Wanawake vaeni mavazi ya heshima kwenye nyumba za ibada

Wanawake vaeni mavazi ya heshima kwenye nyumba za ibada

Pesanyingi

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2023
Posts
1,157
Reaction score
1,983
Hivi kwanini wanawake siku za ibada hasa jumapili, wanaifanya kama ni siku ya fasheni na kujionyesha kwenye kujipamba na mavazi tofauti na makusudi ya imani.

Kuna wanawake bila nguo mpya anaona ibada kwake haina maana(mashindano ya mavazi). Kuna wanake bila wigi jipya anaona ibada haina maana.

Wanataka wanapokuwa kwenye nyumba za ibada wameki tensheni badala ya kumuomba Mungu. Wengine wanaenda mbali zaidi kimatendo kwa kuvaa mavazi yanayowachora maumbile yao hadi ya ndani kwenye nyumba za ibada.

Rai kwa viongozi wa dini kemeeni hayo yanayofanywa na wanawake kwenye nyumba za ibada. Wengine watajitetea kuwa Mungu ana angalia moyo na siyo mavazi hilo si kweli.

Waliokuwa ibadani na wanaotaka kwenda Mungu awatangulie na muwe na jumapili njema.
 
Unaenda kusali au kuangalia watu wamevaaje..?
Alafu wewe utakuwa mnafki, maana ulitakiwa ku address tatizo eneo hilo ulipokuwepo kupitia right channel za kanisa unalosali. I am sure kuna namna yenu ya kupeleka malalamiko hapo unaposali ila wewe ukachagua kuja kuandika mitandaoni ambapo probably hao uliowalenga hawapo.

Luka 6:41 inasema hivi,

“Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.”
 
Wanaume tumeumbwa mateso, kila pahala tunapopita tunawindwa tena kwa competition kali. Ee mwenyezi Mungu tuepushe na hii shida maana watu wanamiliki magonjwa yakuogofya. 🙏
 
Wakemee wakose sadaka maana wao ndio watoaji wakubwa wa sadaka(natania tu)
Kusema ukweli hii tabia ya kuvaa mawigi inaboa sana,unakuta kashonea wigi,kichwani haogi kwani wigi litaloa.Sasa kama kichwa hakipati maji hapo hajaoga kapiga "pasipoti" tu,na nyie wanaume ambao wake zenu wanavaa mawigi kwenye nyumba za ibada waambieni ukweli waache kuvaa. Wapo KE wengine wanatafuta NDOA sasa kwa nini wasjirembe sana ili vijana muingie mkenge,kuna idadi kubwa sana ya KE ambao hawajaolewa sasa wanaona kwenye nyumba za ibada ndio kwa kwenda kujionesha.
 
I am sure kuna namna yenu ya kupeleka malalamiko hapo unaposali ila wewe ukachagua kuja kuandika mitandaoni ambapo probably hao uliowalenga hawapo.
Mkuu ulivyosema upo shua nikajua unaeleza njia ya kuwasilisha maoni au malalamiko iliyowekwa na kanisa la jamaa, kumbe umehisi tu. Rekebisha hapo kuwa unafikiri na sio upo shua.

Ila kuhusu kutoa maoni mitandaoni ni kwa ajili ya kusaidia wengi, wa kanisa husika la jamaa na wa makanisa mengine pia
 
Fanya kilichokupeleka church kamanda sidhani mtu spiritual anayeenda kujikeep busy kumsikiliza Mungu ataanza angalia mambo ambayo hayamuhusu,
Yote hiyo ni mapokeo ndio yameharibu kanisa ambalo ni mwili wako na sasa ukiamini jengo ndio sehemu takatifu wakati utakatifu upo ndani Ya mtu mwenyewe,

Mtu yeyote Power spiritual personal hawezi ku judge mtu maana kanisa ilitakiwa iwe shule ya watu walioshindikana kwenda kupokea Nuru ila maajabu wamegeuza ni sehemu ya kijiwe cha wanafki wanao igiza utakatifu wakati kusanyiko la kwanza alilolifanya Bwana Yesu lilikua kutaniko la watu wote bila kujalisha namna walivyo,
Jitafakarini na mfocus kuwahubiria watu Ufalme wa Mungu wakiupokea Mungu kupitia Roho Mtakatifu atawaongoza namna ya kuishi maana hatuishi kwa namna ya kimwili ila kiroho na haijawahi tokea mahali popote mtu awaongoze binadamu kua na Maadili maana binadamu ni kiumbe mbishi na mwenye hulka za ajabu bila Roho wa Mungu kuingilia Kati habadiliki ng'oo hata umshikie panga labda akufanyie unafki,

So ujumbe wangu ukienda kanisani fanya kilichokupeleka acha kuangalia watu wasiokuhusu!
 
Mkuu ulivyosema upo shua nikajua unaeleza njia ya kuwasilisha maoni au malalamiko iliyowekwa na kanisa la jamaa, kumbe umehisi tu. Rekebisha hapo kuwa unafikiri na sio upo shua.

Ila kuhusu kutoa maoni mitandaoni ni kwa ajili ya kusaidia wengi, wa kanisa husika la jamaa na wa makanisa mengine pia
Kila kanisa lina hizo taratibu za kupeleka malalamiko/ushauri na maoni.
 
Ukiona mwanamke na kimini kanisani malaya
Ukiona mwanamke matiti yanaonekana kanisani malaya
Ukiona mgongo wazi sana malaya
Ukiona mwanamke kavaa nguo yenye kuonyesha vya ndani( translucent clothes) malaya
 
Mleta mada unaogopa majaribu ajabu unataka kuiona pepo, jitafakari; hayo majaribu unatakiwa uyaone na uyashinde sio unakuja huku unaanza kulia lia.
 
Back
Top Bottom