Wanawake wanaojifungua hospitali za umma, wanadhalilika, usalama na stara hakuna

Wanawake wanaojifungua hospitali za umma, wanadhalilika, usalama na stara hakuna

Wangapi wenye huo uwezo wa kulipia.? Au unaongea tu ilimradi !? Wakati mleta mada kaleta hoja fikirishi ili mamlaka iweze kuboresha. !?

Usilete mzaha kwenye Mambo muhimu kama haya yanayohusu afya za watu. Na tambua kuwa, afya njema ndio mtaji nambari moja ktk ujenzi wa Taifa kiuchimi, kijamii na kila kitu.
 
Nimefika hospitali 1 ya serikali nilimtembekea rafiki yangu ( wa kike) aliyefika kujifungua nimesikita mno

Wodi imejaa wajawazito na vichanga

Wajawazito wanalala chini, vitandani wanalala hadi watatu, hii sio sawa

Bora wananchi wachangie huduma ila ziwe Bora, ziwepo wodi za kutosha na wake zetu wawe na usalama na stara

Wamama wanatembea uchi kwenye ka wodi, yaani hamna stara

Labor room mtu anasukuma au anaugulia uchungu kila mtu anasukia kama analia au alikunya kila mtu anajua

Serikali imeamua kuwadhalilisha wanawake

Serikali kuweni tu wawazi na waungwana kama sera ya kujifungua Bure haitekelezeki Toka ianzishwe

Mbona wananchi wanalipia huduma zingine zinazotolewa na Serikali Bure kama umeme na maji na wamezoea wala hawalalamiki

Mtu unamwaminisha kujifungua ni Bure ila gharama zinamtoka na usalama wake na mtoto unakuwa mdogo
Wapi huko kujifungua ni bure?
 
Hospitali zipo kwenye majimbo, na majimbo yana wabunge pamoja na viongozi wengine, je hawa wamejichanga kiasi gani katika kulimaliza hilo tatizo, ikiwa ni sehemu ya uzalendo?​
 
Mtoa mada anaweza akawa yupo sawa. Mana wife kashawai niambie hiki kitu ni kweli kabisa tena bila kificho ngoja nitaje tu hapa hapa dsm kimara mwisho hapo kuna zahanati ipo barabarani ina mpaka kunguni na wanalala wawili kitanda kimoja na waja wazito
 
Back
Top Bottom