Wanawake wa sikuhizi nani amewaroga?

Braitfyucha

Senior Member
Joined
Feb 22, 2019
Posts
163
Reaction score
187
Habarini wakuu,,
Niende mojakwamoja kwenye mada
Ni kweli kwamba wanawake ndoto yao kubwa huwa wanawaza kuolewa
Yani hilo hata halina mpinzani
wanawake siku zote wanawazaga katika fikira zao kuwa ipo siku atapata mume ataolewa atakuwa na familia yake(Women can't think beyond marriage).

Sasa siku hizi sijui ndo zama zimebadilika wanawake wengi wanafikiria kujiongoza,,wanafikiria kuwa na maisha yao,wanafikiria kujenga alafu wawaoe wanaume wanaopenda mtelemko
Cha ajabu pamoja na kuwa na mipango mikakati yote hiyo wanaishia kwenye kudanga tu
Kauli za wadada wengi utasikia anasema hataki ndoa,,hataki kuwa chini ya utawala wa mwanaume anataka kuwa na maisha yake
wakati huo hata uwezo wa kutafuta mia mbili hana anategemea kudanga kwa wanaume ili apate pesa.
Hata walio kwenye ndoa wanasema wamechoka manyanyaso ya wanaume eti wanataka kuwa na maisha yao
Ndo huwa nabaki najiuliza inamaana anataka kutoka kwenye ndoa aende mtaani kudanga?,
Kuna waliohitmu vyuo na kubahatika kupata kazi nzuri tu lakini maisha yao hayaeleweki kwakukosa mwanaume sahihi wakuwaongoza kama ni mimba basi wametoa sana mpaka wamechoka wakaamua kuzaa kiholela yaani unakuta ana watoto watatu kila mtoto na baba yake

Mwanaume anamchango mkubwa sana katika maendeleo ya mwanamke
wanawake mlioko kwenye ndoa acheni ukorofi,acheni kiburi
watiini waume zenu
Wadada ambao hamjaingia ktk maisha ya ndoa omba Mungu akupe mume wa kujenga nae familia
Usijidanganye unaweza kuishi tu hivyo hivyo utaishia kuiba waume za watu au kudanga alafu maisha yako yatakuwa mafupi zaidi.

ova..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sizani kama watakuja hapa.... Wataishia kusoma na kuondoka kimyakimya

Love and peace
 
Umesema mwanaume ana mchango mkubwa kwenye maendeleo ya mwanamke?? Si kweli, kwa hilo umepuyanga. Kama unazungumzia maendeleo ya familia sawa lakini kama unaongelea maendeleo binafsi ya mwanamke si kweli, mwanamke akishaingia kwenye himaya ya mwanaume anakuwa si huru tena na kama amepata mwanaume ambae si mwelewa uchumi wake utakuwa umeishia hapo, career yake anaizika hapo na kila kitu kinachomhusu yeye binafsi anasahau anabaki kuwa msikilizaji mtulivu. Wanawake wengi waliofanikiwa ni wale walioko singo au walioolewa na wanaume waelewa wasiofinya uhuru wa wenza wao(ila wanaume wa hivi wako wachacheee)

Sent using Jamii Forums mobile app
 

😂😂 umeiskia ile nyimbo ya chemical?? #nitajioa
 
[emoji23][emoji23] umeiskia ile nyimbo ya chemical?? #nitajioa
Kwa kweli Mimi nataka kuolewa sio kujioa .....hapa nawaza ule usiku wa saa nane mmejiamsha na mumeo mnaamsha hisia mnaingia mzigoni na kausingizi kenu ....hebu kwa kweli mi nataka ndoa ...

Jamani anaetafuta mke nipo hapa hahahahahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binadamu tunategemeana sana kama ambavyo tuna mchango kwao basi nao wana mchango kwetu. Mchango waweza kuwa hali au mali na kwa kiasi kikubwa pande zote mbili wanachangia sana kwenye maendeleo yetu ni vile tu tunakuwaga wabishi kulikubali hili.

Wanawake wengi wenye mafanikio ukiangalia historia iliyo nyuma yao huwa kuna nguvu ya mwanaume either posively au negatively na kumbuka mwanaume huyo aweza kuwa ni baba yake pia.

Negatively ni ile umekunyanyasa ukaamka ukaamua kupambana hadi ukatoboa, positively ni ile amekutia moyo akaongezea na pesa then ukapambana ukapasua. Upande wa kutupa sapoti kifedha wanaume wako vizuri, ni watoaji wazuri tu ukiachilia wale wenye roho za kimasikini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…