Usiombe ukutane na mshangazi ambao upo toxic! Nilikutana na mmama wa dizaini hiyo yani nilijuta. Nimemtoa out, hata msosi haujafika anaanza kuponda wahudumu na kuwafokea.
Ilikua ni restaurant flani classic huko kanda ya ziwa, ukiagiza menu wanaenda kukuandalia kabisa unavyotaka wewe kwahyo inabidi usubiri kama dk15-20 ili uletewe msosi wako.
Basi nikaagiza maji. Yakaletwa maji ya Dasani! Akaanza kumfokea muhudumu, "hoteli gani hii hamna maji ya kilimanjaro!!!". Yule dada akamjibu kistaarabu tu "madam tunayo nakuletea" akaenda kumchukulia.
Moyoni nikawa najisemea tu, leo nimeyakanyaga!!! Sipendi mtu anaemfokea muhudumu. Order ikakamilika. Nikaletewa wali na samaki sato mkubwa sana na juice ya nanasi. Yeye aliagiza chips akaangiwe na mayai matatu pembeni, aletewe na sato mkubwa! Mimi na njaa zangu nikawa nafakamia tu msosi wangu huku nikienjoy taratibu.
Mwenzangu nikaanza kumuona anazipekua pekua zile chips kama takataka yani, huku anaponda sijui zimekauka sana. Wakati mm naona ziko poa tu. Akawa anamdonoa donoa yule samaki na kulalamika hana ladha. Dah! Akaita muhudumu akaanza kumfokea wamepika vibaya! Yani aibu niliona mimi. Tatizo nilikua na upwiru hatari.
To cut the story short. Baada ya tukio lile yule madam alikula block!