Wanawake wanahitaji vyeti vya kuthibitisha ubikira wao kabla ya ndoa

Wanawake wanahitaji vyeti vya kuthibitisha ubikira wao kabla ya ndoa

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Ubikira kabla ya ndoa ni muhimu kwa wasichana wengi na familia zao, wakati mwingine wanaume uomba wathibitishe ubikira wao jambo ambalo Shirika la Afya Ulimwenguni linachukulia kama ukiukwaji wa haki za binadamu.

Nchini Irani katika mwaka uliopita idadi Wairani wanaotoa wito wa kukomeshwa kwa tabia hiyo imeendelea kuongezeka.


IMG_20221111_095353.jpg

"Mume wa Maryam alimuomba amletee cheti cha ubikira maana hakutoka damu baada ya kufanya mapenzi"

"Ulinidanganya nikuoe kwa sababu wewe si bikra. Hakuna mtu ambaye angekuoa akijua ukweli."

Hivi ndivyo alivyosema mume wa Maryam walipofanya mapenzi kwa mara ya kwanza, alimhakikishia kwamba ingawa hakuwa anavuja damu, hakuwahi kufanya ngono hapo awali.

Lakini licha ya uhakikisho wake mume hakumwamini, na akamwomba atoe cheti ili kuthibitisha ubikira wake.

IMG_20221111_095704.jpg

☝🏾Wanawake wanalazimika kulipa gharama kubwa kutokana na shinikizo la jamii ya kihafidhina.

Full Story ingia hapa; 👇🏾
 
Hii ishawahi kunitokea kwa kipenzi changu J ndo ukawa mwanzo wa mtifuano wa penzi letu.....alisema yeye bikira nikaja kusikia habari zake nyeusi akasema sio kweli nikakomaa na mm kuomba mzigo ili nipate uhakika bikira ipo au laaah alinipa mzigo kwa mbonde na hakutoka damu so utata ukaanza hapo yeye anadai nimetoa bikira mm nagoma nakataa ilaa kitu kilikuwa Mnato aiseee.


Wazee ni kweli demu anaweza kuwa anasex for the first time na asitoke damu?
 
Kipimo cha Ubikra utajua tu mwanamke ukiwa unaishi nae. Kwangu mimi mwanamke bikra ni yule anayehishimu mwili wake.

Hajishughulishi na wanaume nje ya mwanaume wake. Kwangu huyu ndie bikra wa roho. Mambo ya kuhangaika na damu haisaidii kitu.

Unaweza pata binti ambaye hajawahi kuingiliwa kimwili na mwanaume yoyote ila siku umeweka ndani na umeshaoa akili zake zikabadilika na akawa kama wale wadangaji, hapo utakuwa umefanya nn?!

Muhimu ni mabinti kujitunza miili yao. Wasiingiliwe hovyo na wanaume kwa sababu yoyote ile. Kama maisha yanakulazimisha kuweka mwili rehani jua wewe ndie umechagua sio maisha.

Una uhuru wa kuishi unavyotaka.
 
Back
Top Bottom