Wanawake wa Kisabato ndio wanaoiishi Injili

Umaskini wako ndio unaokusumbua. Kama huna hela ya kusukia mitindo ya kupendeza usijifiche kwenye usabato!
Ha,ha,haaa! hilo nalo neno tukijipamba kwa nje tusisahau kupamba miyoyo. maana mwingine hajipambi kwa nje ila ndani ameoza.
 
Kama hujui ibada za RC ziache, ibada za Roman Catholic nilazima somo litoke Agano la kale na jipya, ila siwezi kukulazimisha kukubali.

Sent using Jamii Forums mobile app
sasa wewe ndio umepotea kabisa. hebu chukua kanisa la roma la leo, hata lile la Vatcan kwa Papa, linganisha na kanisa la mitume wale wa awali kina Petro na baadaye kina Paul. jinsi walivyokuwa wanahubiri, jinsi walivyokuwa wanajazwa Roho Mtakatifu, jinsi walivyokuwa wanafanya miujiza (sio kama ya kina mwamposa na hao manabii wa uongo, ila miujiza ya kweli), unafikiri Roma bado ni kanisa la Mungu? yule Mungu alionekana awali bado yupo? kama hayupo anaonekana kwenye makanisa yepi siku hizi? jibu unalo.

muda si mrefu vatcan wana mpango kuhalalisha hata ndoa za jinsia moja. mambo ambayo mitume wamekemea hadi wanakufa.
 

Wasabato huwa hawaokoki,hawaamini wokovu,na kama mtu hajaokoka kuingia dhambin ni kugusa
 
Mmeshaanza kutumia usabato kutafuta wachumba?Maisha siyo kivile!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mbona hata wanawake wanaosaki Kwa kakobe nao hawavai mapambo kama dhahabu,Kwa hiyo si wasabato tu
 
Kila la heri kwao
A
 
Hili jambo linategemea na kanuni zinazokubalika katika jamii Wakristo tujipime kwa WAGALATIA 5:22-23"Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.

Lakini pia 1.YOHANA 4:7-8"Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo".

Na 1.WAKORINTHO 13:13"Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo".

1.SAMWELI 16:7"Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo".

Chamsingi kwa Mungu sio hayo mavazi...namna tunavyovaa .

Hataungejifunika kiasi gani...Hadi pengine mwili usionekane hata chembe,kama maisha hako hayana reflection ya upendo,wewe si kitu mbele za Mungu

1.WAKORINTHO 13"Kama ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au toazi. Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu".
 
Wengine wachawi tu hakuna cha usabato Wala nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…