Wanawake kama hawa wapo wapi jamani?

Kama umelelewa kwa tamaduni hizo naamini bado zitakua kwenye damu japo zinaweza fifishwa na mazingira uliyopo sasa ila haiondoi uhalisia.
Uhalisia bado upo Sana tu
Tabia ya mtu Ni ngozi

Kwa huku mjini kuepusha kushangawa na watu huwa nabend kidogo
Kwangu Ni mwiko kumsalimia mtu nikiwa mkavu nimenyooka km fimbo

Kuna namna ya kujibehave ktk mazungumzo na mtu hasa mtu mzima
 
Tusidanganyane. Siku hizi "no money no honey" Nani akuite "honey" kama huna pesa? Kama nyie wasichana mnasema kamuangalii pesa mbona mnataka harusi zenu ziwe za gharama ambayo ingetosha kiwanja na nyumba ya room mbili?
Si kweli
 
Ila wanaume sijui hata mnataka nini...
Ukipata mdada anayejielewa, hakuombi hela, anafanyakazi, anakushauri maendeleo, anakusaidia unapokwama basi unamchukulia poa, unamuona zoba wa mwisho, unamuona fala kweli...

Ukipata mdangaji vizinga kila siku unalalamika wee mpaka dunia nzima itajua..

Hivi mnajielewa kweli? Mnajua mnachotaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…