Wanaume wengi wanaoa, halafu mke anabeba mimba anazaa mwanaume anaanza kumuona mwenzake anajinenepea tu, anajiachia nk hamwambii mwenzake hadi inapofika "point of no return" ndio wanagutuka!
Halafu hii tabia ya watu kuitana "baba flani" na "mama flani" ndio inaondoa kabisa ile intimacy iliyokuwepo mwanzoni, mnaanza kuonana kwa macho hayo tu, yaani kwamba huyu ni baba/mama fulani wakati zamani mlikua mkiitana majina halisi au ya kimapenzi (for lack of a better word, I mean endearing names, like Honey, Darling etc)
Watu wengi wanadai kuwa eti kuitana majina ya zamani mbele ya watoto ni kuwafundisha watoto tabia mbaya na kuwa watoto wataanza kuwaita wazazi kwa majina hayo. Si kweli. Na kama ikitokea, huwa inapita