Wanawake kuweni makini

Wanawake kuweni makini

Nigga What

Senior Member
Joined
May 1, 2021
Posts
164
Reaction score
448
Kuna rafiki yangu wa karibu ameanza kuhangaikia talaka baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka mitatu. Amejaaliwa maisha mazuri kiasi na mwanamke mzuri sana ambaye amepata nae watoto wawili.

Kisa cha bwana huyo kuhangaikia talaka ni mwanamke kumsaliti na mwanaume mwingine ambaye amethibitishwa kutembea na mke wa jamaa kwa miaka miwili sasa.

Rafiki yangu huyo anasema baada ya kugundua hilo mwanamke aliomba msamaha na kulia sana akaamua kumsamehe kishingo upande ili maisha yaendelee lakini anashikwa na KINYAA kila kimuona mke wake huyo hali iliyompelekea kuanza mchakato wa kuvunja ndoa hiyo, jamaa alimpenda sana mke wake na familia yake lakini uhuni wa mwanamke umeharibu ndoto yao na kuondoa furaha kabisa kwenye familia.

Wiki iliyopita alienda kuwatembelea watoto kwa mama yake na mke wake wakamkalisha kikao wajaribu kusuluhisha jamaa akasema hawezi kuishi na mwanamke kama pambo maana alishakosa hamu na huyo mwanamke, Mke wake huyo amenipigia simu mara kadhaa kuomba niongee na jamaa lakini jamaa hataki kabisa kusikia.

ANGALIZO: Wanawake na wake za watu wote huyo mwanaume aliyekuoa ndiye mwenye nia nzuri na mipango mizuri na wewe hao watu wa pembeni wanataka uchi wako tu wakutumie alafu wasikutake tena na hata hawawezi kukuoa maana wanajua wewe ni msaliti wa ndoa.

Nilikuwa nataka kuoa lakini kama nighairi kwanza
 
wanawake wako makini sanaaa, huyo unayemwongelea aliteleza tu kidogoo

Na anavyokupigia simu si ajabu na wewe upo kwenye list yake ya atakaotembea nao baada ya msala kumalizika

anyway kila shwetani na mbuyu wakeee
 
Kwahiyo atateleza tena kidogo kweli wanawake mko makini sana
 
Ikiwezekana acha mawasiliano na huyo mwanamke mzuri sana msaliti na ni mke wa jamaa yako, maana ambae anaishi nae ni yule jamaa amabae tayari ameshamchoka mkewe, ila maisha sio fair unaweza kukuta jamaa pia ni msaliti ila bado tu hajafumaniwa. Anatafita tu tiketi ya kuhalalisha mahudiano yake mapya. Ushauri wangu, mwambie jamaa asamehe arudiane na mkewe huku mtaani muwinda huwindwa, anaweza dondokea kwa msaliti mwingine ambae ni mshirikina, mchoyo, mchafu, muongo na mengineyo mengi ambayo ni hatari zaidi ya huyo aliyemzalia watoto wawili.
 
Jamaa yupo sahihi kabisa,ukisha kua humuamini mtu ni bora kuachana nae tu kuliko kuishi maisha ya wasiwasi,amtwange talaka tu ili akaolewe na huyo aliyekua anachepuka nae,

Life is very short hakuna haja ya kuishi maisha ya wasiwasi.

jamaa angeona comment yako angekuagizia hennessy BTW you are right
 
Ikiwezekana acha mawasiliano na huyo mwanamke mzuri sana msaliti na ni mke wa jamaa yako, maana ambae anaishi nae ni yule jamaa amabae tayari ameshamchoka mkewe, ila maisha sio fair unaweza kukuta jamaa pia ni msaliti ila bado tu hajafumaniwa. Anatafita tu tiketi ya kuhalalisha mahudiano yake mapya. Ushauri wangu, mwambie jamaa asamehe arudiane na mkewe huku mtaani muwinda huwindwa, anaweza dondokea kwa msaliti mwingine ambae ni mshirikina, mchoyo, mchafu, muongo na mengineyo mengi ambayo ni hatari zaidi ya huyo aliyemzalia watoto wawili.

Mawasiliano tena kiongozi unataka kujiweka, jamaa ni mtu decent na anatuasa sana kuhusu uhuni nahisi swala la usaliti kwake sidhani
 
wanawake wako makini sanaaa, huyo unayemwongelea aliteleza tu kidogoo

Na anavyokupigia simu si ajabu na wewe upo kwenye list yake ya atakaotembea nao baada ya msala kumalizika

anyway kila shwetani na mbuyu wakeee
Huku kuteleza kidogo kwa miaka miwili, bila shaka wanawake mpo makini sana.........kifupi piga chini maana hilo halisameheki, mengine kama kuchelewa kurudi home au kuandaa msosi yanaweza kuvumilika.
 
Jamaa yupo sahihi kabisa,ukisha kua humuamini mtu ni bora kuachana nae tu kuliko kuishi maisha wa wasiwasi,amtwange talaka tu ili akaolewe na huyo aliyekua anachepuka nae,

Life is very short hakuna haja ya kuishi maisha ya wasiwasi.

Huku kuteleza kidogo kwa miaka miwili, bila shaka wanawake mpo makini sana.........kifupi piga chini maana hilo halisameheki, mengine kama kuchelewa kurudi home au kuandaa msosi yanaweza kuvumilika.

Endapo kwa miaka yote miwili huyo mumewee hajawahiii fanya na mwanamke mwingine yeyote hata mara moja, basi na amwache mkewe...
 
Aliyekwambia mwanaume ameumbwa kwa ajili ya mwanamke ni nani? mwanamke ndo kaumbwa kwa ajili ya mwanaume ndo maana ukishakubali kuolewa unamilikiwa na huyo mwanaume na wewe huna mamlaka ya kumumiliki mwanaume ndo maana anaweza kuwa na wake zaidi ya mmoja.........tatizo mkishadanganyana na kujazana ujinga na mambo ya usawa wa kijinsia mnaishia kuangukia pua kama hili linaloenda kumtokea huyu punguani mwenzenu.
 
Jamaa yupo sahihi kabisa,ukisha kua humuamini mtu ni bora kuachana nae tu kuliko kuishi maisha ya wasiwasi,amtwange talaka tu ili akaolewe na huyo aliyekua anachepuka nae,

Life is very short hakuna haja ya kuishi maisha ya wasiwasi.
Huyo mchepuko wake akisikia kuwa talaka tayari, atasepa upesi mno, na si ajabu akabadili namba ya cm
 
Vile wanawake wanafuatilia uzi😁😁😁
QEot_.jpg
 
Kuna rafiki yangu wa karibu ameanza kuhangaikia talaka baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka mitatu. Amejaaliwa maisha mazuri kiasi na mwanamke mzuri sana ambaye amepata nae watoto wawili.

Kisa cha bwana huyo kuhangaikia talaka ni mwanamke kumsaliti na mwanaume mwingine ambaye amethibitishwa kutembea na mke wa jamaa kwa miaka miwili sasa.

Rafiki yangu huyo anasema baada ya kugundua hilo mwanamke aliomba msamaha na kulia sana akaamua kumsamehe kishingo upande ili maisha yaendelee lakini anashikwa na KINYAA kila kimuona mke wake huyo hali iliyompelekea kuanza mchakato wa kuvunja ndoa hiyo, jamaa alimpenda sana mke wake na familia yake lakini uhuni wa mwanamke umeharibu ndoto yao na kuondoa furaha kabisa kwenye familia.

Wiki iliyopita alienda kuwatembelea watoto kwa mama yake na mke wake wakamkalisha kikao wajaribu kusuluhisha jamaa akasema hawezi kuishi na mwanamke kama pambo maana alishakosa hamu na huyo mwanamke, Mke wake huyo amenipigia simu mara kadhaa kuomba niongee na jamaa lakini jamaa hataki kabisa kusikia.

ANGALIZO: Wanawake na wake za watu wote huyo mwanaume aliyekuoa ndiye mwenye nia nzuri na mipango mizuri na wewe hao watu wa pembeni wanataka uchi wako tu wakutumie alafu wasikutake tena na hata hawawezi kukuoa maana wanajua wewe ni msaliti wa ndoa.

Nilikuwa nataka kuoa lakini kama nighairi kwanza
Mwanamke ukiamua kumstri na ukamuoe anakuona kama fala, bora muendelee hivo, kuliko kujitolea kumuoe huyu kiumbe.
 
Aliyekwambia mwanaume ameumbwa kwa ajili ya mwanamke ni nani? mwanamke ndo kaumbwa kwa ajili ya mwanaume ndo maana ukishakubali kuolewa unamilikiwa na huyo mwanaume na wewe huna mamlaka ya kumumiliki mwanaume ndo maana anaweza kuwa na wake zaidi ya mmoja.........tatizo mkishadanganyana na kujazana ujinga na mambo ya usawa wa kijinsia mnaishia kuangukia pua kama hili linaloenda kumtokea huyu punguani mwenzenu.

Mwanaume aweza ongoza ng'ombe hata zaidi ya 10 kwa fimbo mojaaa ...... Ilihali mwanamke mmoja aweza wanywesha maji hao ng'ombe kumi ama zaidi kwa ndoo mojaaa

maneno ya kuambiwa changanya na yako sepaaa
 
Ndo hivyo sasa, mwisho wa siku mkosaji atajulikana.......sasa huyo akaendelee kuwanywesha maji hao ng'ombe huko kitaa kwa ndoo yake moja ya maji, kwa nini analia lia sasa.
 
Ni Mara kumi mwanamke ajaribu kuniua kuliko anisaliti.
Maan hadi unaenda panua mapaja kwa jamaa mwingine siyo bahati mbaya hiyo maana mwili wako wote umehusika kuanzia nywele za utosini na ukucha ule wa kidole cha mwisho. Hapo msamaha ni kusepa tu.
Kama huyo tena miaka miwili? Imagine miezi 24 mke wako anafunuliwa tu kama maganda ya pipi ..pumbavuu!!
 
Back
Top Bottom