Wanawake msikae kimya kwenye ndoa kwa unyanyasaji kisa watoto

Wanawake msikae kimya kwenye ndoa kwa unyanyasaji kisa watoto

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,156
Reaction score
1,667
Maisha yako ni bora sana kuliko ndoa.

Watoto watakua tu.

Ukiona dalili hatarishi chukua hatua haraka kwani hakuna spea za uhai wako.

REST IN PEACE MAMA WA EKUWEMEE!
 
Hivi huwa ni mapenzi, uoga, ujinga, au kujichoka jamani!! [emoji2297][emoji2297][emoji2297][emoji2297]
 
Wafia ndoa na watakufa sana, si wanataka kuridhisha watu wa nje kuwa yuko ktk ndoa, acha akaheshimike huko mavumbini. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila wazazi, walezi, wasimamizi wa ndoa, wazee wa kanisa na wachungaji waache habari ya kumwambia mtu VUMILIA.. mtu anateseka anarudi kwao mzazi anaaanza habari ooh vumilia mwanangu ndoa ndo zilivyo mara ukirudi itakua aibu kwa familia, we nenda tu muombee muoe na sisi tunakuombea atabadilika

Hao ndo wanasababisha watu kuogopa kutoka katika ndoa zenye mateso
 
Hakuna udhalilishaji mbaya na unaoumiza hisia km vipigo ndani ya ndoa, jamani inauma mnoo😢😢
 
shida tunaoa/olewa kibabe na michango ya malaki huko zaidi ya mara mbili kwa wale wanaoa anzia michango ya siku ya engafement, kichen pat, sendoff harusi yenyewe sasa michango yenyewe ni kuanzia laki mtu huyu unazani atarudi nyumbani kwao au ataomba talaka?

tumekosea kuanzia mwanzo mtu mnafungashia magharama kana kwamba ukienda usirudi.
 
Yaani single maza huko Instagram wanahamasishana walio olewa watoke kwenye ndoa kisa kifo cha hyo dada mbona ndoa zenye amani bado zipo na kwenye ndoa wanawake mara nyingi ndo wanye matatizo ndio maana wanachezea vichapo hawawaheshimu waume zao .
 
Maisha yako ni bora sana kuliko ndoa.

Watoto watakua tu.

Ukiona dalili hatarishi chukua hatua haraka kwani hakuna spea za uhai wako.

REST IN PEACE MAMA WA EKUWEMEE!
Kuna kitu hukielewi sawasawa, wanaume ndio wanaongoza kunyanyaswa ila wanavumilia na wanaona aibu kusema jambo hili.

Kama ni kuwalk away kwenye ndoa zenye shida ndani basi wahanga watakuwa ni wanawake.

Fuatilia kwa makini bar zinavyofurika watu mpaka usiku wengi wanakimbia kurudi majumbani mwao mapema maana wanawake wamekuwa kama machuina na tabia mbaya zaidi ni kuwajaza sumu watoto wamchukie baba yao, kumbe Baba akisema awaeleze watoto matatizo ya mama ni msiba katika familia.

Dunia iko mwisho mwisho hii.
 
Ila wazazi, walezi, wasimamizi wa ndoa, wazee wa kanisa na wachungaji waache habari ya kumwambia mtu VUMILIA.. mtu anateseka anarudi kwao mzazi anaaanza habari ooh vumilia mwanangu ndoa ndo zilivyo mara ukirudi itakua aibu kwa familia, we nenda tu muombee muoe na sisi tunakuombea atabadilika

Hao ndo wanasababisha watu kuogopa kutoka katika ndoa zenye mateso
Akili kichwan kwa muhusika.
 
Back
Top Bottom