Wanawake mnatuharibia watoto wa kiume


[emoji1431]comment bora kabisa
 
Mbaya zaidi mtoto wa kiume ana miaka zaidi ya nane alafu mama yake anavua Nguo mbele yake uchi wa mnyama bila mama yake hata kuna kama hilo ni kosa kinyume na maadili ya kiafrika.
 
Tabia zenu mbovu ndo zinawakimbiza akina baba katika malezi ya watoto wenu.
Katika malezi ya watoto wenu! ?? Sasa hapo unamaanisha hao watoto ni wa mwanamke pekee?

Halafu kwanini always mwanamke ndio tumuhisi mwenye makosa inapotokea kutengana? kwani hakuna wanaume wanaozingua katika ndoa zao? Tuache double standard jamani wanawake nao ni binaadamu, wanaumia kama sisi.

Mwanamke ana asili ya huruma na upendo kupitiliza, ndio maana hekima ya Mungu iliamua yeye ndiye atabeba ujauzito 9 months,
Kuhusu kulea kwa kudekeza na kubembeleza hiyo ni asili yake kabisa na sio kosa, Tangu enzi na enzi mama zetu walionesha huruma na mapenzi kuzidi baba zetu ktk familia,
Utandawazi na mambo ya kuiga ndio umeharibu mambo kwa baadhi yao, wameanza kuvuka mipaka.

Umuhimu wa baba katika malezi upo mkubwa sana na ndio maana tunatakiwa kuwa mwili mmoja ndio tuzae yaani tuoane,

Haya ya single mother kulea vibaya tunalaumu tu bure maana ni sisi wenyewe tumetoka kwenye misingi,
Mimi ni shuhuda namba moja, nimelelewa na mama pekee mimi na wadogo zangu, Mama yetu alitulea vzr sana sijaona dosari popote hata kwa wadogo zngu, wakati mwingine ni kama tunavuka mipaka tunapowaongelea hawa wanawake maana sio wote wajinga,

Baba alikimbia familia akidai anaenda tafuta maisha na hakumuaga mtu, isipokuwa ndugu zake ndio walimwambia mama hayo, akaenda dar es saalam akaoa huko na kuishi huko, aliondoka nina miaka 9 mpaka sasa nina 32, japo nilishaendaga kumchek nikamuukiza mawili matatu khs kuondoka kwake home, siku moja alinambia maisha magumu ndio sababu na akanisihi nimuombee msamaha kwa kwani anapitia magumu mengi huwenda ni kinyongo cha bimkubwa.

Sio hilo tu, kuna wamama wengi sana wanapambana kulea peke yao na watoto wanakuwa vyema tu, hapa labda ungekuwa specific kuwa unaongelea hawa pisi kali wa mjini nitakuelewa.
 
wewe na alichoeleza mtoa mada ni vitu viwili tofaut
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…