Wanawake mna moyo sana, mnawezaje?

Wanawake mna moyo sana, mnawezaje?

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Unakutana na mtu, wewe tu ndani ya nusu saa ushamchoka. Ni ana gubu, mbishi + mgumu kuelewa. Lakini anaishi na mke na maisha yanaenda.

Ile harufu ya sigara kwa kweli haivumiliki lakini mwanamke analala naye na kuamka naye. Mwingine muda wote kalewa chakali wa kubeba na tolori + kujikojolea (mlevi mbwa), lakini ana mke na watoto.

Kuna wale anajua mpaka bei ya kitunguu na nyanya, yaani kila senti anataka kujua imetumikaje.🙌 Mwingine hasira hazimuishi kidogo tu kalipuka.
 
Unakutana na mtu ww tu ndani ya nusu saa ushamchoka. Ni ana gubu, mbishi + mgumu kuelewa. Lakini anaishi na mke na maisha yanaenda.

Ile harufu ya sigara kwa kweli haivumiliki lakini mwanamke analala nae na kuamka nae.

Mwingine muda wote kalewa chakali wa kubeba na tolori + kujikojolea. (mlevi mbwa) Lakini ana mke na watoto.
Kuna wale anajua mpaka bei ya kitunguu na nyanya, Yaani kila senti anataka kujua imetumikaje.[emoji119]
Mwingine hasira hazimuishi kidogo tu kapaniki.
WAKOLOSAI 3:18-19.
[18]Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
[19]Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.

Kwa maagizo hayo hapo juu [emoji115][emoji115] toka kwa Mungu utagundua aliyeagizwa kutekeleza kitu flani kwa Me au Ke ndicho ambacho hakuumbwa nacho ndiyomaana anasisitizwa na Mungu awe anakifanya kwa mwenziye.

Kiuhalisia huweziwasha tochi mchana sababu mwanga wake hautakuwa na tija yoyote ile tofauti na usiku tu.
 
Kuna mbaba mmoja mtaani kwetu alikuwa analewa mpaka anajikojolea na akawa analala mitarani,mkewe watu wanaenda kumpa taarifa alikuwa anaenda kumchukua anamkokota mpaka nyumbani na wakati huo wa kumkokota huyo mbaba unakuta anamtukana mkewe na kumuita mbwa wewe

Bahati mbaya yule mama alifariki,baada ya msiba yule baba aliacha kunywa pombe kabisa,alikuwa akisema kwasasa siwez kunywa maana malaika wangu hayupo,alikuwa anasikitika sana mkewe kufariki na kumuacha
 
Back
Top Bottom