Wanawake wa Kisabato ndio wanaoiishi Injili

Wanawake wa Kisabato ndio wanaoiishi Injili

Umaskini wako ndio unaokusumbua. Kama huna hela ya kusukia mitindo ya kupendeza usijifiche kwenye usabato!
Ha,ha,haaa! hilo nalo neno tukijipamba kwa nje tusisahau kupamba miyoyo. maana mwingine hajipambi kwa nje ila ndani ameoza.
 
Kama hujui ibada za RC ziache, ibada za Roman Catholic nilazima somo litoke Agano la kale na jipya, ila siwezi kukulazimisha kukubali.

Sent using Jamii Forums mobile app
sasa wewe ndio umepotea kabisa. hebu chukua kanisa la roma la leo, hata lile la Vatcan kwa Papa, linganisha na kanisa la mitume wale wa awali kina Petro na baadaye kina Paul. jinsi walivyokuwa wanahubiri, jinsi walivyokuwa wanajazwa Roho Mtakatifu, jinsi walivyokuwa wanafanya miujiza (sio kama ya kina mwamposa na hao manabii wa uongo, ila miujiza ya kweli), unafikiri Roma bado ni kanisa la Mungu? yule Mungu alionekana awali bado yupo? kama hayupo anaonekana kwenye makanisa yepi siku hizi? jibu unalo.

muda si mrefu vatcan wana mpango kuhalalisha hata ndoa za jinsia moja. mambo ambayo mitume wamekemea hadi wanakufa.
 
ukristo wa kimwili ni kujilisha upepo, hata ujifanye kubadilisha sauti na tembea uwe kama Yesu hutafika mbinguni. Mungu ni Roho, nao wamwabudui imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli, sio katika mwili na kweli. kwa matendo ya mwili hakuna aliyefanikiwa na hakuna atakayemwona Mungu. wanawake wa kisababo na wasabato wote wanajitahidi sana kwa nguvu za mwili kushinda dhambi na kufuata Neno la Mungu, lakini hawawezi, hakuna mwanadamu aliwahi kufanikiwa hilo.

Kinachotakiwa ni kujazwa Roho Mtakatifu baada ya kuokoka ili uongozwe na Roho. Mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria, kwasababu Roho ndio atakuongoza ufanyeje na usifanyeje.

pia, Yesu alisema huyo Roho akija atawaongoza na kuwatia kwenye kweli yote, which means yapo mambo mengi sana ambayo hayajaandikwa kwenye Biblia na ni dhambi, utayatambuaje? kwa kuongozwa na Roho. ukishika tu hizo amri kumi bado huwezi kufika mbinguni kwasababu yapo mambo zaidi ya hayo ambayo ni dhambi na hayajaandikwa.

dunia inabadilika, enzi Biblia ilivyokuwa inaandikwa hata hizi computer na tech zingine hazikuwepo, uelewa wa mambo ulikuwa tofauti na sasa, na wale walengwa walikuwa mbalimbali wa aina mbalimbali. jiulize, wanaposema enyi watumwa watiini mabwana zenu, kwan siku hizi bado kuna utumwa na biashara za utumwa? ilikuwa kwa nyakati hizo. kwa nyakati hizi yapo mengine bado yanatufaa ila mengine yanaongezeka na ni Roho anatujulisha moyoni kwamba hilo sio.

ninyi wafuasi wa MUSSA, kwani, enzi hizo zilivyokuwa jino kwa jino, ukiua unauliwa, alipokuja Yesu si alisema kisasi ni chake Mungu?

wasabato mtaumiza sana miili yenu kwa kujitahidi kumpendeza Mungu na mwisho wa siku mtaenda motoni wote. siongei kwa chuki wala kwa ushabiki ila kwa aliyenielewa ameelewa.

nideclee interest, mimini mpentecost, naamini kuokoka na kujazwa Roho Mtakatifu. kwa kuongea hayo hapo juu simaanishi vyote wanafanya wachungaji na manabii wa siku hizi ni sahihi, wengi wameingia kama magugu wamechafua upentecost pia, hao kina mwamposa na wengine. lakini ukweli upo palepale, awaye yote asipokuwa na huyo Roho wa Kristo, huyo sio wangu. ukiwa na Mungu moyoni utajua, usipokuwa naye utajua. lakini utajua kama alishawahi kuwepo kwako hata maramoja tu. Mungu akiwa moyoni mwako hakuna maswali, anayajibu automatically kufumba na kufumbua, hata ndoto za Kimungu kama wewe una Mungu ni dhahiri, hutaenda kuuliza, zaidi sana labda umuulize yeye. Okokeni mponye nafsi zenu.

wokovu ule wa mitume kumi na mbili, ule wa kujazwa Roho Mtakatifu nakunena kwa lugha, wasababu wanaukataa. wanataka kufuata Mungu kwa kujitahidi kwa nguvu za mwili na akili, sasa Yesu alikuja kufanya nini? na kwanini aliwaambia wabaki Jerusalem hadi wajazwe Roho? na baada ya Kujazwa Roho walibadilika hawakubadilika? walinena kwa lugha hawakunena? wasabato wanayo imani ya aina hiyo?

Wasabato huwa hawaokoki,hawaamini wokovu,na kama mtu hajaokoka kuingia dhambin ni kugusa
 
Kama mmeamua kuifata injili ifatwe inavyotaka, kuipinga injili ni uovu

1 Timotheo 2 :9
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani.

Nenda makanisa mengine ukute aatu walivyotengeneza nywele
Mmeshaanza kutumia usabato kutafuta wachumba?Maisha siyo kivile!😂😂😂😂
 
Mbona hata wanawake wanaosaki Kwa kakobe nao hawavai mapambo kama dhahabu,Kwa hiyo si wasabato tu
 
Kila la heri kwao
Kama mmeamua kuifata injili ifatwe inavyotaka, kuipinga injili ni uovu

1 Timotheo 2 :9
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani.

Nenda makanisa mengine ukute aatu walivyotengeneza nywele
A
 
Hili jambo linategemea na kanuni zinazokubalika katika jamii Wakristo tujipime kwa WAGALATIA 5:22-23"Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.

Lakini pia 1.YOHANA 4:7-8"Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo".

Na 1.WAKORINTHO 13:13"Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo".

1.SAMWELI 16:7"Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo".

Chamsingi kwa Mungu sio hayo mavazi...namna tunavyovaa .

Hataungejifunika kiasi gani...Hadi pengine mwili usionekane hata chembe,kama maisha hako hayana reflection ya upendo,wewe si kitu mbele za Mungu

1.WAKORINTHO 13"Kama ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au toazi. Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu".
 
Kama mmeamua kuifata injili ifatwe inavyotaka, kuipinga injili ni uovu

1 Timotheo 2 :9
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani.

Nenda makanisa mengine ukute aatu walivyotengeneza nywele
Wengine wachawi tu hakuna cha usabato Wala nini.
 
Back
Top Bottom