Mi nimetulia tu miaka mitano ijayo wanaume tutakuwa adimu sana. Covid 29 inaua wanaume sana. 2025 wanaume watakuwa wanalipiwa nahali na wanawake. Hata na za kutolea tutakuwa tumiwa nasisi.
Mwaka juzi niliambiwa kitu na mdada mmoja yuko kwenye late 30's ni mtu nilikuwa namheshimu sana. Tulikuwa tunafanya naye kazi ofisi mmoja akapata ajira inayo mlipa zaidi akaacha kazi na kwenda kwenye ajira mpya, ni pisi kali, na anajiheshimu sana, mtu wa kanisani kwa sana. Huwa tuna kawaida ya kukutana mara kwa mara na kupeana michapo ya kimaisha. Huwa ananiheshimu sana na pia anafahamia hata na wife wanangu pia wanamjua vizuri tu na humwita shangazi.
Kitu alichoniambia ni hiki amechoka kumsubiria mwanaume wa ndoto zake anachohitaji ni sasa ni kuitwa mama haijalishi hata kupitia mume wa mtu.
Nachofahamu huyu dada akiwa kwenye mid 20 alikuwa na mahusiano na mwanaume mmoja classmate wake wa chuo, walikuwa na malengo ya pamoja sana na walikuwa wamefikia hatua ya kujitambulisha katika pande zote mbili. Yule jamaa yake wakiwa katika uchumba akampa mimba rafiki huyu sister, na inaonekana huyu aliyepewa hiyo mimba alifanya kusudi ili kumnasa jamaa. Kwa sababu matukio yalimfanya huyu sister kujua kuhusu ujauzito wa rafiki yalidhihirisha kuwa ilikuwa ni kitu kilichopangwa na hakikutokea kwa bahati mbaya.
Huyu sister aliponiambia uamuzi wake nilimuuliza je umeshapata huyo mtu aliyetayari kuzaa na wewe? Alinambia kwamba " wewe ndiyo mtu Sahihi" nami nikamwambia you can not be serious, unajua kabisa mimi nimeoa na pia mke wangu anakujua na anakuheshimu sana.
Akanambia kwamba, fikiria tu ni jinsi gani unaweza kunisaidia. Nikamwambia nitakusaidia ila sio kwa kuzaa na wewe.
Nilikuwa na jamaa yangu ni classmate wangu yeye alifiwa na mkewe kama miaka miwili iliyopita. Nilitafuta namna ya kuwakutanisha katika matukio mbalimbali na pia nilimweka wazi jamaa kuwa huyu sister anaweza kukufaa she is a potential wife material. Ni event kama mbili tatu nikaona wameanza dating. Baada ya miezi mitatu wakaanza kuishi pamoja. Jamaa alinishukuru sana kwamba nimemwelekeza kwa mke bora.
Tunavyoengea hivi sana mdada ana mtoto wa mwaka mmoja na mtu mwenye furaha sana. Anatuheshimu sana mimi pamoja na wife. Kabla hajaolewa alikuwa na kawaida ya kuwanunulia sana zawadi watoto wangu, ameendelea na tabia hiyo hata leo. Baadhi ya majirani wanajua kuwa ni sister wangu wa kuzaliwa kumbe hata undugu wa mbali haupo.
Hii story nimeleita kwa sababu mwelekeo wa dunia tunakoenda, idadi ya wanaume inazidi kupungua sana. Ndiyo nasema katika miaka ijayo wanaume tutakuwa tunalipwa na wanawake.