji wengi ni kama vile wanabadili tu ratiba ya kura tu basi.

Kuna jamaa yangu mimi miaka yote anafunga na hakuna siku anaamka saa kumi alfajili kwa ajili ya kula hichi kinachoitwa daku.

Yeye akishafuturu jioni, usiku by saa 4 au saa 5 anakula mpunga wake akiingia kulala shughuri imekwisha mpaka kesho muda wa kufuturu.
Ni kweli ratiba ya ulaji inabadilika kidogo,hebu fikiri mtu anakula daku saa kumi alfajiri halafu saa kumi na mbili jioni analalamika kwa Nini kala ugali?Ina maana Hana uwezo wa kuvumilia masaa kumi 14 tu njaa hebu wanaume wa pwani wafike mahali wawe serious Sasa.
 
Kwani ukila ugali mlaini na nyama Kuna shida gani?yaani mtu kushinda na njaa masaa machache ishakuwa kitu Cha kuogopesha kiasi Cha kutaka uji na urojo kweli?Ninachokiona hapo hao rafiki zako wamekariri tu Maisha...Maana Kuna siku zisizo za ramadhani mtu anakuwa busy hali siku nzima na jioni anaenda kula ugali tu fresh.
Tatizo ni kuwaiga waarabu kila kitu, kwani ukifuturu mchemsho wa samaki, wa kuku au wa ng'ombe shida iko wapi? Au ukanywa mtori tu na chapati?

Tatizo wanataka wakae kwenye jamvi kama waarabu na wale vyakula vya kiarabu, huu ndio utumwa hizi dini umeleta.

Ukishinda na njaa ukila tende inatosha sana kuliandaa tumbo kula chakula chochote na kupandisha sukari mwilini.
 
Ila ngozi nyeusi sijui Nani alituroga!hapo tumevaa na makobasi na bakora😂
 
Back
Top Bottom