Wanawake wa Afrika walitumia Mitindo ya Nywele zao kutengeneza ramani za kutoroka Utumwani Miaka ya 1800

Wanawake wa Afrika walitumia Mitindo ya Nywele zao kutengeneza ramani za kutoroka Utumwani Miaka ya 1800

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Inawezekana umesikia mitindo mbalimbali ya nywele kama vile twende kilioni au kilimanjaro.

Hiyo mitindo haikuja tu hivi hivi. Kuna Wanawake enzi za Utumwa huko walikuwa na akili za ajabu sana.

Inadaiwa kuwa wapo waliotumia nywele zao kuwasiliana kwa siri au kwa mafumbo ili wasikamatwe na Askari wa Kikoloni.

Kupitia mitindo hiyo ya nywele waliweza kuonesha idadi ya Barabara na njia zinazoweza kutumika kutoroka Utumwani, ambapo mtindo maarufu ulikuwa ni mistari myembamba iliyonyooka kwenda nyuma maarufu kama twende kilioni.

Pia, inaelezwa kuwa walibuni mitindo mbalimbali kuonesha vikwazo au vizuizi ambavyo wangeweza kukutana navyo katika safari zao na hivyo kuweza kuwasaidia wengine kupata taarifa inayokusudiwa.

Mistari ya nywele iliyopindishwa ilitumika kuashiria uwepo wa chanzo cha Maji au Mto.

Milima ilioneshwa kwa mtindo wa nywele maarufu kama Bantu knots. Sehemu iliyokuwa na askari walisuka mistari mipana ya Nywele na ilifahamamika kama "Tropas" ikimaanisha Vikosi.

Kupitia mitindo hiyo ya Nywele waliweza kuhifadhi vipande vya chakula na Punje za Vyakula kama za mchele ili wasipate shida ya Njaa huko waendapo.

Lakini pia waliweza kuhifadhi vito vya thamani kama dhahabu.

Haya! Mbali na mwonekano tu, nywele zako zinaweza kukusaidia kwa lolote ukipata janga au ndio zitatumika kama kamba ya kukunyongea? Natania tu Mdau!
 
Nayo pia ni sehemu ya ubunifu...
 
Back
Top Bottom