Wanawake vaeni mavazi ya heshima kwenye nyumba za ibada

Wanawake vaeni mavazi ya heshima kwenye nyumba za ibada

Wanawake wanapenda kuonekana sehemu yyte yenye uwingi wa watu.
Iwe kanisani iwe bar iwe msibani popote pale?
Ndio tabia zao na ndivyo walivyoumbwa
Hua nashangaa watu wanao jikeep busy kutaka kushindana na nature,
Yaani mtoa post ni Dume lisilojua kusoma intelligence ya wanawake,
Kiufupi hata Haya makanisa yamejigeuza mafarisayo ya kujudge watu,
Lengo la kanisa la kwanza ilikua watu walioshindikana ndio waende church (mkutano)
Ili wakahubiriwe ufalme wa Mungu ila ikaja badilika wanafki wanaojiita watakatifu wakageuza ni sehemu yao ya kukutana huku waliokusudiwa hawaruhusiwi tena
Usishangae now Shoga na kahaba akienda church na identity yake wanamtimua badala ya kumfanya awe karibu wampe ushauri kimwili na kiroho
Yaani lengo na kusudi la kanisa limepotoshwa
Maana ilitakiwa Wakristo
Waende church kama wanafunzi then wa graduate kisha watoke waende site kuhubiria watu ila maajabu mtu anaenda kanisani miaka kumi yeye ni nenda rudi na hakuna anacho upgrade zaidi ya majungu na Roho mbaya,

Kanisa (jengo)ndio sehemu pekee Mwanafunzi anabaki mjinga na hapigi hatua yeyote katika kile alichojifunza badala yake anageuka kondoo

Angalia kina Petro na wale 12 disciples walikaa na Bwana Yesu miaka mitatu tu wakijifunza baada ya hapo wakawa moto kuliko hata master wao yaani walipiga show nzima kiasi kwamba serikali ya Warumi ikatikisika tena kutoka kwa watu ngumbaru zero brain waliokutana na teacher wa mateacher ndani ya kipindi kifupi tu Waandishi na mafarisayo wakaonekana walienda somea ujinga!
😁😁
 
Wanawake wanapenda kuonekana sehemu yyte yenye uwingi wa watu.
Iwe kanisani iwe bar iwe msibani popote pale?
Ndio tabia zao na ndivyo walivyoumbwa
Hivi Tanzania ndiyo ile nchi ambayo wanafunzi wa kike wanavaa sketi ndefu zinazogusa kwenye vifundo vya miguu, lakini inaongoza kwa wanafunzi wa kike kupata mimba? Hivi ni ile nchi ofisi za serikali wanakaza wanawake waliovaa sketi fupi kupata huduma lakini inaongoza kwa nyumba ndogo?
 
Kwa asili mwanamke ni pambo na kiumbe cha maonyesho. Ukisha kubali hili unakula beer baridi unashika hatua zako
 
Lakini yote haya shina lake ni fedha, wahubiri wengi hawakemei maovu sababu ya kuogopa kukimbiwa na waumini maana weteja wengi ndio hawa hawa wanawake na kama tujuavyo watu wanapenda kubembelezwa ,kupewa fake hope ukweli siku zote ni mchungu
 
Kuna wanawake wao wanapenda kukaa siti za mbele... Wana vaa nguo fupi..

Kiongozi ukiwa juu pale kwenye mimbari unapata shida ya kufuta jasho tu shingoni na usoni. Pages na mistari unatamka mara 3 tatu ila unatafuta tu huoni..

Ukiongea jambo la kuchekesha ndio utajutaaa... Vile wanacheka kwa kujiachia bhas kila kitu utaona ndani ndani hukooo..... Ndio macho yapo na yanaona! Hilo sio la mjadala.. Kosa ni lao wavaa hovyooo...

Baadae Kiongozi na jambo langu naomba nikushirikishe... Niweke kwenye maombi.... Hili na lile.. Mara namba ya simu... Ni sms na calls tu... Kiongozi nimepita kwenye hili.. Mkwamo hapaa... Sasa SAUTI nayo ni kama u.chi tu... Ukiweka sikio vibaya ukasababisha sauti hiyo I connect na kile uliona front seat kanisani ndio kwishaa... Njoo niombee nyumbani.... Hahaha... Kama Isaka na kuni zake.. Kondoo hakujua ni YEYE.....

Roho ya Yezebel at work... Vijana wengi wameanguka.... Ole.. Ole.. Ole.. kwa babilon na mama wa ukahaba... Kwa uzuri na urembo wake na vile amepambwa amewaangusha wengi.
 
nimefika tu kanisani mlangoni nikavutwa na wazee wa kanisa kisha wakanifunga kitenge,,sjui niliwakosea nini😫😫
 
Halafu sisi Wachungaji tukianza kuwapiga miti waumini wasiojiheshimu kama hao jamii inaanza kutulaumu. Kuwapiga mbupu ndo dawa yao.
 
Just imagine...."Feel free Church," and what you expect..?
 
Kama unaongozwa na njaa pamoja na tamaa basi utatishwa na utatishika na utatikiswa na kutikisika.

Waache wavae wewe kikubwa usigawe attention kwa mke ambaye haujamuoa
 
nimefika tu kanisani mlangoni nikavutwa na wazee wa kanisa kisha wakanifunga kitenge,,sjui niliwakosea nini😫😫
Una bahati umekutana na Wazee wa Kanisa wa kiroho hasa. Mimi ningechukua mawasiliano tayari kwa ajili ya kukukaza.
 
Unaenda kusali au kuangalia watu wamevaaje..?
Alafu wewe utakuwa mnafki, maana ulitakiwa ku address tatizo eneo hilo ulipokuwepo kupitia right channel za kanisa unalosali. I am sure kuna namna yenu ya kupeleka malalamiko hapo unaposali ila wewe ukachagua kuja kuandika mitandaoni ambapo probably hao uliowalenga hawapo.

Luka 6:41 inasema hivi,

“Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.”
Mkuu,
Acha kutetea vitu viko obvious aisee. Kukiwa na ovu lolote likemewe bila kujali watu wanasemaje. Kama mleta mada nae ana ovu lake basi litakemewa vile vile ila swala la mavazi kwa baadhi ya wanawake kwenye nyumba za ibada ni la kuangaliwa na viongozi husika.

Tukemee uovu, watu wavae kwa stara kwenye makanisa yao.
 
Back
Top Bottom