Wanawake muwe mnathamini jasho la waume zenu

Wanawake muwe mnathamini jasho la waume zenu

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
6,096
Reaction score
16,390
Kuna baadhi ya wanawake wenye tabia ya kutothamini jasho wala kuhurumia nguvu za waume zao.

Watanzania walio wengi kipato chetu ni cha kuunga unga ili kipato chako kikuwezeshe kutimiza mahitaji ya familia yako na wakati huo uweke akiba kwa ajili ya kesho kunahitaji mahesabu ya hali ya juu sana.

Mfano mwanaume unaamuwa ununue kilo 50 za mchele,mafuta lita 10, tambi box 2, ngano mfuko 1, sukari mfuko wa kg 25 na mahindi labda gunia moja. Huku matumaini yako yakiwa kuwa kwa familia yako ya watoto 2 na mkeo mahitaji hayo yatachukua miezi miwili hivyo pesa utakazo kuwa unapata wakati huo unazielekeza kwenye uwekezaji meingine kwa ajili ya familia.

Lakini cha kushangaza baada ya wiki mbili unaambiwa mahitaji yote yameisha ,kumbe ww baada ya kuleta mahitaji hayo mkeo anajigeuza masihi wa misaada mtaani kwako kwa kuwagawia mashosti na dada zake ,na mbaya zaidi hao mashosti na dada zake nao wana waume zao majumbani.

Hii tabia alikuwa nayo shemeji yangu mke wa kaka yangu na kaka alikuja kuniomba ushauri juu ya hilo lakini mm nikosa cha kumshauri kwakweli, lakini baada ya muda alikuja kumdhibiti mkewe kwa njia moja ya kimafia sijui alifundishwa na nani.

Baada ya kuona mkewe haachi hiyo tabia licha ya kumuonya ,alicho kifanya alienda sokoni akanunua gunia la viazi vitamu.

Ikawa ni mwendo wa viazi asubuhi kama chai ,mchana ugali na mboga za majani ,na usiku wanarudia viazi , walienda mwendo huo mpaka miezi 2 nakwambia mwanamke alinyooka kisawa sawa na mwanamke alipo taka kuleta fyoko alimuambia wazi kabisa kuwa kama huwezi maisha ya viazi na ugali ya kila siku mlango uko wazi inaweza ukaondoka.

Sasa brother akawa ananisimulia njia aliyo tumia kuidhibiti tabia ya shemeji kugawa gawa vitu , sasa nikamuuliza kuwa huoni hiyo njia ulikuwa una watesa watoto akiniambia maneno ambayo yalinifikirisha sana.
Akiniambia mdogo wangu siku hizi wanawake wamekuwa wakiwatumia watoto kama kinga ya kufanya mambo ya kijinga ,na wanaume wengi kwa sasa wanaishi kwa mateso ndani ya ndoa kwa sababu falisafa hiyo ya nikifanya hivi watoto watateseka.

Akaniambia kuwa saa nyingine unatakiwa kuwa mnonko kupitiliza ili uweze kuishi na mwana mke.
 
Sina la kusema, nawaonya wote....wanawake wanaua, watoto kwa vijana, wakubwa kwa wazee, wanaua masikini, wanaua matajiri....tujihadhari woote!

Ni gonjwa baya kuliko yote kwa sasa!
 
Huyo mke mwema sana, Wanawake wengine ukileta viazi unakuta kumepikwa kuku utachagua mwenyewe kuuliza alitoka wapi au ule ukalale. Ukiuliza alitoka wapi unapata na jibu kati ya yai na kuku nini kilianza.
 
Yeye aliambiwa kuwa kama hawezi viazi na ugali mlango uko wazi aondoke.
Ndo maana nakwambia ni mke mwema huyo. Wanawake hawa wanaolalamikiwa wa sasa angekuta viazi huku mama na watoto weshajilia vinono na akileta kelele wanakutana dawatini.
 
Huyo mwanamke inaonekana sio mchoyo .

Usimzuie kugawa vitu Ila mfundishe ugawaji ambao ni mzuri ambao hautaweza kuathiri familia kwa njia ambayo ni negative.

Mfano Excessive - au surplus ndo huwa inagaiwa .

Nia na lengo la kutoa linaweza kuwa zuri Ila utekelezaji ukawa mbaya.

Mimi nimewahi kukaa sehemu nikawa napewa Mboga ,mayai ,nyama na mwanamke mke wa jirani

Ila ukija Kwa mme wake sio kwamba alikuwa anjiweza Sana alikuwa mpambanaji wa hapa na pale .

Nilichofanya nilimwambia mke Wa yule jamaa ajjtahidi kupika chakula ambacho kitamtosha yeye peke yake na familia yake asiweke surplus endapo ikatokea nina shida ya mboga ntamuomba.


So wanawake watoaji na watu watoaji wapo mkuu na mtoaji huwa hatazami Kama umepata Kwa njia ngumu au nyepesi.


So usimzuie kutoa kbisa Ila mfundishe njia bora za utoaji.

Kuwa ukitaka kugawa chakula basi wewe uwe umefikiwa kwanza maana agawe ile ziada Kama ipo.
 
Back
Top Bottom