Wanawake wanaoomba pesa kwenye mapenzi sasa hivi ndio wanaitwa TAMISEMI?

Wanawake wanaoomba pesa kwenye mapenzi sasa hivi ndio wanaitwa TAMISEMI?

Na kinachofurahisha na kusikitisha kwa pamoja, usipompa hiyo hela anakuona masikini lakini yeye ambae hawezi kumudu mahitaji yake mwenyewe hajioni kama ana shida yoyote
Acha hilo, mnaweza mkawa hampishani hata huo mshahara na anajua hilo, lakini bado haitakufanya usipate meseji za baby naomba hela ya.....
 
Na tuna Birthday mara mbili au tatu kwa mwaka, u never know who might surprise you a car😌
Kuna wakati nilikuwa nashangaa status nahisi naona kama mtu ameposti birthday mara mbili ndani ya mwaka mmoja nikawa nahisi labda nimeona vibaya tu kumbe nilikuwa sahihi! Hii nayo kumbe ni mbinu ya mawindo mjini!
 
Unaweza ukatamani sana kutoka na hao watoto wa kishua, classic and all. Swali ni Je, una access nao..? Unakutana nao? Huwezi ukatamani kitu ambacho hakipo kwenye mzunguko wa maisha yako.
Huyo kaongelea ku-date, sio mitoko. Wapo mabinti wa kishua ambao hawaba mambo ya party party. Ukimwendea unampata lakini usiwe choka mbaya kabisa. Lakini binti ya kishua halafu partying girl huyo mwenzangu na mimi hauwezi kumpata.
 
Ukweli ni kwamba unadate na mtoto wa kishua kwa sababu hata wewe unazo au unatoka familia ya kishua, zali(zari) la mentali la Prof Jay ni zari tu, ni wachache wanabahatika.

Sisi masikini tuendelee kukutana na masikini wenzetu, tuzidi kulialia maana ukweli wadada wanaomba sana miaka hii. Wanaongeza soko la kuuza na kununua maana kujiattach na mwanamke ni kujitafutia umasikini zaidi.
 
Ni wajibu mwanaume kumpa huduma mwanamke, na kama unajihisi huwezi basi muache ahudumiwe na wazazi wake au ajihudumie mwenyewe, kisha wewe jaza form ya kujiunga na akina Mbaga Jr
Bahati mbaya ukiangalia uhalisia kwenye uchumi wetu hali ni tofauti. Tunavyowaaminisha wanawake wana haki ya kutimiziwa mahitaji yao na wanaume pia tuangalie kama hali za vijana wetu zinaruhusu kumudu maisha yao na kujiongezea mzigo wa kugharamia na maisha ya mwanamke. Vinginevyo vijana wataona ni bora kununua, na wanawake nao wataona ni bora wawe hata 10 kwa mwanaume mmoja mwenye hela
 
Ni wajibu mwanaume kumpa huduma mwanamke, na kama unajihisi huwezi basi muache ahudumiwe na wazazi wake au ajihudumie mwenyewe, kisha wewe jaza form ya kujiunga na akina Mbaga Jr
Tunakubali 100%, ndio maana tunasema kuna machangudoa wa aina mbili, wale wa barabarani na wale wa sms, na ni wajibu wa mwanaume kulipia huduma wanazompa.

Ila wale wasio wa huduma huwa wanatuambia "baby leo nimeifuma bonus weekend hii nataka nikutoe". Hao ndio tunaooa, sio hao wa baby naomba hela ya birthday ya rafiki yangu
 
Kuna wakati nilikuwa nashangaa status nahisi naona kama mtu ameposti birthday mara mbili ndani ya mwaka mmoja nikawa nahisi labda nimeona vibaya tu kumbe nilikuwa sahihi! Hii nayo kumbe ni mbinu ya mawindo mjini!
Mbinu ziko nyingi sana! Usione watu hawalali njaa ukanifiri bure!😁
 
Kuna wakati nilikuwa nashangaa status nahisi naona kama mtu ameposti birthday mara mbili ndani ya mwaka mmoja nikawa nahisi labda nimeona vibaya tu kumbe nilikuwa sahihi! Hii nayo kumbe ni mbinu ya mawindo mjini!
Ushaona status ya mwanamke mtu mzima imeandikwa.

SI AJITOKEZE MTU ANIULIZE NINATAKA NINI, NIMTAJIE SHIDA ZANGU ZOTE.
 
Kuna wakati nilikuwa nashangaa status nahisi naona kama mtu ameposti birthday mara mbili ndani ya mwaka mmoja nikawa nahisi labda nimeona vibaya tu kumbe nilikuwa sahihi! Hii nayo kumbe ni mbinu ya mawindo mjini!
Wewe kama feminist wa kiume, unalizungumziaje hili suala la mtoto wa kike na wa kiume kupewa fursa sawa kwenye kila kitu halafu wakija mtaani mtoto wa kike awe mzigo kwa mtoto wa kiume? Je haki sawa ina tija kwenye jamii yetu?
 
Back
Top Bottom