FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,789
- 5,401
Erotica nani kakwambia kuweka simu kwenye manyonyo zina madhara hizo mdada.ukiona mwanamke ana treat simu ya mkononi kama mezani, ina mana hakuna mtu
spesheli katika maisha yake kwa kipindi hicho. kama yupo hana mshiko. ila kama kweli yupo aisee simu inakuwa bega kwa bega,
wakati wa shughuli kama kufua or kupika unaibana kwenye sidiria or unahakikisha
nguo ina mfuko. teh teh teh. but kama hayupo usiku unalala simu iko sebuleni.
Bazazi Dah, umenikumbusha mengi mno maana nimepigizana nae kelele hadi nimeamua kukaa kimya, yaani unaweza kuwa na issue urgent halafu simu haipokelewi, ole wangu sasa nimpigie kwa kutumia Simu ya Housegirl wewewwwwweeeee utajuta, jamani akina mama punguzeni kutunyanyasa
tobaaaaaaa unampigia kwa kutumia simu ya nani? Shauriyako...ninavyowajua wakinamam halahala usije mpotezea housegirl kazi yake....
Hahahaaaaa umenikumbusha ugomvi wa juzi, eti kisa tulikua tumekaa tunapata msosi jioni nikamtania housegirl uuuuuhhhhh yaani hata hamu yote ya chakula iliishia hapo, maana yaliibuliwa na mengine hata yametoka wapi sijui, kwa ufupi akina mama mnatunyanyasa sana na hawa ma-HG ambao wasipokuwepo ndio mnapiga kelele, wakipataikana kelele nyingine inaanza, aaaaaaghhrr
akhaaaa muache mamsap a-mark territory yake, mzaha mzaha hutumbua usaha......
Acha utani na hg, utampotezea kazi
yani wanawake tayari mshajitafutia na visababu hata ukiwa jikoni kwani simu haiwezi kukaa sehemu jikoni mkaisikia?
Wanawake mna matatizo gani na simu za mkononi? Kwanini mnazigeuza kuwa simu za mezani.
Hii haina cha mwanamke msomi na mbumbumbu, mfanyakazi na mkulima/mfanyabiashara, mbinti na mmama, mkurugenzi na mhudumu, waziri na mfagizi: Mradi ni mwanamke kwao simu ya mkononi ni ya mezani.
Ole wetu tuchelewe kupokea simu zao! Tunakutana na maswali mengi sana. Oh mara ulikuwa wapi hupokei simu, Oh ulikuwa na nani? Ni kasheshe iwe nyumbani-chumbani au katika nyumba za wageni au ufukweni. Ni full Kasheshe!
Lakini kwao simu ya mkononi ni ya mezani. Na hujitetea sana ukiwabana kwanini hawakupokea mapema.
Nauliza tena ni KWANINI KWAO SIMU YA MKONONI NI YA MEZANI?
Bazazi ni Bazazi!