Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 5,921
- 19,772
Kwa miongo mingi sana mwanamke kote duniani alionekana ni kiumbe dhaifu, dhalili, kisichojiweza wala kujielewa, ndio maana wakakinyima elimu, uhuru na hata utashi hii yote sio kama mwanamke alikua hivyo walivyomchukulia, waliona mbali, wakamuogopa, ukweli ni kwamba mwanamke ni Jasiri, Shupavu, Mkakamavu na mwenye Akili sana, baada ya hadithi ya Adam na Eva hapo ndipo walipomuogopa mwanamke na kuweka mfumo dume, kumfanya mwanaume awe ndie kila kitu na mwanamke awe dhaifu, walifanikiwa kupandikiza hilo lakini kama kawaida asili (mother nature) hua haikosei, sasa mwanamke anaanza kuijua nafasi yake duniani, mwanamke anaanza kutanua mbawa zake, mwanamke anaanza kutetemesha wanaojiita majabari na marijali,
Wakati raisi Samia anapokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake kila mtu alisema "huyu mwanamke hawezi kuongoza, huyu mwanamke ni dhaifu, huyu mwanamke analegeza macho na sauti," wengine wakaenda mbali zaidi na kusema "tutavamiwa na maadui zetu sababu huyu mwanamke hajui mbinu zozote za kivita, hajui kuwakemea na kuwakaripia maadui" hahahahaha wale wale leo wamegeuka na kusema "huyu mwanamke amekua mkatili, huyu mwanamke hana huruma, huyu mwanamke anatuuza" wanashindwa tu kusema ukweli kua wamekutana na chuma cha pua, mwanamke shupavu na hodari, amewatingisha mijanaume yenye ndevu zao na makoromeo yao, nchi imetulia tuliiiiii, kila mtu kawekwa kwenye kiganja cha mkono laini wa mwanamke Samia Suluhu, hawafurukuti,
Ahsante Rais Samia umetuonesha kua utawala wa mwanamke sio wa kubezwa, umetuonesha kua mwanamke akitaka lake linakua, umetuonesha kua mwanamke hatunishi misuli wala kufoka foka ili mambo yaende, mwanamke anaendeshwa na nguvu ya asili nguvu ambayo walijaribu kuificha kwa miongo mingi na sasa inaanza kujitokeza,
Hii ni list ya Wanawake shupavu walioibadilisha dunia,
1. Rosalind Franklin (mgunduzi wa DNA)
2. Mae Jemison (mwanamke wa kwanza mweusi kwenda angani)
3. Katherine Johnson (mtaalam wa hesabu)
4. Indira Ghandi (ushawishi wake kwenye siasa unajieleza hadi leo)
5. Margaret Thatcher 'iron lady' (misimamo yake mikali kwenye siasa haiwezi kusahaulika)
6. Angela Merkel (utamsahau vipi huyu mwanamke shupavu aliyewatikisha mabeberu na sharubu zao)
7. Waangari Maathai (mwanaharakati shupavu, jina lake litaishi sana)
8. Samia Suluhu Hassan (Rais wa kwanza mwanamke Tanzania, shupavu asiyeyumbishwa)
9. List ni ndefu sana kwa leo naishia hapa
Kama tulivyokubaliana Samiaaaaaaaaa mitano tenaaaaaaaaaaaaaaaaaa🖐
Soma hii pia
www.jamiiforums.com

Kaeni Mguu Pande, Zama za Utawala wa Mwanamke Duniani unakuja
[emoji253] Mwanamke wewe ni wa Thamani sana, wewe ni Imara mwenye Nguvu, wewe ni mlango wa Uhai, Wanakudanganya eti umetoka kwenye ubavu wa Adam kwa hiyo wewe ni Dhaifu, hapana alikuwepo Adam peke yake lakini akaonekana hatoshi kuipendezesha Dunia, ukaja wewe na Dunia ikapendeza, [emoji253]...