Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
saana baharia..hata mpaka hapa ilipofikia kwani kujapata hata tekniki moja!? hahaNahisi tutajifunza mengi hapa mabaharia!
awali ni awali ndugu miaka ya 2010 nikiwa huko chuo pale mlimani city ndo ilikua kiwanja hatari...
karibu moshi na arusha....au uje marangu mtoni kabisa kwa wazee
KWANZA NAPENDA NIWAOMBE RADHI WADAU MLIOKUWA MNASUBIRI MUENDELEZO! KIFUPI WAKATI WA ASUBUHI NA MCHANA NAKUWA BUSY NA SHUGHULI ZA MAISHA NA KAZI NDO MAANA NASHINDWA KUMALIZIA HATA JIONI NIKIWA HOME MAMBO MENGI ILA BADAE YA LEO KWENYE SAA MOJA MBILI HIVI SAA ZA EAT NITAKUWA NIMEMALIZA MUENDELEZO ASANTENI
wewe ndo huelewi kitu wapi nimesema kuwa ni miaka 2010!? hapo nimesema nilisoma..hii story ndugu yangu ni mwaka huu 2019 mwezi wa kwanza!Lakini kipindi hicho kulikuwa hakuna bar maeneo hayo inayopiga karaoke mpaka hapo ushakuwa muongo bar kubwa ilikuwa catalunya
wewe ndo huelewi kitu wapi nimesema kuwa ni miaka 2010!? hapo nimesema nilisoma..hii story ndugu yangu ni mwaka huu 2019 mwezi wa kwanza!
Unatumia simu gani ? Tuanzie hapo kwanza 🤔Kifupi mimi naishi countryside na huko Dar nilisoma tu mavyuo na hivyo mimi siku hizi huja kwa kupumzika na matembezi mafupi kwenda znz nk au kufanya deal moja mbili tatu kisha nasepa huku mikoani ambao ndio watu tunaoishi maisha tunaishi! no bughudha no stress na pilikapilika za maisha ya huo Dar.
Sasa bana mimi niko vizuri sana ...kifupi hela ninayo kifupi sijapungukiwa iwe mi ndinga au mijengo. Ila nikiwa Dar kwa kuwa napenda kuwa huru na kujiachia maana mimi huwa najiweka simple saana vyeo na cadre niliyonayo ukiniona huwezi dhani. Kifupi napenda kuishi maisha to the fullest.
Kuliko nipande uber au tax nikiwa Dar mm huwa napenda nipande daladala au mwendokasi kutegemea na uharaka wangu wa siku hiyo lakini haimaanishi sipand hizo vingine. Sasa kupanda Daladala huko ni kwa ajili nipate kujichanganya nione maisha ya watu na masumbuko ya binadamu jijini Dar. Kifupi nimeona watu Dar kila mtu stress kwa kumsoma tu uso na gestures zake. Maisha yanapiga watu saana Dar.
Sasa nirudi katika mada..mara nyingi nimekuwa nikiona mademu wa Dar katika Daladala au nikiwa posta au mwenge nk kule kwenye malls mbalimbali yaani mademu utamuona classic kama malaika...yaani mtoto mzuri alivojiweka utadhani anakunya katika choo cha dhahabu ila sasa jitahidi kuwajua utasikitika.
Nilishawahi fanya uchunguzi kama huu ila nikasema nirudie tena..kuna siku nilikuwa nimepanda Daladala kifupi nikamkuta du moja kwenye seat jiran kwanza nikamsalimu hakuitika alikua busy na simu mi earphones masikoni nini...yaani ukimuona Utadhani beyonce..ooh nikasema no sweat haina tabu nikaketi. Tukawa kimya mimi natafakari uturi ananukia yaani utadhani mtoto ametoka mbinguni. Basi konda akawa anachukua nauli mimi nikampa elfu kumi note maana kiukweli huwa natembea na hela kama hizo tu..bas konda akasema wawili!? duh nikawaza nikasema okay wawili kata nikimaanisha na yule duh. Ifahamike yule Duh alikua busy na m simu wake ile wakati narudishiwa change ndo akawa kama ameona ni suala la nauli akawa kama anatoa yake nikamwambia usijali nimeshakulipia. Akasema ooh realy?? why?? no way huna haja kunilipia..mm nikamwambia no problem sisi binadamu tu niliona vema kufanya hivyo kwa wakati huo sahihi no strings attached na ajisikie amani. Akawa kama ananiangaliaa kunipimiaa kisha akasema ok thanks. Basi ukimya ukatanda tena ikumbukwe mimi nilikua nataka kwenda maeneo ya mlimani city ila jamaa angu fulani akaniambia mlimani city hakuna issue nimfate sijui wapi pale chini mkabala na mlimani city kunakuaga na karaoke nini panahappen sana. Basi nikawa nashukia pale kituo karibu na kwa kakobe. Mara na yule du akawa anashukia hapo..nikasema kimoyo moyo hebu ngoja nirushe nyavu hata kama demu anaonekana mtoto wa kigogo. Basi nikashuka na yeye akashuka pale basi mimi sikuvunga nikavunja ukimya oh ni kumbe tunashuka kituo kimoja naona ni bahati sana kwangu!? akanigeuka akawa kama like what!? nani huyu ananiongelesha! ikawa kama alivogeuka kuniona mimi kama vile akawa anataka kusita na kuignore ila kifupi mimi kama nina charisma hata kama najiweka simple sana ila maduu wengi wakiniangalia napata sana kibali kwao yaani sikataliki. Yaani niko charismatic nilishaambiwa na wengi hata huyu hapo baadae. Basi akaona no sweat anijibu tu kwani shi ngapi!? basi akasema yah nashuka hapa...huku akiwa busy kama kuondoka. Nikamwambia hey hunijui sikujui ila ningependa nikufahamu! akanijibu what!? what are you talking about! ikumbukwe mimi nilikua naongea kiswahili ila duh viingereza vingi bila yeye kujua hiyo lugha mimi ndo ya kwanza kuongea mpaka nilipofikisha miaka sita kurudi Tz na wazee. Mimi sikutaka ligi nikabaki na kiswahili...nikarudi ndio nahitaji kukufahamu najua uko busy na yako na mimi pia niko busy ila nahitaji nikufahamu ( huku nampa simu yangu aweke namba yake nimemuwekea kabisa moja kwa moja kwenye kusave contact...Dem akawa kama ananitazama kwa dharau sio dharau yaani kama vile hanielewei na hanimalizi hivi. Ila kwa kuwa pale kituoni kuwa watu wengi na mimi nimejitoa ufahamu basi akawa kama automatic hivi amepokea simu yangu na kuweka namba yake...nikasema kimoyomoyo yeess..aliponikabidhi simu nikafanya kama kuhakiki namba kwa kumpigia kisha nikamwambia ya kwangu hiyo save na kumtajia jina.
ITAENDELEA.........
Is that Yes ?[emoji38][emoji38][emoji38]
nokia ya tochi mkuu! unadhani mm ni ka wewe mwanaume wa Dar simu ya milioni ila umekopa salio la 500..mm simu yangu ya elfu 20 tu nipe namba nikupe salioUnatumia simu gani ? Tuanzie hapo kwanza [emoji848]
hii sio story ni life story yangu halisi mkuu..hivyo naandika navyotaka..na ww soma utakavyoMbona imekuwaa fashion story zenu kuzigeuzaa kuwaa series Nani kawalogaaaaa
nikisubiri unisifie nitasubiri sana..tatizo wanawake wa Dar mnashindwa tofautisha kati ya mtu anayeongea maisha halisi na yule anayejisifia...unataka sasa stori niandikaje kiaje yaan nidanganye!?Unavyojisifia sasa mkuu, utakua muhaya ww sio buree
Haya ndio madhara ya kukosa ajira.
Interesting