Wanawake kuota Ndevu na Vipara: Chanzo, tahadhari na tiba yake

Mbona wengine hawajipodoi na wanna ndevu,ni vyakula tu na hormone
 
Haya, paka mkorogo basi uje na majibu.

Mkuu acha kupotosha. Kama unapenda kujisomea tumia hata mtandao kusoma endocrine system uone jinsi gani homoni zinafanya kazi kwenye mwili wa binadamu. Mambo ya mkorogo weka pembeni hayo. Ndevu ni effects za homoni mwilini nothing else.
 
Kwa hiyo serikali ianze kusambaza vinyoleo kama neti za hati punguzo?
 
Mkuu acha kupotosha. Kama unapenda kujisomea tumia hata mtandao kusoma endocrine system uone jinsi gani homoni zinafanya kazi kwenye mwili wa binadamu. Mambo ya mkorogo weka pembeni hayo. Ndevu ni effects za homoni mwilini nothing else.

Sure thing mkuu! Mie na mkorogo mbalimbali hata nywele ni za asili lakini nina ndevu japo si kihivyo so nakubaliana na wewe
 
acheni uswahili, is that a national disaster?

mjipodoe wenyewe huko kwa mapodozi feki kutoka china, mkuze makalio huko weeee halafu mtwambie janga la kitaifa!

What a ffffffffffffffffffffffffffffine day! lol

Duh! Umemalizia vizuri mkuu! What a fffffffffffffffffffffine day!
 


Hapo umetuacha wengi
 
1.Dawa za majira 2. Minyama ya kisasa 3. some vipodozi 4. Dawa za matibabu bazo haziepukiki japokowa zaweza kuwa zimesababishwa na above reason. Kwa kuelewa wangu
 
Wakuu nimekuwa nikitafakari na kujiuliza, hivi kwanini wanawake hawapati vipara kama wanaume, au ni kuwa mimi ndo sijaona ila wapo?
Je ni nini kinasababisha kutokewa na kipara?
Je kuna namana yeyote ya kudhibiti mtu usipate kipara?
Je ukishatokewa na kipara kuna njia za kurudisha nywele?, ni zipi?
Je upara ni ishara ya nini?

Tafadhali, tusaidiane kujibu hayo, nimekwama.
 
Tyta eti ni kweli wanawake wenye viwalaza hawapo ?
 
Last edited by a moderator:
Wakuu nimekuwa nikitafakari na kujiuliza, hivi kwanini wanawake hawapati vipara kama wanaume, au ni kuwa mimi ndo sijaona ila wapo?
Je ni nini kinasababisha kutokewa na kipara?

Tafadhali, tusaidiane kujibu hayo, nimekwama.

Biology kidogo ya pre-BRN niliyosoma ilinifahamisha kuwa kipara ni genetic trait. Hurithishwa kutokana na genes. Sasa kuna baadhi ya traits ambazo ni sex-linked yaani hujitokeza kwa watu wa jinsia moja zaidi ambayo sadly ni wanaume. Hii ni kwa kuwa genes za hiyo trait zinabebwa na X-chromosome na wanaume tuna X moja tu ilhali wanawake wana mbili. Kwahiyo X-chromosome yako kutoka kwa mama yako ikishakuwa na hii gene unakuwa affected na hiyo trait, wakati kwa wanawake wakiirithi kutoka kwa baba au mama zao wanakuwa carriers (wanaibeba hiyo charactersistic ndani ya DNA ila haionekani. Itaonekana pale tu ambapo baba alikuwa affected na mama alikua carrier, ndio maana ni wachache).

Kipara ni mojawapo ya hizo traits. Nyingine ni kama colour-blindness ambayo hutokea kwa wanaume zaidi na haemophilia (damu kutokuacha kutoka mwilini pale kinapotokea kidonda)
 


Ingawa upara si kawaida sana katika wanawake kama ilivyo kwa wanaume, athari za kisaikolojia za kupoteza nywele huwa kubwa zaidi. Kwa kawaida ukanda wa nywele za mbele hudumu ilhali uwingi wa nywele hupungua katika maeneo yote kichwani.

Hapo awali iliaminika kuwa ilisababishwa na testosteroni sawa na katika upara wa kiume, lakini wanawake wengi ambao kupoteza nywele huwa na viwango vya kawaida vya testosteroni .

Hata hivyo, upotezaji nywele kwa mwanamke umekuwa tatizo linaloendelea, ambalo kwa mujibu wa Akademia ya Marekani ya Matibabu ya ngozi, huathiri karibu wanawake 30,000,000nchini Marekani.

Ingawa upotezaji nywele kwa wanawake kwa kawaida hutokea baada ya umri wa miaka 50 au hata baadaye, isipoambatana na matukio kama ujauzito, maradhi sugu, ya mlo, na mfadhaiko kati ya nyinginezo, kwa sasa inatokea miaka ya mapema na huku ripoti zikionyesha kuwa hutokea hata wanawake wachanga kama wa miaka 15 au 16.

Sababu za upotevu wa nywele mingoni mwa wanawake zinaweza kutofautiana na zinazoathiri wanaume. Kuhusiana na alopeshia androjeni, upotevu wa nywele za wanawake hutokea kulingana na athari za homoni za androjeni (testosteroni, androsteinedioni, na dihaidrotestosteroni (DHT)).

Homoni hizi za kiume, kwa kawaida hutokea kwa kiasi kidogo kwa wanawake. Hata hivyo, kulingana na Ted Daly, MD, tabibu wa ngozi kutoka Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Long Island, alopeshia androjeni sio sababu kuu ya kupotea kwa nywele kwa wanawake na wataalamu wa ngozi kwa sasa hupendelea kuita hali hii mkondo wa upotevu wa nywele.

Kwa wanawake badala ya kutumia neno androjeni alopeshia. Anaongeza kuwa mkondo wa kike ni wa mtawanyiko na hudhihirika katika eneo lote la juu ya kichwa na waweza kuathiri wanawake wakati wowote.

Wakati mwingine pia mchakato wa homoni huweza kusababisha upotevu wa nywele kwa mwanamke. Baadhi ya mifano ni: uja uzito, kufikia kutoweza kuzaa, uwepo wa uvimbe wa ovari, dawa za kudhibiti upataji mimba na kiwango juu cha androjeni , dalili za vimbe nyingi za ovari.

Pia matatizo ya tezi , anemia, ugonjwa sugu na baadhi ya dawa husababisha upotevu wa nywele kwa mwanamke

Dawa utaweza kwenda London kwenye clinic Harley Street Hair Clinic aliyotibiwa Rooney.


Credit: Katulanda
 
Hahahaaa hlo mbna ttzo dgo sna mwambie limeisha bdo kumalzika tyu mm dawa hyo naijua
 
Nenda kamuone daktari tu, tatizo hili kwa wanawake linaweza sababishwa na sababu zaidi ya kumi, sasa kujua ipi hasa inasababisha ya kwako ili itibiwe effectively ni mziki, bora ukamuone doctor tu achukue details zako zote, upimwe... Kama ukikosa kabisa solution then tafuta sehemu wanayofanya laser hair removal, kwa dar utapata ila mikoani sidhani, hii najua itakua ghali kidogo, ila inaondoa ndevu hazirudi tena, ni njia hata wanaume hua wanatumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…