bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,097
Jana nilikuwa natoka zangu Dodoma kuja Arusha kwa kutumia usafiri wa basi la (...) Nilikaa siti ya dirishani, pembeni alikuwepo dada moja mrembo kweli. Muda wote alikuwa busy na simu yake masikioni akiwa na ear phone.
Nikawa navuta muda achoke kuchati au simu izime chaji nianze mchakato wa kujiprint kwake.
Kwa bahati mbaya nikapitiwa na kausingizi nikaota ndoto kabisa.
Nilikuja kushtuka yule dada akinitikisa kwa nguvu ili niamke huku akipiga kelele "kaka fungua dirisha bwana kwanini unatuumiza namna hii"
Kusema ukweli hali ya hewa ilikuwa mbaya sana ukizingatia A.C haikuwemo mle ndani. Watu wote waliokaa siti za jirani walikuwa wameziba pua zao kwa mikono huku baadhi wakijaribu kujizuia kutapika.
Nikajua kwa vyovyote vile nikajua kitu kiliniponyoka nilipokuwa nimelala maana tangu asubuhi tumbo lilikuwa limejaa gesi.
Nilifungua dirisha nikiwa nimefedheheka sana. Kila mtu kule ndani alikuwa anaongea lake huku baadhi ya masela wakibaki wanacheka tu.
Wanawake wengi walikuwa wakinisimanga utafikiri wao hawajambi..