Wanawake ni viumbe wanaoeleweka sana sema Sisi ndio hatutaki kuwaelewa

Wanawake ni viumbe wanaoeleweka sana sema Sisi ndio hatutaki kuwaelewa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
WANAWAKE NI VIUMBE WANAOELEWEKA SANA SEMA SISI NDIO HATUTAKI KUWAELEWA!

Anaandika Robert Heriel
Kuhani.

"Mwanamke hajui nini anataka"
"Wanawake hawaeleweki"
"Huwezi kuwaelewa Wanawake" na kauli zingine kama hizo ni kauli za kizamani zilizolenga kuwahukumu Wanawake na kuwafanya wakosaji, wasiaminike, kuwafanya wasijiamini, na kuwa na mtazamo hasi juu Yao wenyewe.
Hakuna kiumbe kisichoeleweka. Kila kiumbe kina hulka na silika yake.

Kuwaelewa Wanawake itakupasa uwachukulie kama Wanawake. Kosa kubwa wanalolifanya Watu wengi ni kumuelewa Mwanamke katika msingi WA mwanaume hapo lazima mpishane.
Ipo namna ya kumuelewa Mwanamke katika msingi WA ubinadamu na ukiumbe kama walivyoviumbe wengine. Hiyo ni kumuelewa kijumuishi na hapo unatengeneza mazingira ya kutomuelewa.
Lakini Ipo namna ya kumuelewa Mwanamke katika msingi WA upekee wake kama Mwanamke bila kuhusisha Sifa za ubinadamu zinazoingiliana na wanaume au viumbe wengine.

Pia Wanawake wakati mwingine wanalalamika wanaume hatueleweki, lakini watafikia hitimisho hilo ikiwa watamfikiri na kumchukulia mwanaume katika mtazamo wa kike.

Kwa nini Wanawake wanaonekana hawaeleweki?

1. Hawapo Huru, wengi wapo Chini ya sheria kandamizi.
Sheria nyingi tangu zamani ziliwekwa na Sisi wanaume kama Watawala. Kwa bahati Mbaya baadhi ya sheria zilikuwa kandamizi na zenye kuminya Uhuru wa wanawake. Hii ilifanya Wanawake wafiche tabia zao za Asili(Silika) na Tabia zao za makuzi(Hulka).
Mtu yeyote ambaye hayupo huru sio rahisi kumuelewa Kwa sababu atakuwa mnafiki na mficha mambo yake.
Uhuru ndio sehemu pekee itakayodhihirisha tabia halisi ya kiumbe.

Mfano wa Sheria kandamizi;
i) mwanaume ndiye mwenye ruhusa ya kuoa Wake wengi. Wanawake walidanganywa na visheria vya Mila na desturi au visheria kandamizi vya Dini huku wakiaminishwa ndivyo miungu watakavyo ilhali wao wenyewe hawataki kitu kama hicho kimoyomoyo. Hii iliwafanya Wanawake kuwa Wanafiki na kukubali kishingo upande,

ii) sheria ya Uhuru wa kushiriki burudani na Michezo ya kijamii.
Wanaume ndio tumepewa nafasi ya kufurahi na kushiriki mambo ya burudani kama Michezo ya mipira, kwenda Club, disko n.k.
Wakati Kwa Wanawake kwenda Club inachukuliwa kama Tabia Mbaya na dalili ya umalaya. Jambo ambalo ni Uongo.
Kuchukulia Mwanamke kama Mnyama wa kufuga nyumbani yaani anatakiwa kuwa nyumbani tuu huku akiletewa mahitaji yake yote kama chakula ni sehemu inayofanya Wanawake wasieleweke endapo wakienda kinyume na Kanuni hiyo.
Unakuta mwanaume anasema, kazi yako kuzurura tuu, nimekuwekea kila kitu ndani lakini unazurura tuu. Wewe Mwanamke unataka nikufanyie nini? Mbona hutosheki?😂😂
Mwanamke hatosheki kama tulivyosisi wanaume. Kukaa sehemu moja muda wote kunachosha.
Mwanamke anahitaji Uhuru ili unafahamu vizuri. Huwezi mdhibiti Mwanamke Kwa kumnyima Uhuru. Ni rahisi kumdhibiti Mwanamke akiwa yupo Huru.

Mwanamke anahitaji umpe Uhuru lakini uwe unamsaidia kumuongoza katika Uhuru wake. Huo atauita UPENDO.
Kuudhibiti Uhuru wake kupitiliza kutamfanya aone unamfanyia Ukatili. Pia ataona haujiamini.
Lakini pia kumuachia Uhuru uliopitiliza itamfanya aone haumjali na humpendi.

Haya ni mambo ya kuyajua unapodili na Wanawake:

1. Wanawake hukifanya kitu kidogo kuwa kikubwa.
Kiwe kitu Kizuri au kibaya. Elewa kuwa Mwanamke hufanya kitu kidogo kuwa kikubwa. Ni Watu wakukuza mambo.

2. Wanawake MLANGO wao Mkuu wa ufahamu ni masikio.
Kadiri unavyomtakia kitu hicho mara Kwa mara kinakua katika moyo wake.
Chochote utakachomuambia Mwanamke hata kama ni utani atakichukulia Serious. Wanawake hawanaga kitu inaitwa utani hasa utani wa maneno. Hiyo kitu hawanaga.
Ukimtania yeye ni Mbaya na Hana Mvuto hata kama ni Uongo ataichukulia serious kauli hiyo. Sio ajabu akakasirika au akaanza kukuchukia.
Wanawake wanaamini Kwa kusikia zaidi kuliko kuona. Wakati wanaume tunaamini Kwa kuona zaidi kuliko kusikia.

Saikolojia hiyo ni muhimu unapodili na Mwanamke.
Ukiwa MTU wa maneno ya kejeli na dharau Wanawake watakupita kushoto Sana. Hata uwe na Pesa au mzuri vipi.
Lakini ukiwa mzuri kwenye kuzungumza, kuwachekesha, na kutoa maneno matamu basi Wanawake watakupenda mpaka Basi.

3. Wanawake wanapenda wanaume wazuri wa Sura, wenye Akili na wajanja, na maumbile ya kiume.
Pesa Kwa Mwanamke ni ziada Sana.
Wanawake kiasili mpaka kwenye viumbe WA jinsia ya ke Kwa ndege, wanyama na Samaki. Hawanaga ujanja na madume yanayovutia Kwa Sura, wajanja wajanja, wanaojiamini. Watanashati.
Hizo Pesa zako kwao ni zuga tuu. Wanawake hawatakupenda Kwa sababu ya Pesa zako Ila watakupenda Kwa Sifa za Asili.

Ni ngumu Mwanamke kumsaliti na kumgeuka mwanaume anayempenda. Lakini ni rahisi Mwanamke kumgeuka mwanaume mwenye Pesa asiyempenda.
Mwanamke akikupenda kikamilifu atakutetea kivyovyote.

4. Wanawake ni Watu wa Sanaa kiasili.
Ni lazima ujue Jambo hili ili uweze kuishi na hao viumbe bila matatizo.
Wao wenyewe ni Sanaa tosha, Kwa sababu unaposema Sanaa ni ufundi na uzuri WA Jambo lolote lile.
Wanawake wanapenda ufundi na uzuri WA mambo.
Wanapenda urembo, mitindo, fasheni, Lugha za Sanaa, Swaga,

Wanapenda Drama, burudani, muziki, dance, vyakula vitamu, location Kali n.k.
Hawapendi Watu waliozubaa, wasio na jipya, Akili ndogo.

Ni kweli Wanawake wengi wanaakili Below ukilinganisha na Sisi wanaume, lakini kitu pekee ambacho Wanawake hawatokubali ni kuishi na mwanaume mwenye Akili ndogo. Lazima atampa shida.

5. Wanawake hawapendi mwanaume dhaifu.
Kujinyenyekeza hovyohovyo hawapendi mwanaume WA Sampuli hiyo. Wanapenda mwanaume ambaye anajiamini na mara Kwa mara anakuwa na matambo na majivuno, sio kila saa kulia Lia. Kutaka kudeka deka kama mtoto wa kike.

Mwanamke anapenda mwanaume asiyeogopa Kufa, shujaa ambaye yupo tayari kufanya maamuzi magumu kwaajili ya familia. Sio mwanaume dhaifu.

Mwanamke anahitaji mwanaume anayepiga show ya kibabe, asiye na kazi mbofumbofu. Uwe fundi kwelikweli.
Mwanamke yupo Radhi ukose yote atakuvumilia lakini sio kipengele hicho.

Mwanamke ukiwa unamkojoza na kumkamua mpaka anajisikia kweli yeye ni mwanamke, mikunjo, shughuli iliyokamilika, akitoka anajihisi mwepesi mwili wote umelegea sio magoti sio kiuno yaani anapepesuka, kamwe hawezi kukusumbua kivyovyote vile.

6. Mwanamke anapenda mwanaume anayegombewa na Wanawake wengi.
Mwanamke hapendi kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Anataka mwanaume mwenye Sifa zote za kiume, ili asifiwe na Wanawake wenzake au awadharau Wanawake wenzake,
Mwanamke kuwa na Mwanaume anayegombewa kwake ni heshima na ufahari.

Mwanaume kama haugombewi na Wanawake upo kwenye hatari ya kusumbuliwa na Mkeo. Kunyanyaswa na hata Wakati mwingine kunyimwa tendo la Ndoa.
Wanawake wanapenda kuishi Kwa mashindano, Roho juu. Wanapenda kuwatishia Roho Wanawake wenzao.

Ndio maana ni lazima kijana uwe na Sifa moja Kati ya hizi;
i) Uzuri, Mvuto na utanashati.
ii) uwezo wa kupiga mzigo kikamilifu
iii) Pesa
Uwe na kimojawapo au zaidi ya kimoja au vyote.

Mwanamke anataka sababu ya kukuonea wivu nje ya kukupenda. Sababu ni hizo nilizokutajia. Na hata Watu wa nje watajua wivu wa Mkeo unachochewa na kitu gani Kati ya hivyo.


Elewa kuwa, Wanawake wanajifanyaga hamnazo Makusudi ili wakupasue, yaani wanaweza kujifanya Hawana Akili ili ujichanganye na kushindwa kuwaelewa.

Mwanamke ni rahisi kumuelewa na kumjua mwanaume Kwa sababu Sisi wanaume tunapokutana na Wanawake tunalazimisha kuwa na Sifa kubwa kama Akili na Hali zetu za kifedha, huku wao wakiwa Low Key.

Elewa kuwa Mwanamke unapomuambia Jambo analipokea Kihisia kisha baadaye huenda kulitafakari Kwa Akili zake.
Ndio maana Leo anaweza kusema hivi lakini kesho akasema vinginevyo.
Hivyo unapomueleza Mwanamke Jambo lolote Kwa mara ya kwanza, mueleze Jambo linalopatana na hisia zake, kisha ukikutana naye mara ya pili libadilishe jambo lile lipatane na Akili yake. Hivyo ndivyo utakavyoendana nao.
Tunasema kuishi nao Kwa Akili.

Acha nipumzike
Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hili povu lote halieleweki unacho pinga na unachokubali kwa mwanamke kumvua tabia ya kutoeleweka, na inaonekana kuna utata juu ya kulifahamu vizuri neno
HUELEWEKI
 
Kumbuka binadamu ni kiumbe kinechotengenezwa na miungu Fulani Kwa wakati Fulani na matukio Fulani kama ilivyo wanaume .

Kuna viumbe wamejichanganya na binadamu ndio Wenye uwezo Wa kuongoza kiumbe Kinachoitwa binadam.
Mfano : Kuna Wakati Wanawake vipotable au slim walikua NDIO Wenye mvuto. Wakati huo Dunia nzima iliwekwa kwenye mtizamo Wa vipotable. Binadam wakajikuta WOTE wanapenda wanawake wembamba na vipotable. Wanawake wakawa Wanajinyima kula Ili tu wawe na maumbo membamba na madogo na uzito Mdogo. Wanaume wakawa wanawapenda wanawake Wa aina hiyo. Wale wasiokua na maumbile hayo walijichukia na kujiona hawana mvuto .

Ukaja wakati Wa Wanawake wembamba na warefu ikawa ni fasheni na mvuto Mkubwa.
HALIKADHALIKA wanaume kuna Wakati waliokua wanajazia vifua. Ikawa ni fasheni kubwa kabisa. Wakaja wanaume wembamba wasio na vitambi. Huku Wakiwa wamenyoa O. Ikawa ni fasheni . Ukaja fasheni ya kunyoa panki n.k.

Yote hiyo ni nyakati ziazoongozwa na viumbe waliofichika wanaojua Dunia inakoelekea. Baada ya hayo mara nyingi watu wanaishi Kwa matangazo kama vile binadam ni bidhaa lengo bado ni moja kuhamasisha ngono na inapokolea inakua Haina usalama na magonjwa yanaongezeka na Chuki baina ya wanaume na wanawake na Ndoa nyingi kuvunjika.

Sasa ni wakati Wa Wanawake Wenye matako makubwa na wanaume Wenye Pesa na matumbo makubwa Kwa Imani kuwa kitambi ni dalili ya kuwa MTU ana pesa. Kwa Sasa Hata mpiga kura hachagui MTU asiye na pesa. Hata mzazi hapendi mtoto asiye na pesa. Pesa inaleta utanashati, pesa inaleta starehe,pesa inamfanya MTU ajiamini,pesa inaleta kiburi,pesa inaleta majivuno,pesa inaleta Raha ,pesa inaleta mvuto ,pesa Kwa Sasa ndiyo Nguvu ya kiume.
Mwanaume asiye na pesa Inabidi alelewe na Mwanamke mwenye pesa Ili apate mvuto na kuwa mtanashati na kuweza kunyoa Hata nywele kwenye saluni NZURI na pafyum NZURI.

Ni wakati Wa Pesa Kwa Kila MTU. Hata Mbwa mkali mahiri anapatikana kwenye nyumba ya MTU mwenye pesa.
Ni kimefanyika ni ile ile Hali ya viumbe waliohusika katika kumuongoza binadam wamecharuka na kuweka pesa kwenye Agenda za kumwendesha binadam mana pesa ndiyo msingi Wa mengine Kwa Sasa.

Mfume dume umeasisiwa na wanawake.
Hakuna mfumo unaanzishwa na wanaume.Wanawake NDIO walimu Wa familia Tangu mwanzo. Mtoto Wa kiume yupo karibu ZAIDI na mama kuliko baba ,hiyo ni nature Haina ubishi. Anayesoma mara nyingi usishindane na Mwanaume ni Mwanamke,anayeiaminisha jamii kuwa Mwanaume lazima awe na mchepuko ni Mwanamke lakini kiuhalisia wanawake Wana MICHEPUKO mingi kuliko wanaume Kwa Ujumla wake. TATIZO ni moja Mwanamke ni mama hivyo ni rahisi sana kuwalea wanaume Hata Kumi Kwa wakati mmoja na WOTE wakajiona Kila mmoja anapendwa kuliko Mwingine na akaamini yupo peke yake. Hii ni akili aliyoumbiwa Mwanamke NDIO Maana anaweza kuwa na Watoto Kumi na huwezi kujua Kama anampenda Yupi ZAIDI, Hata kama Mmoja ni kichaa Bado atampenda Kama mwanawe.
Kusema kuwa Kuna MTU anayeweza kujua Kwa hakika anachotaka Mwanamke ni kudanganya watu na kutaka kuwafurahisha wanawake na kuwadhalilisha wanaume. Jamii imemdhalilisha sana Mwanaume Karne hili . Mwasisi Wa udhalilishaji Huo ni Mwanamke.

Mfume dume uliasisiwa na Mwanamke na mfume Jike utaasisiwa na Mwanamke.
Mabadiliko yote ya Dunia yemefanywa na Mwanamke.
Eva aliubadili Ulimwengu na uumbaji wake.
Delila alimuangamiza Mwanaume mwenye Nguvu Kwa pesa.
Sara aliasisi mfumo Wa ndoa za mitaala Kwa kushawishi Ibrahimu mumewe aoe House Girl wake.
Sara huyo huyo akamfukuza House girl na mtoto wake kinyama na kumfanya mtoto akose malezi ya baba yake na ndugu yake.

Mfano Mwingine ndani ya Biblia ni Yakobo na Esasu. Walikua ni mapacha lakini aliyewajengea uadui ni mama Yao baada ya KUFANYA njama ya kumdhulumu Esaú Haki yake Kwa kumpa Yakobo chakula Ili akamdanganye baba yake kuwa yeye ndiye Esaú. Lakini pia mama yao aliamua tu kuanzisha mfumo Wa kilaghai ambao NDIO unaougharimu Ulimwengu mzima mpaka Leo.

Mabadiliko na udanganyifu Mwingine uliofanywa na Mwanamke na ukaleta TATIZO ni MKE Wa Mfalme Farao kumsingizia Nabii Yusuf kuwa alitaka kumbaka. Ni mfumo mbaya uliasisiwa na Mwanamke. Mwingine ni MKE Wa Herode aliyemshawishi Binti yake aombe kichwa Cha Yohana Mbatizaji.
Mwanaume TATIZO lake ni moja Kudhani kuwa anaweza akamfurahisha Mwanamke Bila kujali madhara yanayoweza kutokea. Matokeo yake ni kuibuka Kwa Chuki na mifumo kandamizi. Aliyetaka kukandamizwa alikua ni Yohana Mbatizaji.Aliyetaka KUTUMIA nafasi yake kukamilisha unyanyasaji na ukandamizaji na mauaji yaYohana asiyekua na hatia ni Mwanamke.


Agenda ya Sasa ni moja kuhakikisha Dunia inakua na wanaume dhaifu wasio na nafasi katika jamii. Ukiwa na wanaume dhaifu na watawala na wasimamizi wengi wanawake basi ni wazi inakua na jamii inayowaza starehe tu muda WOTE. Matokeo yake ni kuibuka Kwa tamaduni zisizofaa kwenye kizazi chote.

Mwisho Wa Yote jamii inakosa wanaume Wenye kutamani kuoa mana wanaojiona kuwa WAKO chini ya wanawake walioasisi mfume Jike lakini pia jamii inapotoshwa Kuhusu Heshima ya ndoa na majukumu Sahihi ya wanawake ,hivyo wengi hukosa nia ya kuolewa. Panaibuka Suala la Ushoga na Usagaji.
 
Ww naye siku hizi mada zako hazieleweki zina tetea nn na zinakaa nini yaani zina pingana.

Mara uzi huu useme mwana mke ajaubwa kupenda bali kutii uzi mwingine unaseme wanawake wanaupendo kwa wanaume wazuri wa sura na utanashati.

Mara useme ili ndoa idumu na iwe na amani inahitaji iongozwe kwa mfumo wa zamani leo tena unasema mifumo za zamani ni kandamizi na mwana mke ana hitaji uhuru hapo sasa tukueleweje?

Suala la upendo halija wahi kuwa na kanuni yeyote kwa jinsia zote bali upendo kwa mtu fulani huwa unakuja tu automatic kwa mtu bila kujali ni mtu wa aina gani.

Kiufupi kila binadamu hapa duniani anajeelewa yy mwenyewe si kwa mwanamke wala mwanaume hayo mengine tuna changamsha genge tu.
 
Hayanaga muongozo, tatizo binadamuwa siku hizi ni wabishi sana...
 
Ww naye siku hizi mada zako hazieleweki zina tetea nn na zinakaa nini yaani zina pingana.

Mara uzi huu useme mwana mke ajaubwa kupenda bali kutii uzi mwingine unaseme wanawake wanaupendo kwa wanaume wazuri wa sura na utanashati.

Mara useme ili ndoa idumu na iwe na amani inahitaji iongozwe kwa mfumo wa zamani leo tena unasema mifumo za zamani ni kandamizi na mwana mke ana hitaji uhuru hapo sasa tukueleweje?

Suala la upendo halija wahi kuwa na kanuni yeyote kwa jinsia zote bali upendo kwa mtu fulani huwa unakuja tu automatic kwa mtu bila kujali ni mtu wa aina gani.

Kiufupi kila binadamu hapa duniani anajeelewa yy mwenyewe si kwa mwanamke wala mwanaume hayo mengine tuna changamsha genge tu.
Uko Sahihi.
Mungu alimuumba Adam akiwa mkamilifu na mwenye ufahamu Mkubwa sana na vitu vyote viliwekwa chini yake.

Mkewe Hawa au Eva alipoumbwa kasheshe ikaanzia Hapo. Shetani alijua wazi kuwa Mwanamke hawezi kuridhika na Kile anachopewa au alicho nacho. Hata vile alivyoumbiwa haridhiki navyo.mfano,kucha nywele , Kope n.k.

Eva alikua na Mwanaume wake aliyepewa uwezo na Sifa zote kuliko wanaume WOTE lakini aliamua kuasi na kumtii Shetani Kwa sababu ya kutaka kufanana na Mungu.

Alijua kuwa akifanana na Mungu Atakua Juu ya vyote akiwamu Adamu. Tamaa ya Mwanamke kamwe haiwezi kuifikiawisho na kuridhika. Mwanamke anapenda kitu kipya kinachosifiwa au Chenye kupendeza Hata kama kina madhara .

Ule uchungu anaoupata Mwanamke wakati Wa kujifungua angekua ni mwanaime asingezaa Tena. Tamaa ya mwanamke inamfanya kurudia Hata mara 10. Ndivyo alivyoumbiwa. Kwa hiyo hakuna binadamu anayeweza kumfanya Mwanamke aridhike na Kuona kuwa amefikia mwisho Wa mahitaji yake na matamanio yake yasiyo na mwisho.

Usione Kwa Nini wanawake wanajazana makanisani ,ni Kwa sababu wanatamani pia Kwenda MAHALI pa Raha milelele,japo hawawezi kujitoa kikamilifu katika matendo ya wema hasa ya kuwapenda wengine Hata pale wasipo stahili.
 
  • Thanks
Reactions: ITR
Taikon upo vizuri sana na lakini unasahau kitu kimoja cha msingi sana ambacho ni,"Mwanamke ni mwili tu bila kichwa na kichwa cha mwanamke ni mwanaume,sasa kosea uweke kichwa tofauti na mwili uone mziki wake",na kupata kichwa sahihi nayo ni kazi sana mpaka ufuate hatua maalimu kwa kutumia akili kubwa sana. Mwisho we ngoja uoe ndiyo utajua haujui!.
 
Kama biblia imesema tuishi nao kwa akili wewe ni nani wa kusema wanawake wanaeleweka?

Na huwezi ishi Kwa Akili Kwa kitu kisichoeleweka.
Akili mi ufahamu, ujuzi, uelewa, maarifa n.k.

Bado hujaelewa maana ya kuishi na Mwanamke Kwa Akili?
 
Taikon upo vizuri sana na lakini unasahau kitu kimoja cha msingi sana ambacho ni,"Mwanamke ni mwili tu bila kichwa na kichwa cha mwanamke ni mwanaume,sasa kosea uweke kichwa tofauti na mwili uone mziki wake",na kupata kichwa sahihi nayo ni kazi sana mpaka ufuate hatua maalimu kwa kutumia akili kubwa sana. Mwisho we ngoja uoe ndiyo utajua haujui!.

✔️✔️✔️
Well prepared, well summarised, well presented
 
Mwanamke unaweza kumnunulia nguo nzuri ila kuna msela akimsifia atampa utamu.
Unaweza kumpa hela ya Tax ila ikatokea jamaa akampa lift bure, ataona jamaa anamthamini sana kuliko wewe.
Unaishi na mwanamke, atagongwa nje na kubeba ujauzito lkn bado ataendelea kuishi kwako.
Unaweza kuwa na hela, gari, nyumba kali na unapeleka mashine lkn anagongwa na boda boda au msela tu wa mtaani.
Unaweza kuwa hauna kitu ila akagongwa na mwenye hela.
Ukiwauliza wanawake wengi watakuambia wanataka mwanaume mpole, anayemjua Mungu, siyo mkorofi na anayejua kuhudumia. Angalia wanaume walionao kwenye mahusiano? Ni play boy, wakorofi, wezi n.k
Ulisoma kisa cha jamaa wa mkongo na PS JF?
Unaweza kuona jamaa ni tajiri lkn ndoa yake inapumulia mashine lkn utakuta masikini lkn ndoa yake ina furaha.
"Ukiona unakaribia kumjua mwanamke, ujue unakaribia kufa" mimi mpaka kwa umri wangu huu, sijawahi kujua mwanamke anataka nini.
 
Mwanamke unaweza kumnunulia nguo nzuri ila kuna msela akimsifia atampa utamu.
Unaweza kumpa hela ya Tax ila ikatokea jamaa akampa lift bure, ataona jamaa anamthamini sana kuliko wewe.
Unaishi na mwanamke, atagongwa nje na kubeba ujauzito lkn bado ataendelea kuishi kwako.
Unaweza kuwa na hela, gari, nyumba kali na unapeleka mashine lkn anagongwa na boda boda au msela tu wa mtaani.
Unaweza kuwa hauna kitu ila akagongwa na mwenye hela.
Ukiwauliza wanawake wengi watakuambia wanataka mwanaume mpole, anayemjua Mungu, siyo mkorofi na anayejua kuhudumia. Angalia wanaume walionao kwenye mahusiano? Ni play boy, wakorofi, wezi n.k
Ulisoma kisa cha jamaa wa mkongo na PS JF?
Unaweza kuona jamaa ni tajiri lkn ndoa yake inapumulia mashine lkn utakuta masikini lkn ndoa yake ina furaha.
"Ukiona unakaribia kumjua mwanamke, ujue unakaribia kufa" mimi mpaka kwa umri wangu huu, sijawahi kujua mwanamke anataka nini.
Hahaaaa umezaliwa juzi kwani na umepiga shoo za kutosha hadi uwafahamu kiasi hicho🤣🤣🤣, wanawake ni mashetani wanaishi na kutembelea Nyumba za ibada na kusikiliza na kuimba nyimbo za dini daily ila hawaachi matendo ya Baba yao kipenzi shetwani
 
Back
Top Bottom