Pre GE2025 Wanawake wamchangia Rais Samia Milioni 120 za Fomu ya Urais. Majaliwa aongoza zoezi, asisitiza Fomu ya Urais 2025 itakuwa Moja tu

Pre GE2025 Wanawake wamchangia Rais Samia Milioni 120 za Fomu ya Urais. Majaliwa aongoza zoezi, asisitiza Fomu ya Urais 2025 itakuwa Moja tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tuna nchi ya kijinga sn, muda wote ipo kwenye kampeni, hizi fedha wangewachangia manesi waliopo pembezoni wanakesha na wagonjwa bila mapumziko

Wananchi wenyewe wako kwenye kampeni masaa 24.

Wakipoa kidogo kwenye Siasa, wanahamia TFF, upepo ukivuma wanahamia kwa Haji Manara.

Manesi wakuchangiwa ni hawa hawa waliopo Mwananyamala na Muhimbili sasa hivi?
 
Wanadamu wana akili finyu sana, wao wanajuaje ya kesho???

Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja.

Mithali 27:1

hao ni waislamu Mithali ya Biblia wataijulia wapi? wao wanaamini binadamu zaidi hawajui kwamba binadamu yuko limited wanaweza wakachanga hata mabilioni na hata asiweze kuchukuwa hiyo fomu, wawaulize raila odinga na mwenzake uhuru kenyata walijiandaa kibidanamu katika kila sekta na kila mahali lkn Mungu aliamua mwingine awe raisi …
 
Wananchi wenyewe wako kwenye kampeni masaa 24.

Wakipoa kidogo kwenye Siasa, wanahamia TFF, upepo ukivuma wanahamia kwa Haji Manara.

Manesi wakuchangiwa ni hawa hawa waliopo Mwananyamala na Muhimbili sasa hivi?
wa kwenye zahanati vijijini wanafanya kazi 24hrs mkuu, sisi wa vijijini tunajua magumu yao maana ndiyo madaktari na kila kitu
 
Mtu mmoja mtani wetu, alipitia Kila ofisi ya marafiki zake na kuchangisha pesa kuwa anafunga NDOA,

Baada ya kukusanya pesa za michango ya harusi Kwa miezi mitatu, iliwadia siku ya harusi,

Ndugu huyo hakuonekana, alizima simu, na zilipopita wiki tatu alionekana na gari mpya aina ya RAV4, tulipomuhoji kwanini hakutualika harusini, akadai mchumba alizingua, akaamua kununua gari.

Kwa kuwa michango tulitoa Kwa hiari yetu, tuliishia tu kulalama na baadae mambo yakiendelea kama kawaida.

Kiukweli,

HATOGOMBEA!!!
 
Back
Top Bottom