Wanawake Wa Kigogo Mungu mmemkosea nini?

Wanawake Wa Kigogo Mungu mmemkosea nini?

Kuna wimbo mmoja wa Prof Jay una mstari unasema 'bora kumcheka mchafu kamwe usimcheke kilema'..... Itoshe tu kusema Mungu tunusuru waja wako kwa kukashifu uumbaji wako.
 
Sijapendezwa kabisa na uzi huu. Huwa nakasirika na kusikitishwa sana mtu anapomkejeli mtu kutokana na maumbile yake ya asili Mungu aliyomjalia. Binadamu tumeumbwa tofauti wengine warefu, wafupi, weusi, weupe, walemavu, wanawake, wanaume, nk na tunatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine kulingana na asili au mazingira aliyotuweka Mungu au tunayoishi tukiwa na tamaduni tofauti.

Kwa ufupi hakuna mtu aliyechagua kuwa jinsi alivyo. Sasa wewe unapomcheka nwenzako ulitaka afanyeje wakati siye yeye aliyeamua kuwa hivyo?! Ni jambo baya sana kuwacheka watu mara mseme wanawake wa kichagga hawana matako makubwa nk. Hivyo ndivyo Mungu alivyoamua sasa wafanyeje?

Kejeli zenu ndizo zimesababisha wanawake kuhangaika na madawa ya kuongeza makalio, kubadili rangi ya ngozi, kope nk mbaya wakiathirika mnaanza kuwacheka tena! Acheni Mungu aitwe Mungu kila Moja aheshimu mwenzake jinsi alivyoumbwa!



Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekupenda bure
 
Back
Top Bottom