Wanawake wajawazito watafuta wanaume bandia kupata kadi ya kliniki

Wanawake wajawazito watafuta wanaume bandia kupata kadi ya kliniki

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wakina mama wajawazito wilayani Kilindi mkoani Tanga wamewalalamikia wanaume wanaowapa ujauzito kukwepa kwenda kliniki kupima afya zao kama kanuni zinavyodai hali inayopelekea wakina mama hao kutafuta wanaume wengine kwenda nao kupima ili waweze kupata kadi ya kliniki.

Hata hivyo ITV ilimtafuta mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Kilindi Abubakari Makengwa ili kuthibisha swala hilo nae akakiri kuwepo kwa tabia hiyo kwa baadhi ya wanaume.

Aidha, Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya Dr Daniel Chochole nae amekiri kuwepo kwa hali hiyo ila amesema wanaendelea kutoa elimu kwa akina baba wenye tabia hiyo.

CHANZO: ITV
 
Na bado wanataka watu wajifungulie hospital na kilnik wahudhuriei, failure plan!
 
Kina baba na Kliniki wapi na wapi? Kama mtu anataka kwenda kliniki na mwenzi wake ni hiyari yake ila wakina mama wasinyanyaswe kwa sababu hio.
 
Wanaume wengi ni wazembe sana kufuatilia afya zao. Wengine mpaka aanguke ndiyo inajulikana ana kisukari.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wanaume tunakwama wapi??
Inatakakiwa public health awareness, hili ni tatizo la dunia nzima. Nchi nyingine zimeanzisha test mfano wa MOT kwa watu wote wenye miaka 40. Haijalishi uwe wa kike au wa kiume ukifikisha miaka 40 unapata mualiko kwa daktari. Unachekiwa kuanzia PB, mkojo, uzito, nk.
 
Kina baba na Kliniki wapi na wapi?Kama mtu anataka kwenda kliniki na mwenzi wake ni hiyari yake ila wakina mama wasinyanyaswe kwa sababu hio
Wanaume wengi ni wazembe sana kufuatilia afya zao. Wengine mpaka aanguke ndiyo inajulikana ana kisukari.
Wanaume tunakwama wapi??
Nani anataka kwenda kupima na mkewe halafu ukikutwa nao aanze kuropoka? Kila mtu akapimwe kivyake na apewe "karanga" zake kivyake
  • Katibu wa uenezi wa CCM mh Polepole katika kusheherekea siku ya wanawake duniani amesema wanawake wana akili kuliko wanaume tena wana uwezo kuliko wanaume.
  • Polepole amesema kwa mujibu wa Biblia ya kiyunani mwanamke hakuumbwa kama msaidizi wa mwanamme bali aliumbwa ili kumsaidia mwanamme na mara zote mtu " anayesaidia" anakuwa na uwezo zaidi
  • Polepole amesema hata yeye wasaidizi wake wote ni wanawake kama kanali Muammar Ghadafi.
  • Mwisho Polepole amempongeza mama Samia Suluhu ambaye ni makamu wa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya.
 
Wanaume wengi wanakwepa kuwasindikiza wake zao Kliniki kwa hofu ya kupima Ukimwi. Wengi huwatanguliza Wanawake wakiamini kwamba, Kama mke akikutwa hana automatically nae atakua hana. Hata hivyo, Kuna umuhimu Mkubwa wa mwanaume kumsindikiza mke wake Kliniki hasa ya hudhurio la kwanza, kwani ni katika kipindi hicho mama na baba hushauriwa juu ya namna nzuri ya kumlea mtoto aliye tumboni. Kama mama anaviashiria vya hatari, baba nae anajuzwa na wataalam hivyo kurahisisha huduma kwa mama mjamzito kwa kipindi chote Cha ujauzito.
 
Majukumu yetu sisi akina baba ni kuwafyatulisha akina mama
 
Vitu vingine kupeana presha wana lazimisha utadhani wamepata dawa. Watu ache kina baba tuna stress zingine wasituongeze
 
Kwani mwanamke akienda mwenyewe hapewi kadi ya kliniki?

Akifiwa na mumewe mara baada ya kupata mimba je?
 
Back
Top Bottom