Unaenda kusali au kuangalia watu wamevaaje..?
Alafu wewe utakuwa mnafki, maana ulitakiwa ku address tatizo eneo hilo ulipokuwepo kupitia right channel za kanisa unalosali. I am sure kuna namna yenu ya kupeleka malalamiko hapo unaposali ila wewe ukachagua kuja kuandika mitandaoni ambapo probably hao uliowalenga hawapo.
Luka 6:41 inasema hivi,
“Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.”