carbamazepine
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 46,562
- 285,591
Nakuelewa! ILA
Wimbi la mzazi upande mmoja linazidi kuongezeka kwa kuwa na wanaume hamtizimi wajibu wenu wa malezi.
Huyu dada maskini wapi anajua Wanaume wanalelewaje, anajikuta tu anapaki lipshine mwanae akiamini ndo mapenzi!
Wewe unayejua Unamume HAUPO!
Hata wanaoshi na watoto wao ni absent fathers, nani atafundisha watoto wenu wa kiume kuwa wanaume?
Watoto hujifunza kwa kuona matendo, wapi nyie mnaojua UANAMUME mnadisplay huo uanamume?
MTOTO ANAJIFUNZA ANACHOKIONA!
inahitaji busara na ufahamu wa tofauti sana wa mama anayeelwa tofauti ya malezi ya mtoto wa kike na wa kiume!
WANAUME MSIPOCHUKUA HATUA ZA DHATI KABISA KUONESHA MWANAUME ANAPASWA KUWAJE!
aiseeeeh msiwalaumu hawa wanawake mnaozaa nao wakiwapakia lipstick watoto wenu!
thats the best way anajiona anapendeza, anaamini na mwanae anatakiwa kupendeza hivyo!
Hebu hata kama umeachana na mamake! BE THERE for your son!
hata mamake ni mwehu, wewe USIACHE KUWA BABA KWA MTOTO WAKO!
hali ni tete!
Rai kwa kina mama
HUMKOMOI MWANAUME ULIYEZAA NAE KWA KULEA MTOTO WAKO WA KIUME KIKE.
malezi ya kiyai yai sio kumpenda mtoto!
Mwanaume ajue tu maisha ni magumu, kutafuta ni kutafuta kwa jasho, chakula hakitupwi wala hakichaguliwi, mwanaume ni kuwajibika, mwanaume ni kulinda, mwanaume ni kuprovide, mwanaume ni kuongoza. Hizi ni vitu unapaswa kumjaza mtoto wako wa kiume mapema kabisa!
Mwanaume kama ni mlinzi atatamani kujifunza ulinzi, kama mwanaume ni kutafuta ili familia ile, atajikuta hana muda wa kujiremba remba afanane na Hanna Montana!
Acha kusihi matamanio yako ya kuwa na mtoto wa kike kwa kumvalisha mtoto wako wa kiume traits za kike!
HATA KAMA UMEACHANA NA BABAKE, aseeee usiache kumkumbusha mwanao wa kiume yeye ni MWANAMUME!
Kuna kaka yako mahali, rafiki yako and stuff! hebu hakikisha huyo mtoto ana Male figure anayoitazama.
idolize hata kuhusu BABU YAKE!
msimulie nyakati baba yako alikuwa brave, msimulie kuhusu mjomba wako alivyokulipia ada!
Hupotezi kitu KUISHI NA MWANAO AKITAMBUA NAFASI YA UBABA hata kama BABA hayupo!
narudia
HUMKOMOI EX WAKO KWA KUMUONDOLEA MWANAO DHANA YA UBABA KICHWANI, tumia hata picha za wanaume mashujaa, tumia masimulizi, tumia hadithi.
Pengine ndo baba hana time, aseee tumia hata mawe, kuwe na jiwe dume na jike.
mradi mwanao ASIJIKUTE MAHALI PA KUONA KUWA WA KIKE NDIO SAHIHI na alikosewa kuwa wa kiume!
[emoji1431]comment bora kabisa