Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
WANAWAKE KATIKA MIKUTANO YA MWANZO YA TANU MNAZI MMOJA
Peleka jicho lako upande wa kushoto utaona wanawake wamevaa mabaibui meusi.
Hawa ndiyo wanawake ambao Daisy anawahadithia katika kumbukumbu ya marehemu baba yake:
''Kitu cha kufurahisha ni kuwa hawa akina mama wa Kiislam wote walivutwa katika siasa na Bibi Chiku bint Kisusa, maarufu akijulikana kama Mama Sakina.
Alikuwa Mama Sakina ndiye aliyewapa hawa wanawake niliowataja hapo juu utambulisho na wakaja kuwa watu maarufu.
Baba yeye ndiye alikuwa kiongozi wa mikakati hii yote kwa sababu bila yeye kuwatia hima kwa kutumia ushawishi wake ingekuwa vigumu kuweza kuwatia hawa wanawake katika kuwahamasisha wanawake wenzao wa na wao watoke majumbani kuja mstari wa mbele katika mikutano wakiimba na kutoa vibwagizo vya kuunga mkono TANU na kudai uhuru.
Hili jambo lilikuwa jipya, jambo ambalo katika utamaduni wetu kwa wakati ule halikutarajiwa na ni kinyume katika utamaduni wetu kwa wanawake wa Kiislam kulifanya katika siku zile.
Nimesikia mazungumzo mengi wakati baba na wenzake walipokuwa wakijadili majina na shughuli ambazo hawa akina mama walikuwa wahusishwe ili kuleta mvuto wa kisiasa katika mikutano yao ya TANU.''
Iweje, iweje, iweje leo tunawasahau mama zetu hawa?
PICHA:
1. Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja (Picha kutoka Maktaba ya Mohamed Shebe).
2. Kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa (Mama Sakina), Bi. Titi Mohamed, Kushoto wa kwanza Bi. Tatu bint Mzee katikati ni Julius Nyerere wanamsindikiza uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO 1955.
3. Mama Sakina (1984).
4. Bi. Mwamtoro bint Chuma (1970).