Wanawake punguzeni masharti ili muolewe

Unaweza kuandika ujumbe wenye kufikirisha na kutoa njia ya kuona mbele ila hilo jina lako linanipa ukakasi.
 
Hao ni wadada wa kwenye mitandao. Huku mtaani wanakuwa wapole sana
Hadi wakifika miaka 30 baada ya kuringa huku wakijuta waliowakataa wamekuwa smart guy na tayari wanamilikiwa na wengine
 
Kabla ya kuanza kuwafundisha hao wanawake,hebu jaribu kutafakari kuwa wewe ungekuwa ndio mwanamke,ungewakubalia wanaume wangapi kabla ya kujua kama huyu ni muoaji au muonjaji,maana kwa kumkubalia kila anaekuomba penzi ukidhani ni muoaji unaweza pia kuishia kuonjwa mpaka unazeeka...
 
Kwa taarifa yako kila ke ana mtu wake sasa sijui hao unaowasema umewatoa wapi.
 
Mfano kama Dar kila mtu anamuona mwenzake ni mwalibifu na kila mtu hana muda sahihi wa kutafakari mwenzake, labda tu muwe kanisa moja, sehemu ya kazi sio rahisi waliowengi ufika kazini na watu wao, mtaani nako sio rahisi ukizingatia unaondoka saa 12 na kurudi saa 3 usiku muda wa kuongea hapo katkati haupo, kwa mwendo huo utajikuta umegonga 30 bila kutarajia.
 
Shida ni wao wakitongozwa na mwanaume asiye na hela wanakataa ila akija mwenye pesa anakubali chap. Matokeo yake tumebaki kuwa na limbwi kubwa la masingle mothers. Wao swala la kuenda kuanza maisha na mwanaume asiye na kitu hawataki.
 
Shida inaanzaga pale wanapotaka "tall, dark and handsome" halafu wanataka wapate watoto weupe kama wazungu. Kwahiyo acha muda uwe mwalimu wao tosha maana ni ngumu kuwaelewa.
 
Unaweza kuwa sahihi kabisa. labda tunataka wanaume ambao ni Mr. Perfect tukisahau na sisi tuna mapungufu fulani pia.
wakati wa Mungu upo ndio. lakini kuna muda ni sisi wenyewe tunamiss the time.

kuna rafiki yangu alikutana na mwanaume mzuri sana anaupendo mcheshi kasoro si mkristo sana ila alijitolea kuwa tayari kupita njia anayopitia ya kumpenda Mungu kwelikweli.
sema mdada akiona hii kitu sio kweli kama ndoto akajiona anamadhaifu pia. Hafanani naye. So alimuacha mwanaume ambaye alikuwa ndio mme wake.

sasa yuko single mwanaume inasemekana ameoa japokiwa rafiki yangu alipomfuatilia ni kama bado hajaoa ila anamwanamke mzuri. so inategemeana na mtu na muda Mungu akimleta mume sahihi. so ladies take care!
 
Reactions: Sax
Sisi mahusband material tunaonekanaga kama mazombie,kisa hatuna range rover.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…