Wanawake wa kijiji cha Magingo, kata ya Mkongotema wilayani Madaba mkoani Ruvuma, wapo hatarini kupata magonjwa ya zinaa kutokana na kukumbwa na vitendo vya ukatili wa kingono vinavyofanywa na baadhi ya wanaume katika maeneo ya mashambani.
Wanawake hao wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kukomesha vitendo hivyo vya ukatili na udhalilishaji wa kingono vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya wanaume, wakisema hali hiyo imeendelea kuhatarisha usalama wao na kuathiri shughuli za uzalishaji mali.
Mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Ndile amewataka viongozi wa kijiji cha Magingo kuitisha mkutano wa wananchi kwa lengo la kuwabaini wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria