Wanawake: Kwa nini huuliza maswali haya.........

Wanawake: Kwa nini huuliza maswali haya.........

fikirini

Senior Member
Joined
May 24, 2011
Posts
114
Reaction score
22
Mara kadhaa imenitokea na pia nimesikia wenzangu pia wakishuhudia........wakati mwanaume anapokuwa katika harakati za kuomba uhusiano kwa mwanamke hukumbuna na maswali kama....hivi umenipendea nini? Unanipenda kweli? nitajuaje kama unanipenda?hivi ni kweli huwa wanapewa majibu ambayo ni sahihi na hao watarajiwa wao? na je ni sahihi kuuliza maswali haya mwanzo wa mahusiono? mimi napata shida sana kujua umuhimu wa maswali haya, nakaribisha mtazamo wenu wanajf
 
Mwanamke wa hivyo ni yule uliemvamia kariakoo hivi.....

Ili usipate maswali ya kijinga usimwambie nimekupenda....

Wewe anzisha urafiki wa kawaida kwanza......

Lunch hivi,,,,mara mbili tatu......

Halafu usiseme nakupenda since kupenda si jambo dogo...

Sema nimevutiwa na wewe.......
 
Nyie nanyi!Kwani kuulizwa hivyo kuna ubaya gani?!Ndo kipimo cha kama unamjua au umekurupuka tu!
 
Mwanamke wa hivyo ni yule uliemvamia kariakoo hivi.....

Ili usipate maswali ya kijinga usimwambie nimekupenda....

Wewe anzisha urafiki wa kawaida kwanza......

Lunch hivi,,,,mara mbili tatu......

Halafu usiseme nakupenda since kupenda si jambo dogo...

Sema nimevutiwa na wewe.......
akikataa kwa mtindo huu wala usihangaike naye tena.
 
Nikimpenda na kumtokea mwanamke hana haja ya kuniuliza bali matendo yangu yatamwonyesha kama nampenda ama la. Kumwuuliza mtu eti ni kweli unanipenda it's ok lakini ni nani ataulizwa hilo swali then aseme No sikupendi? Midomo inawesasema kila kitu utakachopenda kukisikia lakini matendo ya mtu ndio muhimu kwenye kipimo cha kujua kama mtu anakupenda kwa dhati ama la
 
Mi nafikiri ni kasumba tu ambayo wanawake/wasichana wanarithishana. Utakuta wale wazoefu ktk mahusiano wanawashauri wenzao ambao mara nyinig ni wale new comers (yaani wanaochipua ktk mapenzi) kwamba mwanaume/mvulana akikutoke muulize hivi na hivi, so ni kama wamekremishwa vile!
 
Nikimpenda na kumtokea mwanamke hana haja ya kuniuliza bali matendo yangu yatamwonyesha kama nampenda ama la. Kumwuuliza mtu eti ni kweli unanipenda it's ok lakini ni nani ataulizwa hilo swali then aseme No sikupendi? Midomo inawesasema kila kitu utakachopenda kukisikia lakini matendo ya mtu ndio muhimu kwenye kipimo cha kujua kama mtu anakupenda kwa dhati ama la
Hapa pekundu pamenikumbusha msemo fulani wa kisheria kwamba unamuuliza mtu leading question unategemea nini? yaani you ask him a question that suggests an answer straight away!
 
Back
Top Bottom